Huyu Mo ni tapeli, Magufuli atusaidie kumdhibiti


Mzee mwenzangu leo sijakuelewa kabisaaaaaa sijui umekula maharagwe ya wapi [emoji23]

Kwa mujibu wa taratibu sioni Magufuli anahusikaje na hili

Pili wewe hujui mikataba inasemaje kuhusu hizo b20 kwamba zitatokaje kwa awamu ngapi na baada ya stage ipi ya transformation

Tatu hujui chochote kuhusu ruzuku kama ni sehemu ya mkataba na haihusiani na 20b

Kuhusu matangazo mzee baba ni sehemu ya mkataba Mo kuwa mwekezaji mapesa yote hayo ni matangazo yatakayo mlipa zaidi kuliko gawiwo unalofikiria wewe

So relax mkuu kila kitu kinakwenda accordingly to mkataba
Mo anamkataba na Simba na hakuna mahali umesikia Simba SC imelalamika Mo anaitapeli

Sijui wewe ni shabiki wa timu gani lakini kwanini wasio kuwa wana simba ndio wanajifanya wanauchungu sana na Simba kutapeliwa na Mo?.........najiuliza tu
 
Masikini wana taabu sana, mtaachiwa li timu lenu mrudi kwenye migogoro na hatimaye muwe wabovu kuliko yanga
 
Hao wenye hisa 51 % wametoa kiasi gani Cha kuwa na thamani ya asilimia hizo?
Mkuu hapa utakua unakosea
Simba ni mgodi tayari unathamani Mo ni mchimbaji anatakiwa kutoa gharama za kuwezesha simba kupata hayo madini

Ni sawa na wewe uwe na basi bovu lakini una ruti nzuri ila unapata hasara sababu basi bovu kila siku gereji
Natokea mimi nakwambia hili basi likiwa zima thamni yake ni milioni 100 lakini mimi ntaweka milioni 50 tulikarabati liwe safi lianze safari na mapato tutagawana 50/50

Ndio ilivyo kwa Mo na Simba mkuu
 
Tatizo mtu anapotoa mada hizi watu wanajadili kiushabiki tena wanakushambulia na matusi juu na mo anatumia watu kama hao kama kinga yake.
Nkwabi alipohoji hizo pesa alikuwa anapiga vijembe Twitter na kumgombanisha na wanachama wa simba .
Mo kutoa bilioni 20 si hisani ni wajibu wake na hizo pesa anazotoa ni faida anayopata kwa kuweka fixed account.
Aliwapumbaza simba wasimpe timu mtu mwingine bila yeye kumbuka alivyogombana na uongozi wa simba kuongia mkataba na sportpesa aliona kama simba wakipata udhamini mkubwa yeye asingepata simba kwa bei rahisi.
Alikuwa anataka hati ya jengo ili akakopee benki lakini kina Kilomoni walimshitukia
 
This is too low aisee
 
Teh teh teh Yanga mnaumia sana na Simba ya Mo..

Komaeni na huyo Injinia feki asiye na vyeti Mkimbizi kutoka Habeshi 😂😂😂
 
Mchakato haujakamilika ? Au Hawa taki kuukamilisha!!

Niwaambie tu mnaosema sijui anatoa hisani ya 3bil a year na haingizi chochote ni hvi hakuna CAPITALIST duniani anayefanya biashara ya hasara.
Kwani Simba nayo haiingizi chochote?? Uwekezaji wowote ni win win boss..

Hata Dangote ameinvest apate faida lakini pia wateja wake wanapata cement kwa bei rahisi...

Dhumuni lolote la timu ya mpira kwa mashabiki ni kushinda vikombe na sio kugawana pesa. Hakuna mwaka nimeona Simba ikigawia wanachama au mashabiki wake pesa, kiu ya mashabiki ni kushinda vikombe. Kama Mo anaiwezesha Simba kushinda vikombe na kucheza mpira safi hilo pekee ni furaha kwa mashabiki. Hayo eti sijui anaiba, sijui tapeli hayana msingi wowote wala hayatuumizi mashabiki..

Yanga pambaneni na GSM wasajili wachezaji sio kwenda kuokota wachezaji waliotemwa au wanaokaa benchi kwenye timu zao..
 
Nilitaka kuayasema haya lakini nikahisi wenye akili nyepesi hawata nielewa
 
Unajua yeye anapata kiasi gani kutokana na Simba?

Ndicho alichomaanisha The Boss
Sasa akipata shida iko wapi?? Si anatumia zake au anapata bure tu?? Kama huyo The Boss anayo Billion 25 aende kumpindua Mo na yeye apate..

Shida hapa ni Mo anapata au ni nini?? Kuna ambacho Simba inapoteza? Ni kipi?? Mbona wabongo mna wivu wa kipumbavu hivi??
 
Wewe jamaa nilidhani uko njema up steers kumbe ni uto
 
Nilitaka kuayasema haya lakini nikahisi wenye akili nyepesi hawata nielewa
Mkuu shida ya wabongo wengi ni chuki na wivu.. Na wanaopiga kelele wala sio Simba ni wa upande wa pili
 
Kama ameenda kinyume na mkataba ni tatizo ila kama walikubaliana hivyo sawa tu..........
 
Nimelisemea sana hili jambo, naona watu wamevaa mawani ya mbao.
 
MO alishawahi miliki Singida united, African Lion na zote izo,zilimshinda inamaana Mo anaipenda sana Simba kuliko klabu alizowahi kumiliki yeye binafsi. Ina maana MO hapati chochote Simba ila ameamua kuja kumwaga miela free? Mbumbumbu fc ebu tumieni akili kidogo sio muda wote mnakua na akili za Manara.
 
Alternative ni nini ?

Kama wapo wenye pesa wakutosha basi wote wange-bid kuchukua hio nafasi ya MO ili nao wapate free Promo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…