Mkuu
Slowly nakushukuru sana kwa kutambua mchango wangu kwenu,mbarikiwe nyote mnaoendelea kutambua mchango wangu katika hii platform pendwa ya Jamii Forum!.
Nimepitia comments zote na nimeona upendo wenu kwangu ulivyo mwingi!,nawashukuru sana ndugu zangu!.
Pengine ninachokipaji ambacho bado sijakielewa kuhusu uandishi,mimi naona naandika kawaida kabisa lakini watu wengi wanasema naandika vizuri!,niwapongeze sana kwa kuliona hilo ndugu zangu,mimi muda mwingi nashinda kijiweni hapa bunju na kazi yangu ni muendesha bodaboda tu!.Sina kazi au kibarua kingine tofauti na hiki ninachokifanya kwasasa!.
Mara zote naandika haya masimulizi kwa kutumia simu yangu ya mkononi niliyonayo mpaka sasa ambayo ni Samsung S9.Hii simu ndiyo kila kitu kwangu kwa kuandika,kupiga na kupokea simu!.Huwa nikiwa nimekaa sina abiria najitahidi kuandika chap,na nikipata abiria nasevu nilipoishia na nikirudi naendelea tena!.
Sababu ya mimi kuendesha bodaboda nadhani nitaieleza kwenye Mkasa wangu unaoendelea wa NILIVYONUSURIKA KIFO BAADA YA MZEE KUNITIMUA NYUMBANI.
Hivyo niwatoe shaka tu ndugu zangu ya kwamba sina kibarua kingine tofauti na hiki cha bodaboda.
Nawapenda sana[emoji120]