Huyu Mwafrika mwenzetu "anatisha", anaongea maneno mazito sana kuhusu ujinga wa Waafrika

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Kama kichwa cha habari kinavyosema, katika pita pita yangu mtandaoni nimekumbana na hii video. Kwa mtazano wangu, huyu jamaa ana upeo, muono na mawazo mapana sana na ana kipaji cha kuzifikisha fikra zake kwa ufasaha na utulivu wa viwango vya juu kabisa. Ana uchungu na ujinga wetu Waafrika na anaufafanuwa vizuri sana. tafadhali msikilize mwenyewe upanuwe mawazo. Hili ni zaidi ya somo. πŸ‘‡πŸΎ


Tafsiri ya Kiswahili kwa msaada wa google ya anachokisemaπŸ‘‡πŸΎ

(what's up family this is your man not your boy gold black to AfricaI did a video that did not actually go through
being that uh the reception is off but I'm back and I would like to really share with)


Nini habari familia, ni mtu wako si kijana wako, salaam kutoka kwa Dhahabu Nyeusi kwa Afrika.

Nilifanya video ambayo kwa kweli haikupanda kwenye mtandao, mtandao haukuwa vizuri ukazimwa lakini nimerudi tena na ningependa kushiriki na Ninyi nyote, mnisamehe, nafahammu wengi wenu huenda msipende jina la ujumbe wangu "Nakabiliana na Ujinga uliojazwa na ukoloni kwenye akili za (ki) Afrika". tunaposikia maneno kama" ujinga" tuelewe kuwa neno ujina siyo tusi bali ni neno ambalo watu wengi linaweza kuwatatiza na kuwashughulisha lakini tuchukulie kuwa ujinga sio kosa, ni sifa kwa sababu tunajuwa kuwa ujinga unamaanisha mtu ambaye hana ujuzi au ni mtu ambae hana ufahamu wa kitu fulani, na na pia ni kile kilicho juu ya uwezo wa mtu.

Wengi wa ndugu zangu wa Afrika hatuelewi kuwa ni ujinga kujifanya tunajuwa namna ya wenzetu wa kutoka nje na wageni wetu kutoka nje kuwa wanawaza na kufikiri kama sisi.

Kina kaka na akina dada ninaowaona hapa Afrika wana shida sana linapokuja suala la kukabiliana kibiashara na watu wa nje. Kutokuelewa mawazo ya kigeni ndio utaona Mwafrika anateseka anapokaa mezani na wale ambao anafanya nao biashana, hata haelewi mawazo ya biashara za kibepari na njia za kufanya nao biashara. jambo ambalo hupelekea kupoteza faida, kimsingi biashara ni faida.

Lakini hiyo sio haswa kile ninachozungumzia linapokuja suala la ujinga wa Afrika. Najuwa wewe unaona nalisema hili kiwepesi sana. Siyasemi haya kwa nia ya kumkosea mtu yeyote. Ni wazi, wakati mimi naanza kuangalia mienendo ya hapa hivi karibuni nikaona muono wa kikoloni.

Inaendelea post # 53
 
DP oyeeeeeee
 
Sa100 kaiuza nchi ya Tanganyika kwa wajomba zake Oman
Endelea kubaki na ujinga wako, kama Dhahabu Nyeusi anavyosema hapo juu, siyo maneno yangu hayo. Usinizozomokee. Wewe basi hata tofauti ya Oman na Dubai huielewi jalafu unajifanya unajuwa, ndiyo ujinga wa Mwafrika anaousema Dhahabu Nyeusi huo. Tumia muda wako kufanya japo kijitafii kidogo ili uelewe tofauti ya Oman na Dubai wanapotokea DP World.

Nafaham, hukumuelewa Dhahabu Nyeusi kwa kumsikikiza, lakini farijika kidogo, nimeshaweka tafsiri ya Kiswahili kwa msaada wa google, rudi juu ukamsome.

Swali kwako: Hivi Tanzania hii Akasankara hauna hata shemeji wa kusingiziwa wa Kiarabu?
 
Endelea kubaki na ujinga wako, kama dhahabu nyeusi anavyosema hapo juu, siyo naneno yangu. Usinizozomokee.

Nafajamu, hukumuelewa kwa kumsikikiza, lakini farijika kidogo, nimeshaweka tafsiri ya Kisqahili kwa msaada wa google, rudi juu ukamsome.
Hivi kwanini sa100 anauza nchi na kukutumia wewe kupiga promo?
 
Huo ujinga unaozungumziwa hapo unaanzia kwa viongozi tulionao, kuna viongozi wajinga wasiotaka kuhangaisha akili zao kwa lolote, ni wavivu, mpaka kwenye mambo nyeti kama mikataba muhimu inayohusu hatma ya mataifa yao hawana muda wa kuipitia, wao ni kuwaachia wasaidizi tu.

Matokeo yake wnajikuta kwa ujinga wao wameshajitumbukiza wao binafsi na mataifa yao shimoni, kinachofuatia baada ya hapo ni kujificha kwa aibu, huu ujinga wa kuwaona wawekezaji ndio solution ya kila changamoto inayozikabili serikali za kiafrika, kwangu ndio ujinga mkubwa zaidi ya mwingine wote.
 



Umekuwa mtu mjinga sana, and thw only justification ili nikuelewe ni kwamba umepata financial gain.
 
Ujinga na unafki ni sehemu ya utamaduni wa mtu mweusi, haijalishi yuko wapi.
 
Umekuwa mtu mjinga sana, and thw only justification ili nikuelewe ni kwamba umepata financial gain.
Tatizo kubwa sana ninalolishuhudia kwa Watanzania wengi ni ujinga mbaya, tuelewane kuwa ujinga siyo tusi, ujinga ni sifa ya kutokuelewa. Sifa inaweza kuwa nzuri au mbaya, sifa ya ujinga mbaya ni ile ya kutokuelewa kuwa huelewi, sifa nzuri ya ujinga ni ile ya kutokuelewa lakini unafahamu kuwa huelewi.

Ukishaelewa kuutofautisha ujinga katika sifa nzuri na mbaya basi itakuwa wepesi sana kutokana na ujinga mbaya mwingi na kubaki na ujinga mzuri mchache wa yale mapya usiyoelewa. Na namna ya kuufuta ujinga mbaya ni kujifunza kile usichokielewa, ukishakielewa ina maan hu mjinga tena kwenye hicho unabaki kuwa mjinga katika kile tu ambacho hujajifunza.

Mfano mzuri tena ni mfano hai, ni huu wa sakata la bandari. Wengi tunajifanya tunaelewa kumbe hatuelewi chochpote, tunakuwa washitaki sisi, watowa hukumu sisi, waadhibuji sisi, wachimba makaburi sisi ya tuliowahukumu sisi. Siyo vibaya yote hayo, si ndiyo tunafanya kazi zote hizo kwa bidii, hatungoji kufanyiwa, au sivyo? Ni sifa kubwa hiyo.

Lakini ni sifa ya ujinga mbaya, sana tena sana. Kwa sababu huyo tunaemhukumu hatumjuwi. Tunamhukumu bila hata ya kumuona. Ujinga mbaya unazidi pale aliyekwenda kumuona, akmjuwa huyu ni nani, anafanya nini, tunamuona yeye ni mjinga. Nadiriki kusema tulionao ni zaidi ya ujinga mbaya, ni uhayawani kabisa.

Anaebisha atwambie, yeye kishafanya biashara ipi inayohusu bandari? Na kishafanya na nani? na kaifanya wapi?

Kama hana qualification hata kidogo za kuyajuwa hayo, na haujafanya hata utafiti japo kidogo wa kupata uelewa wa hayo, basi huna haki ya kunyanyua mdomo. Mao Tse Tung alisema "haujanya tafiti hauna haki ya kuongea". Nyerere alisema mmoja katika maadui zetu ni ujinga. Na mimi nakubaliana nae kwenye hilo 100%, nisichokubaliana nae ni zile sifa nyingine za maadui zetu. Nna sababu yangu moja tu ya kuzikataa hizo. Nayo ni kuuta ujinga, naamini tukifuta ujinga zile sababu zake mbili zingine hazitakuwepo tena.

Ambae hajafanya biashara za kimataifa au hata za kitaifa zinazohusiana bandari na ambae hajafanya japo utafiti wa anachokipinga katika sakata la bandari, hana haki ya kupinga na hana haki hata ya kufunguwa mdomo wake, yeye akubali tu, awawachie waliokwishafanya biashara hizo na au waliokwishafanta tafiti kwenye hilo.


Mimi napinga wajinga wote wanaopinga kijinga kwenye sakata hili. Haya, leta ujinga wako tuupime hapa ni ujinga mzuri au ujinga mbaya.
 
Wewe unapinga kimhemko tu,

Kwanini unahisi waliotofauti nawe kimtizamo ndo wako kwenye upande wa ujinga, hujawaza kuwa wewe ndiyo unaweza kuwa mjinga hufikirii athari zinazoweza jitokeza hapo baadae kulingana na huo mkataba ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…