Huyu hapa anayetazamiwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza mwenye Asili ya Asia

Huyu hapa anayetazamiwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza mwenye Asili ya Asia

Wazazi wake ni Kenya Baba na Mama Ni Tanzania

Sasa Mama akiwa muhindi wa Tanganyika na Baba muhindi wa kenya ambao wote walihamia uingereza miaka ya 1960 na jamaa kazaliwa uingereza yaani mkiitaja Tanzania ambayo inakataa uraia pacha kwa raia wake inasaidia nini? Au kuitaja kenya kutasaidia nini? Kama sio utumwa wa fikra mchana kweupe? Jamaa ni muingereza story za mara Tanganyika mara kenya mnabaki nazo wenyewe kamwe hatonufaisha hizi nchi kwa lolote afadhali ungesema hata India kwenye roots zake vizazi na vizazi lakini sio tofauti
 
Rishi Sunak pichani chini anategemewa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza.
View attachment 2396584

Sunak alizaliwa katika mji wa Southampton mnamo mwaka wa 1980.

Wazazi wake wana asili ya nchi ya india, walihamia nchini Uingereza wakitokea nchini Tanzania kwenye miaka ya 1960.

Huyu jamaa ndiye anatizamiwa atakuwa Waziri mkuu mwenye asili ya india na wa kwanza kushika madaraka hayo makubwa nchini Uingereza.
Labda
 
Ulishaona mtanzania mhindi??? hao wahamiaji tu, ni sawa na mtu mweusi kujiita ni muingereza hapana ni muafrika tuu. Kwahio huyu ni mhindi na hajazaliwa Tanzania pia. Kwa kifupi haijui hata hio Tanzania ilipo,.

Ni yale ya waafrika kushabikia obama kua Rais ujinga ulioje? Obama mmarekani wewe zuzu wa buza unajifanya kushangilia itasaidia nini nchi yako? Halafu blacks hua tunapraise mtu mwenye kitu mbona hatukuwahi kumjadili hapa akiwa hajagikia level hiyo?
 
Acheni ushamba mbona Fred Mecury alikua staa mkubwa duniani na alizaliwa hapo wanakojambia "jambiani"😂, Zanzibar! Na anatambulika kama raia wa uingereza mwenye asili ya India
 
Huyu mhindi, acheni upotoshaji eti ana nasaba ya Tanzania. Watanzania wa kuzaliwa waturutumbi mnawanyima uraia pacha mnajidai huyu mhindi ni ana nasaba ya Tanzania... Kazaliwa Uingereza ni muingereza mwenye asili ya India....period.
Kanda ya ziwa....eti waturutumbi 😅😅😅
 
Rishi Sunak pichani chini anategemewa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza.
View attachment 2396584

Sunak alizaliwa katika mji wa Southampton mnamo mwaka wa 1980.

Wazazi wake wana asili ya nchi ya india, walihamia nchini Uingereza wakitokea nchini Tanzania kwenye miaka ya 1960.

Huyu jamaa ndiye anatizamiwa atakuwa Waziri mkuu mwenye asili ya india na wa kwanza kushika madaraka hayo makubwa nchini Uingereza.
Waziri mkuu lazima awe muanglikana, sijui itakuwaje
 
Ulishaona mtanzania mhindi??? hao wahamiaji tu, ni sawa na mtu mweusi kujiita ni muingereza hapana ni muafrika tuu. Kwahio huyu ni mhindi na hajazaliwa Tanzania pia. Kwa kifupi haijui hata hio Tanzania ilipo,.
Acha uboya kina Dewji familia yao ilihamia hapa miaka ya 1800's kutoka Gujarati, vivo hivo kina Karimjee. Sasa utasemaje leo kina Mwamedi Dewji sio watanzania wakati wamezaliwa hapa na wengekua hawana pesa hata India wasingewai fika!
 
Hili linawezekana nchi za Afrika?
Jibu liko wazi kabisa!

Katika jamii za watu waliostaarabika, asili ya mtu haina uhusiano wowote na utendaji kazi wake katika wadhifa anaokabidhiwa.

Ni jamii zenye fikra duni pekee ndizo ambazo zinaweza kutumia asili ya mtu kama kigezo cha kumkataa mtu ama kumchagua mtu kushika nafasi ya uongozi kitaifa ama kitaasisi.
 
Nilipoona Tanzania nimechekaa kwa hiyo ndugu yetu 😂😂
 
Back
Top Bottom