Huyu Mke sasa ananishinda, nimepoteza hisia kwake kwa kiwango Kikubwa sana

Kuna mmoja niko nae miezi michache, naona ana tabia za namna hiyo.

Vipi familia yake? Maana hizo tabia mara nyingi zipo kwenye familia ambazo hazijiwezi, labda hakupata hivyo vitu kipindi akiwa kwao.

Kiukweli mwanamke alietoka familia masikini na kakulia mjini huwa ni changamoto mno.
 
... sisi Kobazi, mambo ya shopping ni jukumu lako wewe baba mwenye mji!
Fanya manunuzi muhimu yote, ye mpe pocket money yake tu!
... kudokoadokoa ni dalili msosi hautoshi, yaani unataka mpaka kuhesabu vipande vya nyama Mzee!!!?
Ndoa inahitaji usuluhishi hiyo!
 
Mkuu pole sana kwa changamoto hizo. Ni mambo madogo madogo kimuonekano ila ndiyo yanayoharibu ndoa nyingi. Mkeo inaonekana chimbuko lake aidha katoka familia ya baba, mama na mtoto, au familia ya survival of the fittest. Haya mambo ilibidi uyabaini mapema sana kabla hamjaingia kwenye ndia. Aidha ulipuuzia viashiria kadhaa kwa kumezwa na tamaa zako kwake, ukiamini utavumudu hivyo "vitu vidogo", kumbe leo vinakutoa roho.
Huyo ni wako, usimwache. Kadhalika usiweke attention sana kwenye mapungufu yake. Dili na shida zako na utaona matokeo.
 
Ukioa au kuolewa kamwe huwezi kukuta kila kitu kiko sawa lazima kuna mmoja atakuwa na mapungufu.

Na hayo mapungufu ndio NDOA yenyewe.

Huyooo ni chaguo lakoo🎵🎶 Huyooo ni chaguo lakoo🎶🎶
😂😂😂😂😂
 
Ushauri murwa kbsa
 
Na mbaya zaidi anaweza endelea naye ukidhani atabadilika,nikuambie tu tabia ya mtu ni kama ngozi ya mwili kubadilika ni ngumu sana.

Kila moja anatabia za mtu ambazo anaweza kuvumilia,hadi umelalamika maana yake hayo mapungufu kwako yanakuudhi na imekuwa ngumu kukabiliana nayo,option uliyo nayo hapo ni moja tu kuachana nae au kuoa mwanamke mwingine.maisha ni kuchagua.

By the way at the end kila kitu kitapita.
 
Inamaana hukupitia uchumba
Ndo maana watu wanaishi na wanawake miaka kadhaa ndo wanawaoa
 
Hakuna aliyemkamilifu ndugu yangu

Huyo mkeo asikufanye umchoke kwa tabia hizo chache alizoonesha

Ni suala la wewe na yeye kukaa Chini na kuanza kumueleza kuhusu hivyo vitu usivyopenda kutoka kwake

Vile vile mpe nafasi nayeye aseme vitu asivyopenda kutoka kwako(Nina imani atakuwa nayo)

Najua sio rahisi mtu kubadirika kwa siku moja, ila ukimpa muda atabadirika

Kingine jitahidi kuona mema Kwa Kila alifanyalo mkeo

Ukianza kuokoteza mabaya yake, automatic hautaona mazuri yake hata kama yapo anayofanya kukufurahisha

Ukiona mtu na Mume wameishi hadi kuzeeka pamoja, ujue wamevumiliana katika mengi

Jifunze hilo, Kila la heri 🙏🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…