Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Huyu ndugu anaweza kuchukua nchi moja kwa moja kupitia sanduku la kura tukiwa na uchaguzi ulio huru na wa haki, lakini pia anaweza kusababisha mambo yatayosababisha mageuzi yatokee katika nchi yetu.
Wanasiasa wa aina hii husababisha katiba na sheria za nchi katika mataifa mbalimbali duniani kubadilishwa ili kua-accomodate wapinzani ndani ya serikali kutokana na kuwa na uungwaji mokono mkubwa wa wananchi na zaidi kuwa na misimamo isiyoyumba ambayo hulazimisha watawla kufanya nao mazungumzo ili mambo yaende kama ilivyotokea huko Zanzibar kwa Maalim Seif kupewa wadhifa wa kuwa makamu wa kwanza wa Raisi mwaka 2015 kama sikosei.
Baada ya Zanzibar,sasa inaweza kuwa ni zamu ya Bara kufanya mabadiliko ya katiba kuwezesha wapinzani kuwa ni sehemu ya serikali ingawa si jambo rahisi kutokea na hata likitoea, basi huwa na mchakato mrefu lakini mwisho wa siku mambo hutimia ingawa inluence ya taasisi za kimataifa na mataifa makubwa huwa pia ni sehemu ya kufanikisha mambo haya hasa pale upinzani unapokuwa na nguvu na kusimama imara.
Lissu akijiridhisha kupata kura nyingi za kumuwezesha kushinda,basi lolote kati ya hayo linaweza kutokea maana najua hatotaka kurudi nyuma zaidi ya kupigania haki yake na hapo ndio inaweza kuwa mwanzo wa haya niyasemayo kutimia bila kujali itachukua muda gani au kutakuwa na ugumu kiasi gani.
Matamshi yake ya leo kuhusu yeye kupigwa risasi na aliowatuhumu/aliemtuhumu,ni ushahidi wa jinsi gani alivyojasiri wa kusema au kutenda mambo yasiyotegemewa na wengi kwani leo kaenda mbali zaidi katika kutoa tuhuma za waliompiga risasi.