Huyu Hapa ndo aliyeokoa maisha ya Tundu Lissu pale Dodoma, sio Mbowe

Huyu Hapa ndo aliyeokoa maisha ya Tundu Lissu pale Dodoma, sio Mbowe

na kwa technology inayotumika MNH kwa sasa, nashauri awahishwe NAIROBI ili baadae asogezwe nchi zenye advanced technology." akasisitiza "Ushauri huu ni wa kitaalam nashauri uzingatiwe
Ndio maana sirudi tena huko mavumbini....
Nafia hukuhuku kwa watwana....
 
Mimi ni mchaga lakini mbowe ametudhalilisha sana wachaga haiwezekani kulialia na kukumbushia msaada uliompa mtu kisa tu anataka nafasi yako has if huo msaada ulikua deni hakujifunza hata kwa mzee mengi amesaidia wengi lakini hakuwahi kuwahikumu hata wale waliozuia maslahi yake? Huyu mbowe mshamba sana kwa mwendo huu ni mbora nirudi ccm tu
Kwani Mtemi Kimweri alikuwa mchaga?
 
Na wewe umekubari kwamba ubalozi ni kutumbuliwa??
Lakin mkuu huyu ulisubsya ni mtaalamu wa afya hospitali, ndipo eneo lake la ujuzi linamuhitaji, sasa ubalozi ambao mm nautafsiri kama siasa wapi na wapi?

uoni kama haikuwa sawa?
 
Taarifa zilipofika Bungeni, chap watu wakawahi eneo la tukio kisha Hospital.

Kufika Hospital, Katibu Wizara ya Afya wa wakati huo , this great man , Dr. Ulisubisya , Daktari wa Kuua na Kufufua ( Anesthesiologist)akawahi kuingia Theater for bleeding management and major first aid akishirikiana na general physician waliokiwepo zamu.
-
Wadau wengine akiwemo mbowe , chadema na baadhi ya viongozi wa CCM akiwemo Ndungai wakabaki nje ya Hospital wakifacilitate communication ili Lissu awahishwe Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.


After few hours, Daktari wa Kuua na Kufufua, akatoka Theater na kwenda kwa wadau, Ulisubsya does not speak so much , ana sauti nzito kidogo na niliwahi kufanya nae kazi, na alikuwa ni mmoja wa waliosaini my docs nilipokuwa naondoka

Aliwauliza wadau WHAT NEXT ? Plan zmekaaje?

Mbowe na Ndungai wakajibu tumekubaliana awahishwe MNH.

Dr. Ulisubsya, ni mtu mwenye HESHIMA... akawaambia "vema lakini ninaomba kushauri; kwa hali niliyomkuta nayo LISSU na kwa technology inayotumika MNH kwa sasa, nashauri awahishwe NAIROBI ili baadae asogezwe nchi zenye advanced technology." akasisitiza "Ushauri huu ni wa kitaalam nashauri uzingatiwe"

Ndio chap chap simu zikaanza kutembea kupata vibali na ndege to Nairobi....aliyefacilitate zoezi zima la kupata ndege ni aliyekuwa mkurugenzi wa mamlaka ya viwanja vya ndege wa wakati ule.

Wakati huo JPM anasubiri Lissu aletwe MNH na akaahidi serikali itagharamia matibabu yake; Job Ndungai anampa Taarifa JPM kuwa Lissu amepelekwa Nairobi,!

JPM akauliza why ? Job akamjibu

"Ulisubsya ameshauri hivyo na ndio alisimamia zoezi zima na ameonesha kuwa MNH inatumia technology ya zamani kwenye treatment"

Hii kitu ilimuudhi sanaJPM , akasema :

"bunge lisigharamie matibabu yake"

Chap akala kichwa
Cha Ulisubsya na kumwambia kwamba unasafiri snaa nje hata safari za kuwapa watendaji wako wa chini unaenda wewe.

akawa anatakiwa kwenda pale wizara ya mambo ya nje kunywa chai asubuh na kusoma magazeti bila ya kukosa kila siku.

Gharama za matibabu ya Lissu zilichangwa na wadau wengi akiwemo Samia Hassan, aliyekuwa makamu wa Rais wa kipindi kile.

Mbowe alishiriki kama walivyoshiriki viongozi wengine wa Chadema na CCM kwenye ku facilitate zoezi zima.Mbowe alishakuwa ameingia kwenye mtego wa kumpeleka Lissu MNH.

Kama sio Ulisubsya na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege wa wakati ule..... probably we would not have Lissu today .

Siwezi kusema Mbowe hakuwa na Mchango, bali mbowe alikuwa na mchango kama walivyokuwa na Mchango viongozi wengine wa Chadema na CCM . In truth , Maisha ya Lissu yaliokolewa na viongozi yaani government officers ambao walikuwa kwenye position kubwa ya kusaidia na sio Mbowe that is hard truth ...

.. Champion aliyetoa idea ya kitabibu akiwa Ulisubsya of which it costed him .... Champion namba 2 akiwa yule mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege.hawa ndio game changer .....and never Ulisubsya kuwahi kuzungumzia hili swala.....kama nilivyosema Jamaa haongei sana wala sio mtu wa Media kama Mwafulani. Anajua ethics za kazi zake and he is very much composed. Hata alivyotumbuliwa … hakuwahi ku comment anything . His mouth was always sealed🤐

kama ilivyo wana siasa Mbowe ndio akaanza kuonesha nimeokoa maisha ya Lissu. Big Liar and it is a shame kuona jamaa anaongea maneno kama hayo kuwa ameokoa maisha ya Lissu akisahau dunia ya sasa kila kitu kipo wazi.


Dr Megalodon
WHO Regional Office,
Rue 52, Ottawa
Canada

View attachment 3196694
View attachment 3196695
Hakika Leo umeongea ukweli Wengi walioogopa Kuusema..
Asante
 
Mwanafyale, nenda youtube kaisikilize ile hotuba ya Lissu bungeni masaa machache kabla hajapigwa risasi, aliyekua ana chair kikao cha bunge that day alikua dada yako, nenda kamtazame vizuri sister halafu njoo tena usifie Wanyakyusa wenzio. Sister that day alikua poa sana na siku zingine
Yulia Sio Mnyakyusa ni Manyafu
 
Ni kina nani walihakikisha lissu mpaka kukutana na dokta na pia kupelekwa Nairobi ?
Ndio anawadanganya hivi? Connection ya ma dr inapatikana kwa ma dr
Vitu vingine mnatakiwa ku Reason tu

Wanasiasa ni wahuni kama unavoona kwa sasa wanaunguzana kwenye media
 
Mbowe kwa sasa anatapatapa, anajaribu kushika popote ilimradi ajiokoe...hakujifunza kusoma alama za nyakati au pengine wapambe nuksi maslahi ndio wamempotosha kugombea awamu ingine baada ya miaka 21 madarakani.
Alishazoea kucheza rafu na akawa anafanikiwa. Hakukuwa na refa wa kuziona rafu zake na kuchukua hatua stahiki. Akadhani na safari hii umafia wake utaendelea. Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Umafia wake umefika kikomo. Angekuwa muungwana angesoma alama za nyakati na kukaa kando kwa heshima.
 
Mimi ni mchaga lakini mbowe ametudhalilisha sana wachaga haiwezekani kulialia na kukumbushia msaada uliompa mtu kisa tu anataka nafasi yako has if huo msaada ulikua deni hakujifunza hata kwa mzee mengi amesaidia wengi lakini hakuwahi kuwahikumu hata wale waliozuia maslahi yake? Huyu mbowe mshamba sana kwa mwendo huu ni mbora nirudi ccm tu
Wewe mchaga keyboard yako ina shida gani aiseee
"has if"
"Ni mbora"
"Kuwahikimu"

Na pia majina ya watu na mahali huwa tunaanza na herufi kubwa, Mbowe, Mengi ...
 
Nakubaliana na wewe Mkuu

Ndiyo maana Juzi akiwa uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Lissu alisema kitu cha namna hiyo

Kwamba tunahubiri kuhusu Fulani ni mfanyabiashara Mkubwa, lakini anafanya biashara gani isiyo na TIN, leseni, Wala anwani ya makazi

Kwa kweli Mbowe, safari hii hata kama atashinda lakini Chama chake kinaenda kupoteza credibility Kwa Wananchi
They have lose credibility already....🚮
 
Back
Top Bottom