Huyu mpangaji mwenzangu nashindwa kunielewa

Huyu mpangaji mwenzangu nashindwa kunielewa

Upo vizuri sana lakini lisemwalo lipo kama halipo linajongea
 
Jenga kwako basi ili upunguze maneno ya majirani maana ukiwa kuta njee hawakumizi kama wanakucheka unaishi nao
 
Mkuu, toka kacheze hata draft mtaa mwingine kama umeridhika na kipato. Usishinde ndani iwapo ww ni below 45.

Mfanya biashara gani anayeshinda nyumbani na amepanga nyumba za kushirikiana uwanja?
 
Jenga nyumba Yako utakua huru sana yumba ya kupanga Inamambo mengi huwezi ata kwenda uchi
 
elewa kwamba watu hatufanani aina ya maisha, labda unataka kufahamu nina jishugulisha na biashara gani na nina iendeshaje. kifupi mimi nimesha tega hata nisipo kuwepo ofisini mambo yanaenda. kaziyangu nikwenda kukusanya mzigo ukipungua au baadhi ya mahitaji yakiisha nitaleta utapangwa na nitawapangia bei. na usiku nikwenda kufunga mahesabu nakua nimemaliza

na kuhusu usimamizi nasimamia coz kilasiku lazima nitembelee site na kama kuna mapungufu nitajua tu.

na mambo si haba God is good

na kuhusu maneno ya mimi kulelewa hayo yatabaki kwenye kila mtazamo wakila mtu kutokana na vile atakavyo ona yeye. acha waje kushtuka siku nimehamia kwangu
Anza kupanga nyumba nzima
 
Mtembea bure si sawa na mkaa bure.

Usijiendekeze kukaa sana ndani sio vizuri mkuu.

Idle mind is a workshop of devil.
 
Naona wameamua kukushambulia wewe Tena mkuu🤣😄,futa Uzi wako umsubiri mke wako akutengee maji ya iriki ukaoge zako upumzike walimwengu hawana dogo
 
Wape watu taarifa chache kuhusu wewe. Wasipojua chochote juu yako, watatengeneza za kwao na kimsingi hazitakuwa taarifa nzuri (chanya).
Mfano, waweza kuwabebea bidhaa na kuwaomba wakuungishe kisha ukawaeleza kuwa una maduka yako na umeweka vijana wasimamie nk.
Yote ya Nini hayo kuelezea watu Maisha yako!? Wachaa wao wafikirie wanavyotaka wao,Kama kuna Mtu anataka kweli taarifa zako aje uso kwa uso na siyo kusemea pembeni,na Mtu anaekusemea pembeni huyo ujuwe anakuogopa!!
 
Yote ya Nini hayo kuelezea watu Maisha yako!? Wachaa wao wafikirie wanavyotaka wao,Kama kuna Mtu anataka kweli taarifa zako aje uso kwa uso na siyo kusemea pembeni,na Mtu anaekusemea pembeni huyo ujuwe anakuogopa!!
apo sasa
 
Hii Jf sijui inakwenda wapi yani watu wote wamemgeuka ndugu mtoa uzi mpaka kapewa na jina " mfanyabiashara mvivu"
 
habari za leo I hope nyoote hamjambo.

wakuu kwa wale wenzangu na mimi ambao bado tunajitafuta yaani tunaishi kwenye nyumba za kupanga mnawezaje kuishi na wapangaji wenzenu wanaotaka kujua maisha yako kindaki ndaki?

iko hivi mimi ni kijana na nina miaka 26, na nina mke japo hatujapata mtoto na nimejiajiri na vibiashara vidogodogo ambavyo nimeajiri vijana. mimi nikusimamia na kuhakikisha mambo yanakua kwenye mstari kama kufuata bidhaa ambazo zinakua zimekwisha na kwenda kufunga mahesabu. mara nyingi huwa sipatikani sehem husika mimi niki maliza kama ni asubuhi narudi zangu nyumbani kutulia mimi sio yule mtu wakujichanganya na watu sana. kwasababu situmii kilevi kwamba utanikuta bar nk .

mara moja moja huwa tunatoka wikend na wife, sasa hapa tulipopanga tuko wapangaji wa tatu na wote tuna wake japokua kwenye hawa wapangaji kuna jamaa mmoja na yeye anamke lakini na wao hawa jabahatika kupata mtoto. huyu mwingine ndio ana familia na wote (wanaume) huwa wanaamka nakusepa zao. nyumbani kunabaki wake zao sababu mke wangu na yeye nilimfungulia biashara yake ya duka la nguo, so mara nyingi akisha amka akafanya majukumu yake kama mwanamke nyumbani basi huondoka kwenda kwenye mihangaiko yake ya kila siku na huniacha nyumbani. na huwa nina kawaida natoka satatu natembelea biashara zangu na kuwajulia hali vijana basi kama hakuna tatizo na rudi zangu nyumbani kutulia na maisha yanaendelea.

sasa basi kutokana na maisha nimeyokua ninaishi hata hapa tulipopanga hakuna anaejua mimi na fanya kazi gani. wanaonaga ni salam na vijistory vya hapa na pale kama majirani basi sinaga mazoeya ya hovyo na mtu.

sasa leo wakati nimepita naelekea zangu biasharani kuna mama ni wamakamo kidogo na ni jirani yetu nyumba inayofuata ndio kanisimamisha baada yakumsalimia akawa ananipa story wanazokua wana mzungumzia wife hawa wanawake wa wapangaji wenzangu,

ya kwamba mke wangu ni mjinga haiwezekani mtoto mdogo kama yeye awe ndio anatunza mwanaume (mimi sasa) kwa kila kitu, anamvisha na kumlisha, eti mwanaume wake (mimi) hana kazi yupo yupo kazi ni kulala. hajishugurishi na mambo mengine kibao

nimeishia kucheka na nikamjibu yule mama. nikawaida acha waseme wanavyojua wao kwa sababu hakuna anaejua maisha yetu na tunaishije.

na hivi ndivyo ninavyo penda kuishi sipendi majilani wanijue kiundani zaidi

kama na wewe umeshawahi kukutana na wapangaji wafuatiliaji wa maisha yako kama mimi tena wake za watu weka maoni yako
Dogo Mimi ni mpangaji mwenzio,ni kweli hata Mimi hizo story nimesikia
 
Hii Jf sijui inakwenda wapi yani watu wote wamemgeuka ndugu mtoa uzi mpaka kapewa na jina " mfanyabiashara mvivu"
Mfanyabiashara makini huyu,pesa inamtumikia badala ya yeye kuitumikia pesa kama Wafanyabiashara wengi wao huitumikia pesa hadi hata usingizi hawapati, au hata muda wakua na familia zao hawana kisa wanakimbiza pesa!!
 
Back
Top Bottom