Huyu dogo James anakosea sana kusema kuwa Mbowe aliwasaidia kina Lissu, Lema, Msigwa kuwa wanasiasa wakubwa. Mbowe alichofanya ni kama Madrid inavyosajili mastaa wa soka toka timu mbalimbali. CHADEMA iliwahitaji kina Lissu na wenzake kuliko wao walivyoihitaji CHADEMA. Kwa mfano Lema hata angeendelea kubaki TLP bado angeshinda uchaguzi 2010 Arusha mjini kwa jinsi alivyokuwa anakubalika kisiasa. Kwa wakazi wa Arusha tunajua kashfa ya Lema kuuza ushindi wake mwaka 2005. Kusema kuwa Lema kawa mkubwa baada ya kuingia CHADEMA ni uongo na upotoshaji. Hata Msigwa tayari alikuwa kashagombea ubunge na kupata kura nyingi za wana Iringa. Mimi nimeamua kuweka tu hili suala sawa kwa sababu sipendi upotoshaji wa kitoto kama huu.