PostGE2025 Huyu hapa anadai eti Mama Abduli alisikitishwa, na alilia, kutokana na mauaji ya OCT 29

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
..Ndio mpaka WATOTO wauwawe?

..Hivi mmekaa chini mkatafakari unyama uliotokea?
Vita havina macho, kama kuna watoto wamekufa, ilikuwa ni bahati mbaya tu wamefika kwenye eneo la vurugu,Israel kila siku anaua watoto huko Gaza kwa mabomu. Marekani alipiga bomu shule iran na kuuwa watoto zaidi ya 200! Hayo ni mambo yanayotokea kwenye machafuko yoyote,
 
Kwa hiyo unaona sawa kama Israel. Inaua Wapalestina na Marekani wanaua Wairan basi hata sisi kuua RAIA.. Ebu ache mkuu hayakukuta wewe na familia yako wala usiombee vita.

Kwenye hili, Serikali yetu ilifanya makosa makubwa ya matumizi ya nguvu tena kwa raia wasokuwa na silaha. Haipendezi hata kuzungumziwa ni AIBU..
 
Sema Watanzania, tumeshagawanywa Kisiasa na sisi mazuzu tumekubali Serikali ya Samia wameua kwa sababu yeye sio Mtanganyika.

Unajua sasa hivi Europe yote maandamano ya Wanafunzi wanabeba bendera ya Palestine kama Symbol of General Resistance?

..Ccm imevishawishi na kuvichochea vyombo vya dola kuwafanyia kazi chafu.

..Kama unafuatilia siasa zetu lazima ungeona kulikuwa na hali ya Polisi kuwakamia wapinzani na wanaharakati.

..OCT 29 ilitanguliwa na matukio kadhaa ya Polisi kutumia nguvu iliyopitiliza dhidi ya wapinzani.
 
Huko ufaransa walikufa polisi wangapi, oct 29 watu wanavamia vituo vya polisi, kuua polisi na kuiba silaha, ulitaka wafanywe nini?
Kwa hiyo hadi watoto wadogo walivamia vituo vya polisi na kuiba silaha,embu jaribu kuwa na utu hata kama unatetea ugali wako ila sio kwa staili hii.Najua weledi wa vyombo vyetu na kwa teknolojia ya sasa vilipaswa kutumia mbinu mbadala kupambana na hao unaosema walileta vurugu bila kupoteza uhai wa watu.Tusipande mbegu mbaya ya kuzoea kumwaga damu za watu kwa sababu nyepesi kama hizo,mbegu hiyo ikimea na kuota matokeo yake ni mabaya sana na tujiulize kama tuko tayari kupokea matokeo yake.Pia kwa weledi wa kisasa na mbinu bora za polisi wa Ufaransa umesaidia kupunguza vifo vya polisi na idadi ya waandamanaji waliokufa,ndio maana husiki idadi kubwa ya vifo.
 
Kwa hiyo unaona sawa kama Israel. Inaua Wapalestina na Marekani wanaua Wairan basi hata sisi kuua RAIA.. Ebu ache mkuu hayakukuta wewe na familia yako wala usiombee vita.

Kwenye hili, Serikali yetu ilifanya makosa makubwa ya matumizi ya nguvu tena kwa raia wasokuwa na silaha. Haipendezi hata kuzungumziwa ni AIBU..
Sijaombea vita, na kifo sio kitu kizuri hata kidogo, naujua uchungu wa kufiwa, ninachotaka kusema, ni nani hasa alianzisha hizi vurugu za uchaguzi, waliofanya vurugu na kuchoma vituo vya polisi, stendi za mabasi, kukata wapiga kura vidole ndio wakulaumiwa, lakini cha ajabu hawa walioleta vurugu zote hizo hawalaumiwi, wanaonekana walifanya sawa, wanaolaumiwa ni polisi waliotuliza hizi vurugu. Hapo bdio mnaposhangaza
 
..Ccm imevishawishi na kuvichochea vyombo vya dola kuwafanyia kazi chafu.

..Kama unafuatilia siasa zetu lazima ungeona kulikuwa na hali ya Polisi kuwakamia wapinzani na wanaharakati.

..OCT 29 ilitanguliwa na matukio kadhaa ya Polisi kutumia nguvu iliyopitiliza dhidi ya wapinzani.
Yes, nilifuatilia lakini bchinza.Magharibi vyama vya Siasa havianzishi maandamano, wala kushawishi Wananchi wafanye Maandamano. Jumuiya za Wananchi wenyewe ndio huamua.tatizo.la nchi zetu, vyama vya Siasa vimeshiriki mara zote kuhamasisha Maandamano. Hili ni kosa kubwa la Kisiasa kwa sababu Vyama vya Siasa vyote ni sehemu ya DOLA

Sisi tunajitenga na Dola ni Vyama Kinzani na Chama tawala na Dola. Na sababu kubwa ni kutokana na Viongozi wote wa siasa Tanzania sio Wanasiasa hawana elimu ya Siasa ila wamebeba kofia za Siasa.
 
Sijaombea vita, na kifo sio kitu kizuri hata kidogo, naujua uchungu wa kufiwa, ninachotaka kusema, ni nani hasa alianzisha hizi vurugu za uchaguzi, waliofanya vurugu na kuchoma vituo vya polisi, stendi za mabasi, kukata wapiga kura vidole ndio wakulaumiwa, lakini cha ajabu hawa walioleta vurugu zote hizo hawalaumiwi, wanaonekana walifanya sawa, wanaolaumiwa ni polisi waliotuliza hizi vurugu. Hapo bdio mnaposhangaza
Kwa hiyo mkeo akianzisha vurigu ndani ya nyumba, akachoma hata nguo zako, utaua?
 
Kwa hiyo hadi watoto wadogo walivamia vituo vya polisi na kuiba silaha,embu jaribu kuwa na utu hata kama unatetea ugali wako ila sio kwa staili hii.Najua weledi wa vyombo vyetu na kwa teknolojia ya sasa vilipaswa kutumia mbinu mbadala kupambana na hao unaosema walileta vurugu bila kupoteza uhai wa watu.Tusipande mbegu mbaya ya kuzoea kumwaga damu za watu kwa sababu nyepesi kama hizo,mbegu hiyo ikimea na kuota matokeo yake ni mabaya sana na tujiulize kama tuko tayari kupokea matokeo yake.Pia kwa weledi wa kisasa na mbinu bora za polisi wa Ufaransa umesaidia kupunguza vifo vya polisi na idadi ya waandamanaji waliokufa,ndio maana husiki idadi kubwa ya vifo.
Hivi huko Gaza na Iran watoto wanavouwawa na majeshi ya Israel na Marekani, hao watoto wana makosa gani? Na wao ni wanajeshi? Kuwa muelewa, kunapotokea machafuko, hata wasiohusika, kwa namna moja au nyingine wanaathirika, kutokana na uwepo wao eneo la tukio kwa bahati mbaya, hakuna askari alieenda nyumbani kwa raia na kuua watoto. Hao walikufa kutokana na uwepo wao mtaani kwenye eneo la machafuko, na huwezi kuzuia jambo hilo
 
Sijaombea vita, na kifo sio kitu kizuri hata kidogo, naujua uchungu wa kufiwa, ninachotaka kusema, ni nani hasa alianzisha hizi vurugu za uchaguzi, waliofanya vurugu na kuchoma vituo vya polisi, stendi za mabasi, kukata wapiga kura vidole ndio wakulaumiwa, lakini cha ajabu hawa walioleta vurugu zote hizo hawalaumiwi, wanaonekana walifanya sawa, wanaolaumiwa ni polisi waliotuliza hizi vurugu. Hapo bdio mnaposhangaza
Polisi wanalaumiwa kwa sababu wako hai, unaosema walileta vurugu wote waliuawa. Wasingeuawa nao tungelaumiwa.
 
Kwako uhai wa binadamu hauna thamani,vyenye thamani zaidi kwako ni vituo vya mabasi,polisi,petrol station na mali za watu ndio maana unatushangaa sisi tunaotetea uhai wa watu.Kulikuwa na ulazima gani wa kutumia silaha za moto tena nzito kweli zenye uwezo mkubwa sana kwa raia wasio na mafunzo wala silaha nzito kupambana nao,narudia kusema sidhani kama vyombo vyetu havikuwa na mbinu mbadala ya kupambana na raia kuzuia vurugu hizo bila kufanya mauaji ya watu wengi vile.
 
Na raia waliokatwa vidole kwa kupiga kura hawana thamani sio? Hao waliokuwa wanakata raia vidole ulitaka wachekewe sio, ulitaka nchi nzima watu wawe na vilema vya kukatwa vidole na hao wahuni?
 
Hakukuwa na maandamano, acha kupotosha, bali kulikuwa na watu waliojiandaa kufanya vurugu na machafuko, vituo vya mafuta, stendi za mwendokadi, vituo vya polisi , vituo vya kupigia kura vilichomwa na nani? Unavamia kituo cha polisi na kukichoma moto ulitaka wachekewe tu, ni nchi gani duniani ingekubali hilo?
-Kazi ya polisi ni kuua au kuzuia uhalifu???
 
Back
Top Bottom