Huyu kiumbe ananitesa sana usiku

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2021
Posts
4,134
Reaction score
10,644
Yani anakuja anatua karibu na dirishani ninakolala anaanza kulia hovyo.

Hapo ni usiku wa manane, anakuja karibu mara 3 kwa wiki. Cha ajabu majirani zangu hawasikii akilia. Namna gani naweza mdhibiti?

Maana kiasili huyu si kiumbe mwema

 
Chukua torch usiku ukisikia Analia,traatibu nyata!akiwa huko juu ya paa Fanya kama unamlenga na torch ,Kisha washa mara tatu Ile Zima,washa,Zima washa x3 ,atakimbia na hatorudi tena
 
Kama ni muislam piga zile sura 3 usiku kabla ya kulala
(tunaziita Kul 3)
 
Tanya maombi ya Nguvu Mkuu, ukitaka kuthibitisha nguvu ya Maombi, siku akija usiku, amka anza kufanya Maombi, ataondoka na utakuja kutoa ushuhuda hapa!
 
Toa location ili tuhudhurie msiba siku yenyewe ikifika

Au mrudie Mungu wewe na familia yako kwa roho na kweli kama nimauza uza yatakwisha


Tenga usiku mmoja ili umuwinde na kumuua

Mpaka hapo problem solved 100%
 
Ukiwa na mawazo hasi basi hata paka wakimate utasema majini...!pole sana..
 
Tanya maombi ya Nguvu Mkuu, ukitaka kuthibitisha nguvu ya Maombi, siku akija usiku, amka anza kufanya Maombi, ataondoka na utakuja kutoa ushuhuda hapa!
Thank you ubarikiwe sana
 
Mafuta na Maji ya Mwamposa yanamhusu
 
Huyo ndege moja ya sifa yake ni kuweza kunusa mizoga iliyoko mbali.Na huweza hata kunusa kiumbe kinachokaribia kufa(Huwa anauwezo wa kunusa kugundua kiumbe ambacho cell zake za mwili zimekufa nyingi kwamba anae karibia kufa.)

Ndo maana mara nyingi huonekana mahali na baada ya muda kama mgonjwa eneo hilo yupo mtaona siku mbili tatu kafa (japo si mara zote) kwani anauwezo wa kunusa kiwango cha cell zilizikufa hata kwa mtu.


Kwa ushauri wangu Jitahidi chunguza hapo ndani unakitu gani chenye mfumo wa kuumwa sana kama Paka, mbwa au binadam mgonjwa.

Pia kutokana na mazingira yaezekana ame papenda hapo kwako

kama ambavyo ndege wengine hutengeneza Viota vyao kwenye baadhi ya nyumba.


Hivyo ifanye sehemu unayoishu kuwa safi kote ambako kutaondoa mazingira ya yeye kupenda hapo kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…