Huyu James Mbowe anatakiwa ajue Mbowe alisajili vipaji vya siasa CHADEMA na sio kwamba aliwatengeneza yeye

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Huyu dogo James anakosea sana kusema kuwa Mbowe aliwasaidia kina Lissu, Lema, Msigwa kuwa wanasiasa wakubwa. Mbowe alichofanya ni kama Madrid inavyosajili mastaa wa soka toka timu mbalimbali. CHADEMA iliwahitaji kina Lissu na wenzake kuliko wao walivyoihitaji CHADEMA. Kwa mfano Lema hata angeendelea kubaki TLP bado angeshinda uchaguzi 2010 Arusha mjini kwa jinsi alivyokuwa anakubalika kisiasa. Kwa wakazi wa Arusha tunajua kashfa ya Lema kuuza ushindi wake mwaka 2005. Kusema kuwa Lema kawa mkubwa baada ya kuingia CHADEMA ni uongo na upotoshaji. Hata Msigwa tayari alikuwa kashagombea ubunge na kupata kura nyingi za wana Iringa. Mimi nimeamua kuweka tu hili suala sawa kwa sababu sipendi upotoshaji wa kitoto kama huu.
 
View: https://www.instagram.com/reel/DNgYVn1te0F/?igsh=eWx2dGtrcTZ4cmZw

Hako ka James ni ka kilaza!
 
Huyu dogo James anakosea sana kusema kuwa Mbowe aliwasaidia kina Lissu, Lema, Msigwa kuwa wanasiasa wakubwa. Mbowe alichofanya ni kama Madrid inavyosajili mastaa wa soka toka timu mbalimbali. CHADEMA iliwahitaji kina Lissu na wenzake kuliko wao walivyoihitaji CHADEMA. Kwa mfano Lema hata angeendelea kubaki TLP bado angeshinda uchaguzi 2010 Arusha mjini kwa jinsi alivyokuwa anakubalika kisiasa. Kwa wakazi wa Arusha tunajua kashfa ya Lema kuuza ushindi wake mwaka 2005. Kusema kuwa Lema kawa mkubwa baada ya kuingia CHADEMA ni uongo na upotoshaji. Hata Msigwa tayari alikuwa kashagombea ubunge na kupata kura nyingi za wana Iringa. Mimi nimeamua kuweka tu hili suala sawa kwa sababu sipendi upotoshaji wa kitoto kama huu.
Mchezaji hata awe na kipaji cha aina gani anahitaji kuwa na timu bora yenye meneja mahiri ili kipaji hicho kifikie peak yake. Kipaji cha Mbowe ni kuwatambua vijana wenye vipaji, kuwavuta waingie kwenye chama chake, kuwasuka na kuwapa platform ya kuonyesha uwezo wao. Lema angeweza kushinda Arusha lakini angepwaya Bungeni.

Ni back up ya Chadema ndio iliyomfanya awe Lema wa leo. Hivyo hivyo kwa Lissu, Zitto, Heche, Mdee na wengine. Tuliona jinsi wakina Mdee walivyopwaya bungeni walipokosa back up ya Chadema.

Back up hiyo ni sekretariat ambayo ina watu wanaojua kufanya tafiti, kupanga hoja n.k. Aidha, wanasiasa wenzako wenye uwezo kama huo. Msigwa pamoja na kutamba kuwa alipata kura kuliko mgombea wa Chadema leo yuko wapi? Ukweli huu ndio unawafanya wakina Heche, Mdee na G55 waendelee kumheshimu Mbowe.

Wakati Sigrada anahamia Chaumma alielezea vizuri tofauti ya uongozi wa Mbowe. Kuwa pamoja na kumpiga Mbowe madongo, alipomuona alimkumbatia na kumwambia asiwe na wasiwasi. Alilinganisha hiyo na wakina Heche ( pamoja na kukiri mchango wa Mbowe kwake) ambao walionyesha wazi kuwa hawakupenda alivyomshukuru Mbowe katika mkutano wa Bawacha. Na walimshughulikia kisawasawa. Uongozi sio kazi rahisi.

Mimi sijasikia hata kiongozi mmoja ambae anasema wazi kuwa Lissu alimjenga kisiasa.

Amandla...
 
  • Thanks
Reactions: RMC
Huyu dogo James anakosea sana kusema kuwa Mbowe aliwasaidia kina Lissu, Lema, Msigwa kuwa wanasiasa wakubwa. Mbowe alichofanya ni kama Madrid inavyosajili mastaa wa soka toka timu mbalimbali. CHADEMA iliwahitaji kina Lissu na wenzake kuliko wao walivyoihitaji CHADEMA. Kwa mfano Lema hata angeendelea kubaki TLP bado angeshinda uchaguzi 2010 Arusha mjini kwa jinsi alivyokuwa anakubalika kisiasa. Kwa wakazi wa Arusha tunajua kashfa ya Lema kuuza ushindi wake mwaka 2005. Kusema kuwa Lema kawa mkubwa baada ya kuingia CHADEMA ni uongo na upotoshaji. Hata Msigwa tayari alikuwa kashagombea ubunge na kupata kura nyingi za wana Iringa. Mimi nimeamua kuweka tu hili suala sawa kwa sababu sipendi upotoshaji wa kitoto kama huu.

Kweli.
Waliobeba na Mbowe bila uwezo wanajulikana
 
Baada ya kupigwa Chini na Lissu u GOAT uliishia pale.
Kabisa, angestaafu kwa heshima kuliko alivyobugi akaenda kushindiwa kwenye sanduku la kura alipoteza heshima pa kubwa mnooo!
Alionekana ni mlafi wa madaraka, miaka zaido ya 20 we bado tuu hutaki kuamini kwenye wengine?!.
Yote tisa, kumi alivyoonesha dalili zote za kuwa msaliti...hapo ndio akamalizia ile heshima kdg aliyokuwa amebakiwa nayo!!.
Mbowe wa leo haaminiki teena!
 
Kama anatengeneza akaitengeneze chauma tatizo liko wapi?

Kutoka chadema hataki kwenda chauma hataki.

Kukaa hawezi kusimama hawezi.
Kwani ni lazima aende Chaumma? Mbowe ni mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CHADEMA na hawezi kuwa na cheo hicho kama sio mwanachama wa CHADEMA.

Chadema ndio wasiojua walitakalo.
Mara alituchelewesha sana!
Mara kwa nini hatutei!
Mara amelamba asali!
Mara kwa nini haonekani Mahakamani!
Mara ni Mwenyekiti Mstaafu!
Mara ni Makamu Mwenyekiti Mstaafu!

Kama hahitajiki CHADEMA mfukuzeni tu.

Amandla...
 
atajua wapi hayo yeye tu ukiangalia usoni anaonekana mweupe

Pia wakati mbowe anafanya hayo yeye alikuwa wapi pia yeye sio mtoto wa FAM
 
Kwani ni lazima aende Chaumma? Mbowe ni mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CHADEMA na hawezi kuwa na cheo hicho kama sio mwanachama wa CHADEMA.

Chadema ndio wasiojua walitakalo.
Mara alituchelewesha sana!
Mara kwa nini hatutei!
Mara amelamba asali!
Mara kwa nini haonekani Mahakamani!
Mara ni Mwenyekiti Mstaafu!
Mara ni Makamu Mwenyekiti Mstaafu!

Kama hahitajiki CHADEMA mfukuzeni tu.

Amandla...
Mbowe is Legend wa siasa za vyama vya Upinzani,watu hawashiriki sio kwa nahau za NONO bali aibu.
Mbowe kama mwanadamu yeyote anazo kasoro zake lakini mazuri au mabaya hudumu hata wakishakufa.
Mbowe ni mwamba wa siasa za Upinzani katika mazingira magumu.
 
Back
Top Bottom