Huyu mtu alikuwa jini au? Nilisoma na mwanafunzi kipanga ambaye ni mtoro, mtundu, anavuta bangi, kila kesi yumo, n.K

Sio vyema kuja kutangazana humu mkuu, wewe unadhani ningekuwa sijaacha zile tabia za shuleni hapa si ingekuwa kudhalilishana
 
Dah huu uzi umenikosha maana nakumbuka mbali sana ....
 
na hioo shul wanadhani alinunua mtihani.hapa ndipo ulipoharibu stori,yani mtu waliyesoma nae ,maana yake kafanya nao mitiani mingi ya shule na atakua kawaburuza kama alivyokuwa anawaburuza nyinyi,sasa inakuwaje wadhani kaiba mtihani baada ya kupata 1.5
 
Ulitaka kufikisha ujumbe gani kwetu?
Au ulitaka kutusimulia historia yako ya nyuma?? Sijakuelewa mkuu!!
 
Nahisi bangi ina siri kubwa ambayo hatuifahamu. Kuna wengine ina wakubali in a positive way ila wengi ina waharibu.
Inategemea na kichwa cha mtu..
 
Akili kubwa huwaza mambo makubwa! Akili ya wastani hujadiri matukio, akili ndogo hujadiri habari za watu!
 
Mkuu hio 1 ya 5 kwenye shule za kawaida kuipata si shughuli ndogo
 
Wapo wengi tu, kama umewahi soma shule za vipaji unaweza kuwa na mifano mingi...

Mfano mmojawapo ni Wakili msomi wa the Don...kichwa sana yule mwamba na kafanya mambo mengi mengi tu akiwa skonga hahaha
 
alikua ni chalii wa moshi. Akikosa pombe anatetemeka mwili mzima. Malaya wote wa shivaz walikua wanamjua. Akilewa tu kama hamna pindi anaenda kusumbuana nao huko. Ila alikua anajua sana mathematics yule jamaa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]duh!!!
 
Nahisi bangi ina siri kubwa ambayo hatuifahamu. Kuna wengine ina wakubali in a positive way ila wengi ina waharibu.
Inategemea na kichwa cha mtu..
Bangi ina guidance na quality zake
Pia ni usefull sana kwa watu potential wenye motives
Kama Ed ana smoke weed mi nina niikatae
Kwenye bangi hapo kuna siri kubwa.
Bangi inasiri kubwa sana bangi inafikirisha mambo ambayo ukiwa katika akili za kawaida hauwezi yafikiri... Shida kubwa ya bangi ambayo inawakumba wengi tabia ya kusahau vitu vidogo vidogo kwa muda fulani ile hali mara umesahau funguo umeiweka wapi au simu nk
 
Kama ni genius hahitaji muda mrefu wa kukariri, yeye anasoma kama hadithi na anaelewa moja kwa moja alichosoma
 
Hua inatokea kile alichokishika akilini ule mda yuko darasani ndio anakuwa nacho ule mda wa mtihani na kama unavyojua mtihani huwa wanauliza maswali ya mwanzo mwanzo mwanzo hivyo unakuta kile alichoshika ndio kinaulizwa kwenye mtihani.
Sisi elimu ya msingi mwaka 2000 namaliza la 7 kuna demu alikuwa na ugonjwa wa kuanguka na shule alikuwa anakuja anavyotaka wala haulizwi ila la kushangaza mtihani wa kumaliza elimu ya msingi alifaulu tena kwa kupasua vibaya mno na sisi tuliokuwa vinara darasani hakuna hata mmoja alifaulu.huyo demu hakupelekwa shule kuendelea na masomo kwa sababu ya ugonjwa wake ila la kuhuzunisha kipindi kile kile alipigwa mimba fasta na hadi naandika hapa ana watoto 5 na yuko kwa mumewe .
 
Kuna jamaa mmoja advance alikuwa anasoma PCM, ile shule walimu hawafundishi sana, wanatimiza tu wajibu, shule ilikuwa ngumu sana ukijumlisha na ugumu wa masomo watu waligeuza shule kuwa uwanja wa vita,

Yaani ile shule usiposoma unagonga zero, waliokata tamaa hawakuwa wanasoma na walikuwa wanapiga zero pre mock, mock na Necta, watu walikua hawaogi.

Sasa huyo jamaa yeye kazi yake ilikuwa ni kuoga kunga'aa kupiga misele, kwenda Malindi, Sansiro na Mucobs kwa mademu, na alikuwa na wapambe wake machekibob haeasomi wala nini

Cha ajabu pepa la kanda (mock) lilivokuja mwamba akakimbiza lands nzima, wenzake wote wakapiga zero takatifu, necta akatia one kama kawaida, mpaka leo huwa najiuliza yule jamaa alikuwa anatumia mizimu au majini?
Kwa mliosoma physics na Math mtakuwa mnaelewa mziki wa advance ila huyu mwamba hakuwa anasoma kabisa
 
MUNGU SIO MCHOYO

Watu……..endelea sasa kusoma chini

1.Waopata daraja la kwanza kwenye masomo au tunasema distinction ndio wanaokuwa ma-engineer.madaktari na wanasheria

2.Wanaopata daraja la pili kwenye masomo ndio wanaokuwa viongozi wa mashirika mameneja,maofisi waajiri,walimu wakuu,wakuu wa taasisi AJABU SASA WATU WA GROUP HILI ndio wanaowaongoza watu wa daraja la kwanza wanakuwa ni wakuu wao wa kazi au ma manager wao.

3.Wanaopata daraka la tatu kwenye masomo ndio wanaokuwa wanasiasa,wabungu,DED, AJABU SASA WATU WA GROUP HILI ndio wanaongoza magroup yote mawili hapo juu yaani la kwanza na la pili

4.Wanaopata daraja la nne kwenye masomo ndio wanaokuwa wafanya biashara wakubwa matajiri wenye mitaji hasa baada ya kugundua mambo ya darasani hawayawezi sana wanatumia uwezo wao wote mungu aliowajalia bila kuogopa na aibu kufanya biashara hata kama ni biashara uchwara au petty business lakini kiukweli wanafanikiwa na ndio wenye mitaji na hela nyingi.AJABU SASA WATU WA GROUP HILI kutokana na wao kuwa na nguvu ya pesa ndio wanaotawala na kuwaongoza watu wa ma group yote juu yaana la kwanza,la pili na la tatu.

5.Wanaopata daraja la tano kwenye masomo ndio wanaokuwa wanajeshi,polisi AJABU SASA WATU WA GROUP HILI wanapoona watu wa ma group yote juu manne yaani la kwanza,la pili,la tatu na la nne wanapeleka mambo hovyo ya nchi ambayo hayaeleweki wanachukua nchi ili kuyaweka mambo sawa hivyo watu wa magroup yote la kwanza hadi la nne wanafyata mkia wakiamua kuchukua nchi ndio wanaweza kuamua kuwarudishia watu wa ma group ya juu waweke mambo sawa la sivyo watachukua nchi tena na ndio maana watu wa ma group haya wanaogopwa na kuheshimika sana duniani hata raisi anayekuwa madarakani anajua wana uwezo wa kumtoa kwa nguvu.

6.Wanaopata daraja la sifuri au hawakusoma kabisa wanakuwa waganga wa kienyeji.AJABU SASA WATU WA GROUP HILI watu ma magroup yote niliyotaja kuanzia la kwanza hadi la tano wanapoona mambo yao hayawaendei vizuri wakiona ubunge unakaribia kukoma,kwenye ajira cheo hakipandi, biashara zao zinayumba mambo ya mapenzi hayako sawa hii hasa ni kwa wanawake wanakwenda kujisalimisha kwa watu wa group hili kuomba msaada

MUNGU SIO MCHOYO AMEGAWA VIPAJI NA RIZIKI KILA MMOJA AMEMPA STAHIKI YAKE





 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…