Huyu mwanadada member wa JF napenda sana tabia yake

Huyu mwanadada member wa JF napenda sana tabia yake

Mie sijambo kama nyie.

Nasema kutoka moyoni tena bila kushuritishwa na mtu, napenda sana tabia ya huyu dada member mwenzetu hapa JF. Huyu dada hana maringo, hana hasira hata mtu akimjibu utumbo. Hivi kwa nini na mie sina tabia njema kama za huyu dada (nina hasira sana). Mie mtu akinitibua ni jino kwa jino, jicho kwa jicho, mguu kwa mguu, mkono kwa mkono kinachofuatia ni nasomeka BANNED.

Wewe dada una busara sana. Mimi kama mwanamke mwenzio nasema hivi una tabia njema. Na kama una familia basi familia yako utakuwa unawalea katika maadili mazuri.

Huwa nikiona mtu "anamchokoza" huyu dada niko tayari kuingilia huo ugomvi (nina element za ugomvi sipendagi ujinga mimi).

Barikiwa sana Dada Sky Eclat pia nakutakia maandalizi mema ya mfungo (Kwaresma).
Kwa hio avatar.....lazima uwe dizaini hio!
 
Sky yupo vizuri.. sio character tu ni smart pia .. i love nd adore this woman ila ndo hivyo sikuzaliwa mapema

Kuna mtu anaitwa heaven sent ..ingawa hayupo active lakini ni mtu naemkubali pia

Lakini pia kuna watu wengi sana nnaowakubali yaani mtu ukikuta amekupa like yake ni sherehe.. sky, Fisadikuu ,The boss ,Kiranga sijui ndo alwatan maana wanafanana kila kitu kasoro majina.. emmymata ,Daby (Mu boy mwenzangu) etc maana wapo wengi
Weka na Dina hapo
 
Uyo mdada ni mtu wa watu ndyo maana hutokuta anatukanwa hata na kale ka mange kimambi ka umu kanakoitwa the list
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Amiin dada. Yaani niseme ukweli leo nikiona id yako ilivyo ya muda mrefu huwa natamani na mie yangu ije kuzeeka hivyo hivyo.

Wewe ni mmoja wanaonifanya niitunze id yangu aisee. Yaani sitaki itokee siku niikimbie.
Mie nimeingia enzi ikiwa Jamboforums. aliyenishawishi kuingia ni bwana mmoja alikuwa mtangazaji wa ITV, akaja akawa DC na siku hizi yuko Star TV anaitwa Novatus Makunga
 
Back
Top Bottom