Huyu Kamanda wa Jeshi anatukera sana wakazi wa Mbezi

Huyu Kamanda wa Jeshi anatukera sana wakazi wa Mbezi

Mbona huku Segerea Banana Nyerere road
anayopita Mabeyo haina Mbwembwe hizo,japo naye kuna sehemu anapita Wrong lane lkn hajawahi leta karaha aisee Yule jamaa
 
Sana. Pale kwa Museveni yeye katikati ya msafara anaweza akasimama akaongea na simu kwanza tena akiwa ameketi katikati ya barabara kabisa huku raia wanasubilishwa kwenye foleni. Africa ni zaidi ya pasua kichwa mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Muda mwingine tunawalalamikia wazungu(Mabeberu) ila ukweli kuna ujinga sana Africa yetu
 
Sijasema hana msafara, ila sio huo wa kukuta watu eti wananing'inia na mi bunduki, mfano mzuri enzi zile za mwamunyange, waulize watu wa mbezi beach, walikuwa wanashangaa kama ni yeye ndio anapita hakuna mishemishe kabisa!! Hayo mambo ni hulka ya mtu, tu ndio maana akistafu anapata shida sana, mwisho wa siku lazima awahi kufa!! Tungepata na kabila lake huyo tungeweza kwenda mbele zaidi inawezekana analaumiwa bure tu
Ni mrangi wa Kondoa lakini ni mpole sana sidhani hicho wanachosema kama kina ukweli. Huwa anapita na msafara wake huwa hausimamishi magari.

Tofa
 
Hizo ni kero "mpya mpya" zilizojitokeza awamu hii.. Ukipita njia ya Ukonga/Tabata kuna maaskari magereza. jwtz na polisi wanataka hadhi hiyo!
Hata liwe tu basi limejaza wafungwa au askari wao, au lorry/gari linalosambaza askari ulinzi, watapita red lights, njia zisizo halali, ving'ora na honi nyingi tu!
Mbona tunakoma!
😡😡😡😡
 
Hawa jamaa kweli wanapaswa kuwa na walinzi lakini wakati mwingine wana exaggerate zaidi Kuna siku natoka hotel moja kubwa nipo nje wakatoka mp wawili mmoja anaangalia kushoto mwingine kulia yaani utafikiri tunavamiwa yaani kama wana act movie kabisa na mimi nikajisemea sijui nilale chini ku take cover maana na mimi sio wa spotispoti Basi katoka bosi na mbembwe zote zile gari likakataa kuwaka Mimi bado naangalia movie tu
Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Hahahahahaha....aise nimecheka kwa nguvu mno, kidogo nidondoke kwenye kiti, hahahahaha..
Laana za kunyanyasa raia hizo...
Hahahahahha...ni shida kwa kweli...ungerekodi mkuu tucheke zaidi...😀😀😀
 
Nadhani hapa mleta uzi hazungumzii ukubwa wa cheo chake. Issue ni ile adha anayowapa walipa kodi ambao ndiyo wanaomhudumia kunyanyaswa utadhani siyo raia wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa mkuu hata Mimi nilikuwa nataka kuliweka sawa tu yeye alijua ni brigadier general,chief of staff siku zote luten general, All in all ni changamoto za nchi ulimwengu wa tatu,Shida miundombinu yetu siyo rafiki.
Nchi za wenzetu watu kama hao wanaishi sehemu wanapofanyia kazi siyo sehemu za uraiani,Kwa wenzetu wa Tabata CDF naye changamoto kwetu ikifika SAA kumi utasikia chwiiii chwiiiii ng'oooo inabidi tukae pembeni tu mkuu.
 
Hawa viongozi wananyumba zao Osterbay na Masaki kwann hawataki kuishi huko?
Habari wana jamvi,

Kwa wale wakazi wenzangu wa Mbezi Beach, Kunduchi, Goba na watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kwa ujumla
bila shaka Mtakuwa mmekutana na huyu Kamanda wa Jeshi (Chief of Staff) ambaye kuanzia majira ya kila siku Asubuhi 12:30- 1:00 hutugandisha kwenye foleni kwa muda mrefu kila siku akisubiriwa kupita yeye na ma MPs wake wanaoning'inia kwenye milango bila sababu ya Msingi na wakati mwingine waki ning'inia na Bunduki na mavazi kama tuko Afghanistan...wakifokea watu barabarani kukaa pembeni tena wakiwa kwenye wrong Lane!

Binafsi ananikera sana, kama anahitajika kufika ofisini mapema si atoke mapema kama wengine...😡 au ndio Madaraka ya Kulevya?
Kuna siku niliwahi kuongozana na gari ya Waziri wa Ulinzi toka Uwanja wa ndege wa Dsm hadi hadi nilipofika Mwenge nao wakiwa kwenye foleni bila hamaki wala papara.

Hebu mfikishieni salamu huyu Kamanda, awaambie walinzi wake kuwa wastaarabu na kutotukera wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sio uongo
mimi binafsi wakati nasoma Tambaza high school 2003 tulikuwa tunamuona CDF General george waitara na gari yake 4 star akiingia ngome kila siku hakuwa ma vingora wala mbwembe kama za siku hizi, tuliwahi kumpungia mkono na yeye akarudisha salamu.
mwaka huu nilikutanana chief of staff YH Mohamed dodoma anamsafara kama wa magari 5 na MP wa kutosha,tena barabarani kila kona ya dodoma Millitary police wanafanya kazi za trafiki polisi, nilibaki na duwaa ni kajisemea zama zimebadilika
Kiutaratibu hawaruhusiw kufanya kaz trafk wanatakiwa kuwasiliana trfk na huwa wanasbabisha ajali sometimes wao jukumu lao n kuhakikisha mkuu wao anafika salama. Na ndio maaana hufokea watu kwasababu hakuna mawasiliano katika njia zote kuu
 
Habari wana jamvi,

Kwa wale wakazi wenzangu wa Mbezi Beach, Kunduchi, Goba na watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kwa ujumla
bila shaka Mtakuwa mmekutana na huyu Kamanda wa Jeshi (Chief of Staff) ambaye kuanzia majira ya kila siku Asubuhi 12:30- 1:00 hutugandisha kwenye foleni kwa muda mrefu kila siku akisubiriwa kupita yeye na ma MPs wake wanaoning'inia kwenye milango bila sababu ya Msingi na wakati mwingine waki ning'inia na Bunduki na mavazi kama tuko Afghanistan...wakifokea watu barabarani kukaa pembeni tena wakiwa kwenye wrong Lane!

Binafsi ananikera sana, kama anahitajika kufika ofisini mapema si atoke mapema kama wengine...😡 au ndio Madaraka ya Kulevya?
Kuna siku niliwahi kuongozana na gari ya Waziri wa Ulinzi toka Uwanja wa ndege wa Dsm hadi hadi nilipofika Mwenge nao wakiwa kwenye foleni bila hamaki wala papara.

Hebu mfikishieni salamu huyu Kamanda, awaambie walinzi wake kuwa wastaarabu na kutotukera wananchi.
Kiwango chako Wivu kimeshafika hadi 85% sasa...... Kitaalamu hii ni hatari kwa afya Mkuu.
 
Hii ndio tatizo LA viongozi wengi wa Africa,hao walinzi wake huwa kama majambazi,kufokea watu,kama vile walichokibeba,ni kitu nyeeeti sana,
Mimi huwa najiuliza,kama wao ni wanajeshi waliobobea kwenye medani za kivita,kwanini wanakuwa na papara wanapokuwa wanamsindikiza kiongozi wao?kwanini wasikae kwenye foleni,kimya kimya,bila mbwembwe,wamlinde boss wao vzr,bila papala,maana wanachokifanya,huwa ni "Ku atract attention" kiasi kwamba kama kuna watu wabaya wanaweza kumdhuru boss wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Gusa unase
 
... huyu jamaa sijui ana tatizo gani. Mbona Jenerali Mabeyo tunapishana naye mitaa ya Segerea kila siku kikawaida kabisa bila wananchi kuwekwa pembeni au kugandishwa kwenye foleni. Anasahau kila mtu anawahi kwenye mihangaiko yake na sio yeye tu.

I like him mzee yupo peace saaana unaeza kukutana nae na usimjue
Kwanza anajichanganya na watu
I like him kwakwel


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom