Huyu mtoto niliyemkataa ananikosesha raha

Shooter Again

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
5,603
Reaction score
9,263
Wanajamvi jana nilileta uzi humu kuna mtoto nilimkataa miaka minne iliyopita na wamerudi mtaa niliopo yeye na mama yake, sasa muda huu kaja dukani tena aisee nashangaa anafika anasema baba shikamoo.

Sijaelewa hii situation ni kwamba mama yake kashamwambia Mimi ndio baba yake kama ndio hivyo huyu mwanamke naona kaja kishari kunitafutia matatizo aisee maana nilikuwa najifikiria nifanyaje nashangaa mtoto ananiamkia na sijawahi kumuambia mimi ni baba yake

Sijui ikoje hii kwa akili ya mama yake naogopa anaweza siku akaja kumbwaga kwangu mimi nikiwa sipo na wife akastukia hii ishu aisee.
 
Mchukuwe tu mwanao, mke wako tayari tumesha mwambia,kasema hakuna shida,sema anasubiri kauli yako wwe muhusika mkuu uthibitishe tu kwake!!
 
Unaogopa jukumu la kulea mtoto, unamuogopa mkeo, unamuogopa mzazi mwenzako, unaogopa vyote, au unaogopa nini?

Mwanamme hatakiwi kuogopa ogopa.

Mwambie mkeo una mtoto uwe huru kumlea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…