Uchaguzi 2020 Huyu mtu anaweza kuchukua hii nchi au anaweza kusababisha mambo yatakayosababisha mageuzi kutokea katika hii nchi

Uchaguzi 2020 Huyu mtu anaweza kuchukua hii nchi au anaweza kusababisha mambo yatakayosababisha mageuzi kutokea katika hii nchi

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Huyu ndugu anaweza kuchukua nchi moja kwa moja kupitia sanduku la kura tukiwa na uchaguzi ulio huru na wa haki, lakini pia anaweza kusababisha mambo yatayosababisha mageuzi yatokee katika nchi yetu.

Wanasiasa wa aina hii husababisha katiba na sheria za nchi katika mataifa mbalimbali duniani kubadilishwa ili kua-accomodate wapinzani ndani ya serikali kutokana na kuwa na uungwaji mokono mkubwa wa wananchi na zaidi kuwa na misimamo isiyoyumba ambayo hulazimisha watawla kufanya nao mazungumzo ili mambo yaende kama ilivyotokea huko Zanzibar kwa Maalim Seif kupewa wadhifa wa kuwa makamu wa kwanza wa Raisi mwaka 2015 kama sikosei.

Baada ya Zanzibar,sasa inaweza kuwa ni zamu ya Bara kufanya mabadiliko ya katiba kuwezesha wapinzani kuwa ni sehemu ya serikali ingawa si jambo rahisi kutokea na hata likitoea, basi huwa na mchakato mrefu lakini mwisho wa siku mambo hutimia ingawa inluence ya taasisi za kimataifa na mataifa makubwa huwa pia ni sehemu ya kufanikisha mambo haya hasa pale upinzani unapokuwa na nguvu na kusimama imara.

Lissu akijiridhisha kupata kura nyingi za kumuwezesha kushinda,basi lolote kati ya hayo linaweza kutokea maana najua hatotaka kurudi nyuma zaidi ya kupigania haki yake na hapo ndio inaweza kuwa mwanzo wa haya niyasemayo kutimia bila kujali itachukua muda gani au kutakuwa na ugumu kiasi gani.

Matamshi yake ya leo kuhusu yeye kupigwa risasi na aliowatuhumu/aliemtuhumu,ni ushahidi wa jinsi gani alivyojasiri wa kusema au kutenda mambo yasiyotegemewa na wengi kwani leo kaenda mbali zaidi katika kutoa tuhuma za waliompiga risasi.

1597954693090.png
 
Lowassa na Mrema ndio walio wahi kuitikisa CCM na haito tokea tena. CCM iko very dynamics inabadilika sana kufuatana na hali halisi na mapenzi ya wananchi kwa wakati huo.

2020 Utaona asilimia 80% ya wabunge CCM ni chini ya miaka orobaini. Upinzani kujivunia vijana haipo tena, wazee ndio wamesheheni upinzani.
 
Lowassa na Mrema ndio walio wahi kuitikisa CCM, na haito tokea tena. CCM iko very dynamics inabadilika sana kufuatana na hali halisi na mapenzi ya wananchi kwa wakati huo.

2020 Utaona asilimia 80% ya wabunge CCM ni chini ya miaka orobaini. Upinzani kujivunia vijana haipo tena, wazee ndio wamesheheni upinzani.
Sijui kama umesoma ukanielewa!!
 
Watumishi wa umma mateso ya miaka 5 ya hakuna increments, kupanda vyeo (walimu),ongezeko la mshahara,kutolipwa malimbikizo yenu n.k iwe ni fundisho na akili zenu kuikataa ccm kwa nguvu zote. Familia zenu ziikatae CCM.

Msiwapigie kura ya urais,wabunge wala madiwani.Ndiyo wadhalilishaji wenu
 
Lowassa na Mrema ndio walio wahi kuitikisa CCM, na haito tokea tena. CCM iko very dynamics inabadilika sana kufuatana na hali halisi na mapenzi ya wananchi kwa wakati huo.

2020 Utaona asilimia 80% ya wabunge CCM ni chini ya miaka orobaini. Upinzani kujivunia vijana haipo tena, wazee ndio wamesheheni upinzani.
Kibao kimegeuka. Subiri utaona. Mpaka sasa hivi kuna majimbo 10 chadema wameshashinda kabla ya uchaguzi
 
Hivi wee jamaa hata una Wazazi kweli? Na kama unao huwa hata una muda wa kuwajulia angalau hali? Slow down man, hii Dunia haijaanza leo, utakuja kuishia kujiua siku moja kama ukiendelea hivyo kuabudu takataka.
 
Kuna kikundi ndani ya CCM ni wanufaika wa unyanyasaji dhidi ya upinzani, wao humchochea mwenyekiti wa CCM kisha kuomba bajeti ya kudhoofisha kuua upinzani Nchini, hawataki umoja wa kitaifa kwani wanakosa pesa nyingi wanazovuna sasa kwa kisingizio cha kurejesha mfumo wa chama kimoja.
 
Subiri kipenga kipulizwe ushindi siku zote ni uwanjani. Hii kaachiwa watu wamshangae ili wakati wa kampeni kusitokee wakutaka kwenda kwa ajili ya kumshangaa. Ndio maana ratiba imepita kwenye ngome zao zaidi.

CCM leo kutangaza majina ya wagombea wao kumeipoteza cdm, je kampeni zitapo anza na tingatinga arudi barabarani?
 
Bila CCM mda huu Tanzania ingekuwa kwenye G5 na kuwa na kura ya veto, Tanzania ni level ya America, German, England, China, Urusi na mataifa mengine tajiri kutokana na Tanzania kumiliki rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani, pesa nyingi inapotelea kwenye kudidimiza demokrasia badala ya maendeleo.
 
Ni kichaa pekee atampa kura mgombea wa CCM 2020
Hata 2015 lowasa alishinda lakini kile kikundi cha uchakachuaji kiliweka Kambi masaki chini ya usimamizi wa January makamba wakashirikiana na Tumeccm vilimpora ushindi Lowasa, uchaguzi huu wa sasa unaangaliwa kwa siri na Duniani nzima endapo Tumeccm watafanya kama walivyofanya mwaka 1995 na mwaka 2016 watambue kuwa uchaguzi utarejeshwa upya
 
Mpenda sifa atoe kitu kimojakimoja Ikulu mapema
 
Lowassa na Mrema ndio walio wahi kuitikisa CCM, na haito tokea tena. CCM iko very dynamics inabadilika sana kufuatana na hali halisi na mapenzi ya wananchi kwa wakati huo.

2020 Utaona asilimia 80% ya wabunge CCM ni chini ya miaka orobaini. Upinzani kujivunia vijana haipo tena, wazee ndio wamesheheni upinzani.
una mawazo yaliyokongoroka sana! una umri gani mkuu? Lissu hafanani kabisa na hao uliowataja
 
Hata 2015 lowasa alishinda lakini kile kikundi cha uchakachuaji kiliweka Kambi masaki chini ya usimamizi wa January makamba wakashirikiana na Tumeccm vilimpora ushindi Lowasa, uchaguzi huu wa sasa unaangaliwa kwa siri na Duniani nzima endapo Tumeccm watafanya kama walivyofanya mwaka 1995 na mwaka 2016 watambue kuwa uchaguzi utarejeshwa upya
Safar hii wameamua kuweka wazi kituo chao pale dodoma
 
Lowassa na Mrema ndio walio wahi kuitikisa CCM, na haito tokea tena. CCM iko very dynamics inabadilika sana kufuatana na hali halisi na mapenzi ya wananchi kwa wakati huo.

2020 Utaona asilimia 80% ya wabunge CCM ni chini ya miaka orobaini. Upinzani kujivunia vijana haipo tena, wazee ndio wamesheheni upinzani.

Maybe ni mgeni kwenye siasa
Mrema alikuwa amepandikizwa tu so ccm walikuwa wanajua nn kinafanyika

Lowassa still alikuwa ni Mwanaccm Tena ambae 80% ya maisha yake katumikia Chama

Lisu hajawahi kabisa kuwa ccm
 
Back
Top Bottom