Finegirlone
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 1,836
- 3,609
Hamna bhana huyu kaka anatuhadithia tu mikasa mbalimbali hana lengo hiloHongera ingawa umezidisha kipimo hapo kwenye hizo M2.5 nadhani umetumia kama mtego/kivutio cha kuwakamata mabinti wa JF
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hamna bhana huyu kaka anatuhadithia tu mikasa mbalimbali hana lengo hiloHongera ingawa umezidisha kipimo hapo kwenye hizo M2.5 nadhani umetumia kama mtego/kivutio cha kuwakamata mabinti wa JF
Naunga mkono hojaOa mmoja wa hao house girls..
Changamoto tuliyonayo vijana ni kuamini tabia tutazirekebisha tukiwa ndani. Lakini tabia ni ngozi itapretend for a while then irudi kwenye uhalisia wakeNaitwa Mr. Brian (Sio jina langu halisi). Umri wangu ni miaka 35 kwa sasa. Nilioa miaka mitano iliyopita na mke wangu hivi sasa anayo miaka 28.
Kusema kweli naipenda familia yangu na kama mwanaune najitahidi sana kuihudumia. Nyumbani kwangu tunao mabinti wawili wa kazi. Mmoja kwa ajili ya kusaidia kazi za ndani na mwingine kusaidia kulea watoto wetu mapacha wenye umri wa miaka miwili hivi sasa.
Pamoja na yote nayojitahidi kumtimizia mke wangu, yeye amekuwa mtu ambaye hatimizi majukumu yake kama mke.
Amekuwa na ile aina ya maisha ya mitandaoni, kwanza ni mtu wa kushinda sana Instagram, facebook, Watsapp, Snapchat na Jamii Forums
Katika Page zote za Umbea umbea, page za maeneo ya starehe, hoteli za hadhi hakosekani. Hana muda kabisa wa kunipikia chakula, kunifulia nguo na kazi nyingine zote wanafanya wadada wa kazi.
Nilimtafutia kazi katika kampuni fulani, alifanya kazi miezi miwili tu na kuacha maelezo yake eti mshahara ni mdogo mno ukilinganisha na elimu yake. Kumbe aliniongepea kwani ukweli ni kwamba alifukuzwa kutokana na uzembe kazini.
Sikuona tabu, nikamfungulia duka la bidhaa za nyumbani (mini-shop), lakini biashara hata ikawa haistawi, nilivyofanya uchunguzi nikaja kugundua kuwa sababu ni lugha yake mbovu kwa wateja kiasi ya kwamba ilikuwa haipiti siku bila kugombana na wateja kadhaa jambo lililofanya wateja kukimbia.
Nimechukua maamuzi mara kadhaa ya kumrudisha kwao lakini amekuwa akilia na kudai nimsamehe atajirekebisha lakini wapi, hubadilika muda mfupi na kurudi kwenye ujinga wake.
Jambo kubwa ambalo limefanya mpaka uvumilivu unishinde ni hili; Juzi kati kuna fedha Milioni mbili na nusu niliipata baada ya kuuza mazao yangu, kwa kuwa ile fedha nilipewa cash na ilikuwa siku ya Jumamosi usiku nikaazimia Jumapili baada ya kutoka Kanisani nakaiweke benki kupitia Wakala wa Fahari Huduma.
Kumbe mwenzangu aliziona, akachukua na kwenda kununua furniture, Oven, Friji na vikolombwezo vingine kwa ajili ya kumpa rafiki yake ambaye alikuwa anafanyiwa kitchen party Wiki iliyokua inafuata. Nilipomuuliza akawa akinipa stori za alufu ulela ulela. Hazina miguu wala mikono.
Nafikiri sasa nimechoka rasmi, hapo sijazungumzia masuala ya kunyimwa unyumba. Nafikiria Kutalakiana nae. Maana nahisi muda wowote naweza nikafa kwa pressure nikaacha wanangu bado wadogo.
Je , niko sahihi kwa maamuzi ya kumpa talaka nilee tu watoto mwenyewe maana sioni msaada wowote!View attachment 1094860
Changamoto tuliyonayo vijana ni kuamini tabia tutazirekebisha tukiwa ndani. Lakini tabia ni ngozi itapretend for a while then irudi kwenye uhalisia wake
My mama once said "beauty with brain is a big deal"
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji12][emoji12]nyie jamaa bhanaNaunga mkono hoja
Ila nashauri awapandishe vyeo wote wawili
Wife awe 3rd officer, uteuzi uanze mara moja
Asante bro kwa ushauri mwema[emoji1317]Ila mkuu si umeamua mwenyewe kumwekea wafanyakazi wawili wa ndani sasa kinachokuliza ni nini ndugu yangu?.
Nikwambie kitu sipendi uweachishe kazi hao mabinti ila kwa masilahi mapana ya ndoa na familia yako embu fanya kuwapa mitaji hao maninti kiroho safi uwaambie samahanini naomba mkataba wetu wa ajira uishie hapa.
Naona watakusikiliza alafu sasa huyo mkeo umuache afanye hayo yote mwenyewe ataacha ujinga wake na uvivu.
Wala usimpe talaka sababu bado utaumia mkuu, huyo bado mdogo sana miaka 28 anaweza mkagawana mali alafu akaenda olewa na kajamaa kaboya boya ukashangaa kabadilika hapo utaanza sema mkeo alikuwa anakucheat na huyo mume wake mpya kumbe walaa ni kwamba kajifunzia nje ya kwako.
Natumai umenielewa Bro!. Pole sana
Tuachie na sie tujaribu kama kweli ni mwema hivyo.Duuh, huyu wangu sitakaa nimuache ng'oooo! Nimegundua wa kwangu ni mke mwema saaaaana,.. Nikisoma maisha ya ndoa ya watu na visanga vyao... Namshukuru Mungu kwa mke alonipa... Hakika nimepata mke haswaaaa... Pole yako.
Kimbiza mapema kabla hujafa kwa pressure.
Kitendo cha kukunyima MJEGEJO ni pigo kwako, sasa mwanamke mwizi unakaa naye wa kazi gani?
Hapo sasa hatujajua kama kuchapiwa umesalimishwa!
Kuna wanawake wanatumiwa na Shetani ipasavyo. Huyo maisha yake ni kutangatanga tu miaka yote. Hawaambiliki wala kusikia ushauri.
Hatma yake ndilo litakuwa juto lake mbeleni
umekosea sana kuweka home maid wawili
Ebu Mrudushe kwako kwa Mara ya Mwisho, Mpeleke were mwenyewe mpaka kwa wazazi wake, waeleze tatizo, ili asikuone unamgeuka alafu aseme yeye mwenyewe lini atakuwa tayari kurudi akiwa na tabia sahihi... Vinginevyo mpeleke sehemu kama unamtoa out Fulani alafu,mchane live ajuekichwani mwako mini kinaendelea... Nafikiri wanaitaji kukumbushwa mara kwa Mara hawa viumbe thaifu wa Mungu...
Si kweli