ππππππna kitandani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ππππππna kitandani
Kwa kweli, siyo hivi hivi!kwa huyu, inawezekana siyo jinsia tu...hata uchawi unaweza ukawemo!
Mamlaka ya uteuzi in lawama kubwa, lakini washauri wanaohusika wizarani, hususan waziri, naye ana sehemu yake ya lawama.Ni kweli kabisa tatizo la watawala wanadhani kila mtanzania ana njaa na kwamba anatamani uteuzi ili agange njaa. Lakini tatizo hilo wa kulaumiwa sio Jenister bali wa kulaumiwa wa kwanza ni mamlaka ya uteuzi.
Daah alituahidi ajira 1700+ akiwa bungeni kutoka database kasepa bila mkeka kuachiwa.Huyu mama amakuwa katika Cabinet muda sasa. Lakini wizara ambazo ameziongoza ni zile ambazo haziko mainstream, yaani hazitajwi siku hadi siku.
Lakini nilipoona uteuzi wa ma DC unakataliwa na wateule, na hivyo kumuaibisha sana mheshimiwa Rais Samia, nikajua kuna tatizo na mchakato na mamlaka za uteuzi.
Ilikuwa aibu tosha kwa Rais, anapomteua mtu, halafu mteule anasema "No Thanks"
Mchakato wa teuzi za viongozi waandamizi nchini inahusisha vyombo vingi vya uchunguzi, pamoja na kumhusisha mteule kama ataiweza kazi anayopewa.
Kwa wenzetu nchi zilizoendelea wanaenda hatua zaidi kwa wateule kuhojiwa na bunge au kamati zake.
Sasa lile sakata la wateule kukataa teuzi nikajiuliza huyu mama Jenista Mhagama , anaiweza kweli kazi aliyopewa?
Bwana Madelu alisha thibitishia umma wa watanzania ndani ya bunge kwamba wabunge wanaelewa zaidi mambo ya uchawi kuliko hoja za kuijenga nchikwa huyu, inawezekana siyo jinsia tu...hata uchawi unaweza ukawemo!
Hapa waziri anabebeshwa lawama zisizo za kwake, kwa sasa marais badala ya kushauriwa na mawaziri wao wanawashauri mawaziri πππ mawaziri wengi nao kwa sasa mambo mengi wanakutana nayo mitandaoni kama sisi. Lakini hata hivyo waziri wa maDC ni waziri wa TAMISEMI ambaye kimsingi kabisa kama hoja ingekuwa wale maDC kugomea teuzi alitakiwa awe wa kwanza kuwajibishwa. Kwa hiyo nahitimisha tu kwamba uhamisho wa Jenister have nothing to do with alichokisema mtoa hoja bali ni mapenzi ya rais tu na kuamua kuwahamisha au ana sababu nyingine tusiyo ifahamu ila sio iyo mtoa hoja anayoifikiriaMamlaka ya uteuzi in lawama kubwa, lakini washauri wanaohusika wizarani, hususan waziri, naye ana sehemu yake ya lawama.
Alitakiwa kushauri kinachotakiwa kufanywa, kwamba vetting ihusike na kuarifu watu kabla ya teuzi kutangazwa.
Ushauri wake ukikubalika, amechangia kufanya mchakato uwe bora.
Ushauri wake usipokubalika, anapima jambo, kama ni kubwa au dogo.
Kama jambo ni kubwa, anawajibika kujiuzulu, ili asiwe katika serikali ambayo katofautiana nayo katika jambo kubwa.
Kama jambo si kubwa, aanawajibika kukubaliana na ukweli kwamba ushauri wake haujakubalika, na kuendelea kuwa katika serikali kwa kujua kwamba lawama zozote zitakazokuja zitawakumba wote serikalini.
Hiyo ndiyo "collective responsibility".
Ndio NGEKEWA yenyewe hiyo mkuu!!yaani panga pangu yumoSijawahi kuona anachokifanya huyu mama.
Yupo kwenye baraza miaka na miaka lakini hana jipya
Siyo masuala ya kimila kweli? maana hakika ana pooorrr performance ya wazi waziHakuna wizara hata moja aliyoisha iongoza ikawa na mafanikio!!ni kati ya watu wenye NGEKEWA zao tu!!!lakini hakuna kitu.
Nadhani ungeiweka kama ni hisia zako wala sio uhakika asilimia mia kwamba hiyo ndo sababu iliyomuondoa.Mkuu mamlaka ya uteuzi unatayarishiwa wateule na kuwa vet, yaani kuwachunguza kupitia vyombo vya dola.
Hapo ndio Jenistaer anahusika na kulaumiwa vile vile.
Ukishakubali kuwa katika serikali inayoteua watu kabla ya kuwaarifu, umeshakubali lawama zitakazotokana na hatua hiyo.Hapa waziri anabebeshwa lawama zisizo za kwake, kwa sasa marais badala ya kushauriwa na mawaziri wao wanawashauri mawaziri πππ mawaziri wengi nao kwa sasa mambo mengi wanakutana nayo mitandaoni kama sisi. Lakini hata hivyo waziri wa maDC ni waziri wa TAMISEMI ambaye kimsingi kabisa kama hoja ingekuwa wale maDC kugomea teuzi alitakiwa awe wa kwanza kuwajibishwa. Kwa hiyo nahitimisha tu kwamba uhamisho wa Jenister have nothing to do with alichokisema mtoa hoja bali ni mapenzi ya rais tu na kuamua kuwahamisha au ana sababu nyingine tusiyo ifahamu ila sio iyo mtoa hoja anayoifikiria
Kichwani wapi?.Namkubari sana jenista,yupo vizur kichwani
Hata taasisi na mashirika ya umma aliingilia utendaji wao na kupelekea malalamiko na utendaji mbovu,Huyo Jenister hana uwezo wote wa kuongoza wizara. Kavuruga huko utumishi na Sasa hata madaraja tu ya watumishi yemekwama hawapandi tena kwa wakati
Tatizo tunaishi kwa kukariri. Jinsi wanavyoitafuna nchi basi wanaamini kila mtu atakuwa na shauku ya kuwa sehemu ya utafunaji. Ndio maana ilikuwa jambo la ajabu sana kwa mtu kukataa teuzi.Kawaida wateuliwa huulizwa kama wanaitaka kazi kabla ya kutangazwa.
Tanzania inaonekana watu wanabambikwa kazi bila hata kuulizwa kama wanaitaka, wakitegemewa wafurahi tu kwa sababu ni uteuzi wa rais. Hili ni jambo la kijinga sana na moja ya sababu utendaji unakuwa na matatizo, mtu anapewa kazi ambayo hata hakuiomba na pengine haijui.
Na katika zama hizi ambapo wengine wana taaluma zao na biashara zao, ukimbambika mtu kazi ambayo iko nje ya malengo yake matokeo yake ndiyo unapata hayo majibu ya "No, thanks".
Rais anaaibika.
Actually aliyekataa uteuzi anajielewa vizuri zaidi.Tatizo tunaishi kwa kukariri. Jinsi wanavyoitafuna nchi basi wanaamini kila mtu atakuwa na shauku ya kuwa sehemu ya utafunaji. Ndio maana ilikuwa jambo la ajabu sana kwa mtu kukataa teuzi.
Swadakta.Na fedheha kubwa zaidi ni pale aliyekataa uteuzi kuambiwa atachukuliwa hatua za kinidhamu!