Huyu kanichosha

Huyu kanichosha

blaza, nilipofika kusoma sehemu uloandika kachukua hela kaenda kununua jokofu, roho imeniuma sana. dah, pole blaza.
jitenge na huyo binti atakuingiza kwenye umaskini.
mimi nipo napambana na wangu hapa ananunanuna hovyo habadiliki hata umuelekezeje anajisahau sana.
nashkuru Mungu sijamuoa na dalili za kuoa naona zinaanza kupotea, ni jipu huyu, kisirani mno, sometimes nasema labda kwasababu bado mdogo akikua ataacha ila kuna roho inanambia ntachomwa na jua sana huko mbeleni.

fukuza huyo mwanamke hata akiomba msamaha puuzia usiwe na huruma kama mimi huruma inatukosti sana kaka.
 
Pole sana jamaa kama anazingua usiingie kwenye mkataba

Inaudhi na kusikitisha sana kudhani umepata mke kumbe alificha makucha yake. Hivi Mkuu weye ni KE?

Huwa nawahurumia sana wanaume ninapo sikia mambo ya ovyo kama haya.
 
Duhh.....
Samahani mkuu maana nilikua kanisani, kwani huyo my waifu wako ndio huyo kwenye picha...!!??
 
Shida ni kuoa mwanamke unayempenda sana.
Love is weakness, wachache sana tunaoweza kuweka hisia pembeni na kufanya maamuzi sahihi.
Naitwa Mr. Brian (Sio jina langu halisi). Umri wangu ni miaka 35 kwa sasa. Nilioa miaka mitano iliyopita na mke wangu hivi sasa anayo miaka 28.

Kusema kweli naipenda familia yangu na kama mwanaune najitahidi sana kuihudumia. Nyumbani kwangu tunao mabinti wawili wa kazi. Mmoja kwa ajili ya kusaidia kazi za ndani na mwingine kusaidia kulea watoto wetu mapacha wenye umri wa miaka miwili hivi sasa.

Pamoja na yote nayojitahidi kumtimizia mke wangu, yeye amekuwa mtu ambaye hatimizi majukumu yake kama mke.

Amekuwa na ile aina ya maisha ya mitandaoni, kwanza ni mtu wa kushinda sana Instagram, facebook, Watsapp, Snapchat na Jamii Forums

Katika Page zote za Umbea umbea, page za maeneo ya starehe, hoteli za hadhi hakosekani. Hana muda kabisa wa kunipikia chakula, kunifulia nguo na kazi nyingine zote wanafanya wadada wa kazi.

Nilimtafutia kazi katika kampuni fulani, alifanya kazi miezi miwili tu na kuacha maelezo yake eti mshahara ni mdogo mno ukilinganisha na elimu yake. Kumbe aliniongepea kwani ukweli ni kwamba alifukuzwa kutokana na uzembe kazini.

Sikuona tabu, nikamfungulia duka la bidhaa za nyumbani (mini-shop), lakini biashara hata ikawa haistawi, nilivyofanya uchunguzi nikaja kugundua kuwa sababu ni lugha yake mbovu kwa wateja kiasi ya kwamba ilikuwa haipiti siku bila kugombana na wateja kadhaa jambo lililofanya wateja kukimbia.

Nimechukua maamuzi mara kadhaa ya kumrudisha kwao lakini amekuwa akilia na kudai nimsamehe atajirekebisha lakini wapi, hubadilika muda mfupi na kurudi kwenye ujinga wake.

Jambo kubwa ambalo limefanya mpaka uvumilivu unishinde ni hili; Juzi kati kuna fedha Milioni mbili na nusu niliipata baada ya kuuza mazao yangu, kwa kuwa ile fedha nilipewa cash na ilikuwa siku ya Jumamosi usiku nikaazimia Jumapili baada ya kutoka Kanisani nakaiweke benki kupitia Wakala wa Fahari Huduma.

Kumbe mwenzangu aliziona, akachukua na kwenda kununua furniture, Oven, Friji na vikolombwezo vingine kwa ajili ya kumpa rafiki yake ambaye alikuwa anafanyiwa kitchen party Wiki iliyokua inafuata. Nilipomuuliza akawa akinipa stori za alufu ulela ulela. Hazina miguu wala mikono.

Nafikiri sasa nimechoka rasmi, hapo sijazungumzia masuala ya kunyimwa unyumba. Nafikiria Kutalakiana nae. Maana nahisi muda wowote naweza nikafa kwa pressure nikaacha wanangu bado wadogo.

Je , niko sahihi kwa maamuzi ya kumpa talaka nilee tu watoto mwenyewe maana sioni msaada wowote!View attachment 1094860

Yaani kachukua 2M unachekacheka tu hata kofi hamna,
 
Jamaa ntamnyoosha saivi
Shida ni kuoa mwanamke unayempenda sana.
Love is weakness, wachache sana tunaoweza kuweka hisia pembeni na kufanya maamuzi sahihi.

Yaani kachukua 2M unachekacheka tu hata kofi hamna,
 
Kumbe mwenzangu aliziona, akachukua na kwenda kununua furniture, Oven, Friji na vikolombwezo vingine kwa ajili ya kumpa rafiki yake ambaye alikuwa anafanyiwa kitchen party Wiki iliyokua inafuata.
hii ingekua ticket ya kwenda kwao na asirudi tena, halafu inaonekana mkeo ulimuoa akiwa hajaenjoy ujana vizuri mana ana utoto/ujinga wa kiwango cha lami
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23]
hii ingekua ticket ya kwenda kwao na asirudi tena, halafu inaonekana mkeo ulimuoa akiwa hajaenjoy ujana vizuri mana ana utoto/ujinga wa kiwango cha lami
 
Back
Top Bottom