Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Huyu mama amakuwa katika Cabinet muda sasa. Lakini wizara ambazo ameziongoza ni zile ambazo haziko mainstream, yaani hazitajwi siku hadi siku.
Lakini nilipoona uteuzi wa ma DC unakataliwa na wateule, na hivyo kumuaibisha sana mheshimiwa Rais Samia, nikajua kuna tatizo na mchakato na mamlaka za uteuzi.
Ilikuwa aibu tosha kwa Rais, anapomteua mtu, halafu mteule anasema "No Thanks"
Mchakato wa teuzi za viongozi waandamizi nchini inahusisha vyombo vingi vya uchunguzi, pamoja na kumhusisha mteule kama ataiweza kazi anayopewa.
Kwa wenzetu nchi zilizoendelea wanaenda hatua zaidi kwa wateule kuhojiwa na bunge au kamati zake.
Sasa lile sakata la wateule kukataa teuzi nikajiuliza huyu mama Jenista Mhagama , anaiweza kweli kazi aliyopewa?