Mpira wa kibongo miyeyusho.
Timu hua hazijifunzi.
Zitapitia shida ile ile kila mwaka ila hamna kujifunza hata punje.
Walianza Yanga. Manji anaihitaji Yanga kuliko Yanga inavyomhitaji Manji.
Yakatokea ya kutokea hadi leo timu inasua sua.
Naon Simba wanajiandaa kufuata mkumbo. Kwamba Mo anaihitaji Simba kuliko Simba inavyomhitaji Mo? Au siyo?
Yaani hapa Bongo Yanga akizingua na kua omba omba msimu huu usishangae misimu miwili mbele Simba ikafuata mkondo huo huo.
Na hawajui kujitegemea na hawajawahi kua na mipango ya kujitegemea
Mkuu ukweli mchungu kuumeza ni kwamba kutokana na upeo mdogo wa vilabu vyetu na mifumo mibovu ya soka basi ni kwelli kwamba SIMBA INAMUHITAJI MO ZAIDI KULIKO MO ANAVYO IHITAJI SIMBA
kama ilivyokua kwa YANGA KUMUHITAJI ZAIDI MANJI KULIKO MANJI KUIHITAJI YANGA
Kinachotoeka hapa ni kama vile unavyoona machimbo yetu ya madini, unaweza kudhani nani anamuhitaji mwenzie zaidi kati ya sisi wenye madini aridhini au wanaokuja kuyachimba?
Kutokana na mifumo mibovu ya soka na vilabu kiujumla simba na yanga zipo miaka yote na zinajinasibu kuwa na thamani kubwa which is true.......lakini sasa wanajua kuigeuza hiyo thamani yao kuwa fedha kuendesha club?
Angalia Yanga wanavyo hangaika sasa lakini Simba Mo anatakiwa kuweka 20b mezani pamoja na ruzuku na usajili anaodai kuufanya na bado club mambo ni mazuri sana sana
Mo ni mfanyabiashara najua hapati hasara kuwa Simba lakini sasa huu ni ubia mkuu Mo ana asilimia 49 na anajua biashara Simba wana asilimia 51 hawajui biashara kabisaaaa
Yaani bodi ikikaa Mo akisema sasa ili twende sawa b20 zipo lakini mazingira ya asset za simba yanaweza kufanya b20 yake ikarudi kwasasa au ndio b20 pekee za Mo itatumika kuzaa na faida.......mahesabu yanagoma
Hii mikataba haipo kirahisi kama tunavyojadili hapa mkuu kuna vipengele vina calculate risk nk lazima vizingatiwe
Nirahisi sana kumshutumu Mo kwakuwa hatujui mikataba inasemaje kuhusu kuanza ku inject hizo b20 baada ya hatua gani
Lakini pia si rahisi sana kuona mafanikio angalau Mo ameyaleta pale Simba toka awe muwekezaji mbia
Lakini chakushangaza zaidi wanaolilia sana kuhusu simba kudhulumiwa na kutapeliwa na Mo asilimia kubwa sio wana Simba
Sasa unajiuli huu uzalendo wa wapinzani wako kutetea maslahi yako wanautoa wapi