Huyu Gentamycine wa JF ni nani haswa?

Ningetamani Gentamycine ajitokeze mwenyewe ila naona anakulatu chabo sehemu akitusikiliza.
 
Kuna id ilianzisha uzi kama huu akaambiwa yeye ni genta... anajipa promo, ile id iliyeyuka haikurudi tena.

Sasa wewe sikuelewi unatarajia nini
 

Amoxacyline unajitekenya hapa.
 
umeamua kujifungulia uzi mwenyewe na kujisifia ? kweli multiple IDs hazijawahi kumuacha mtu salama....
huyo unaemsifia ambaye ni wewe ni ndezi tu

Nawaomba Moderators na Wamiliki wa JamiiForums fanyeni ' Utaalam ' wenu wote mnaoujua na kama ikiwa ni kweli Mimi GENTAMYCINE nina hii ID na nimejianzishia huu ' uzi ' mnifungie ' permanently ' Mimi kuwepo humu Jamvini. Halafu ifike muda Watu muache chuki na uswahili uliotawaliwa na Wivu kwa kudhani kuwa Mtu yoyote anayeuliziwa humu basi anajipigia ' Promo '. GENTAMYCINE sina haja ya Kujipigia ' Promo ' kwani Mimi tayari ni ' Promo ' tosha na ni maudhui yangu na uandishi wangu humu ambao mara nyingi huwa nauchanganya na ' ukomedi ' wangu wa asili ndiyo huwavutia Watu wengi hadi kupelekea Wao Kunipenda, Kunikubali na wengine kila Uchao ' Kunifolo '.

Na ndiyo maana hata Signature yangu tu inamajibu ya kutosha Kwenu ' Wanafiki ' wote inayosema ' Purely Talented and Charismatic Fella '.

Aliyebarikiwa kabarikiwa tu halafu ' Nyota ' ya Mtu inayong'aa kila Kukicha huwezi kuizima hata ufanyeje na msinichukie Mimi kuwa Kipenzi cha Members wengi hivi bali jiulizeni nyie ' mnaonichukia ' na kusema huu ' uzi ' nimejianzishia mwenyewe kwamba kwanini hamkubaliki kama GENTAMYCINE huku wengine mkiwa na muda mrefu humu JamiiForums kuliko Mimi niliyejiunga rasmi humu mwaka 2013.

Na kwa taarifa yenu tu ni kwamba kadri mnavyozidi ' Kunichukia ' na kunionea ' Kijicho ' humu ndiyo mnazidi kunifanya niwe ' maarufu ' na niwe mbunifu wa kuja na mada mbalimbali motomoto ambazo zinazidi kunifanya niwe tofauti na nyie. Waswahili ni Waswahili tu siku zote.

 
Ni mwanafunzi wa form two
 
Ningetamani Gentamycine ajitokeze mwenyewe ila naona anakulatu chabo sehemu akitusikiliza.

Soma post yangu # 56 nimewajibu ' Wapuuzi ' wote na labda nikupe tu pole Wewe Mkuu kwa kuanzisha ' uzi ' wa Kunisifia na Kunikubali ambao kuna Watu wenye chuki, wivu na husuda na uwepo wangu humu na hii ID wamekasirika na kudhani kuwa Mimi ni Wewe na kwamba nimejianzishia mwenyewe huu uzi.

Na nimewataka Moderators na Wamiliki wa JamiiForums wafanye ' Uchunguzi ' wao wote na kama ikiwa ni kweli kwamba Mimi ndiyo mwenye hii ID basi nawaruhusu upesi sana wanifute Mimi kuwepo humu Jamvini Kwao milele daima. Nimechoka kuzushiwa kila uchao kuhusu Multiple ID's na labda nikuambie tu kwamba kama ungeanzisha huu uzi wako na kunisema au kunizungumzia Mimi vibaya hizo hisia za kwamba Wewe ndiyo Mimi na nimejianzishia uzi usingezisikia. Nyota yangu inawatesa mno Watu na ndiyo maana nawaambia kuwa GENTAMYCINE ni ' Purely Talented and Charismatic Fella '.
 

' Purely Talented and Charismatic Fella '
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…