Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Na ana kata kulia na kushoto akiwanunua watu na viwanja vyao kama hana akili nzuri.
Ukienda wilaya ya Kinondon i utamkuta yupo tele kila mahali.
Mitaa ya Goig Mbezi Beach kanunua mtaa mzima.
Kama utafika Mbezi NSSF road ile RED Hall ni yake.
Ile Kuringe Sports Bar kulekea Baraza la Mitihani haya tena, na hivyo ni baadhi tu ya vitega uchumi na viwanja alivyonunua Kinondoni.
Jina halisi la Kuringe nasikia ni somebody Edward Mushi, kijana mdogo ambaye zimemtembelea.
Nimeona hii clip mahali, nikaona nimpe ushauri wa bure.
Namshauri tu, bwana Kuringe , aste aste brother, taratibu jiji hili la Chalamila, wengi wametajirikia hapa, ila wengi pia wamefilisikia hapa DSM.
Kula na kipofu, gusa mkono wa mwanasiasa wa Kinondoni, ndo utalijua Jiji.
======
Mwekezaji Joanna Chifunda aeleza kuhusu uvamizi wa eneo lake la biashara liliopo Mikocheni kwa Nyerere Jijini Dar es salaam. Inadaiwa kwamba fremu saba katika plot namba 27 zilivunjwa na Watu waliojitambulisha kwamba wametumwa na Kuringe ambaye anadai kwamba amenunua eneo hilo baada ya kuingia makubaliano na kumlipa Mmiliki aitwaye Zacharia Maftah.
Joanna Chifunda anaeleza kwa kirefu zaidi alipofanya mahojiano na Waandishi wa habari siku ya Jumamosi, Oktoba 12, 2024 mbele ya fremu hizo zilizovunjwa.
Abdulmajid Zakaria Maftah ambaye amejitambulisha kama ni mmojawapo wa watoto saba wa mzee Zakaria Maftah akieleza kuhusu uvamizi na mgogoro wa ardhi katika eneo liliopo kwenye plot namba 27, Mikocheni kwa Nyerere Jijini Dar es salaam.
Inadaiwa kwamba fremu saba katika eneo hilo zilivunjwa usiku wa kuamkia Oktoba 12, 2024 na Watu waliojitambulisha kwamba wametumwa na Kuringe ambaye anadai kuwa amenunua eneo hilo baada ya kuingia makubaliano na kumlipa Mmiliki aitwaye Zacharia Maftah.