Huyu mwanamke anafaa kuwa mke kweli?

Huyu mwanamke anafaa kuwa mke kweli?

Fimbo ya mbali haiui nyoka...mimi kuna long distance dem tulikuwa tunadate alipotea wikiend nzima...cm hapokei...mesej hajibu...nikajua tyar mwenzangu anajipakulia...na kwakuwa nlshajiandaa hilo nkapotezea...sijibu meseji na sim zake mpk leo
 
Mbaya zaidi huyu getu me pia namtafuna Sanaa..kwanza ni loose ball hiyo...pole mkuu
 
Habari Wakuu,

Bila kupoteza mda niende Moja kwa Moja kwenye mada.

Nilikuwa na mpenzi ambaye ndiyo nilikuwa nategemea kumuoa, kilichofanya nije niulize hapa ni hili tukio. Mimi Niko mkoa mwingine na mpenzi wangu alikuwa anafanya kazi mkoa mwingine.

Siku moja nikawa nimeenda kumsalimia na nikaa naye kama siku tatu hivi ,baada ya hapo nikarudi mkoa ninaoishi kwa ajili ya kazi, basi ijumaa ya wiki hiyo niliyorudi akaniambia kutakuwa na ugeni ofisin kwao hivyo atakuwa busy maan yeye anafanya kazi hotel.

Basi kuanzia siku ya jumatatu hakuwahi pokea simu yangu wala kujibu text zangu Wala kanipigia yani nikawa nampigia simu inaita weee bila kupokeleea na namtumia text hajibu mpaka wiki ikaja kuisha siku ya jumapili ndiyo akaja pokea simu baada ya kumuuliza kwann hupokei simu wiki nzima na hata text hujibu, akanijibu vimajibu vya kitoto sana basi nikakaa kimya.

Siku hiyo hiyo baada kama ya lisaa limoja hivi nikapokea text kutoka number mpya ikiwa inanitaka nitoe ushirikiano wa kuwa huyu GETU unamfahamu? Na nina yako, maana Mimi nilikuwa naye wiki nzima na simu nilikuwa nazo Mimi.

Basi nikamuelekeza jamaa naye akamaindi sana, kumbe jamaa naye alikuwa katoka zenzibar kamfata Getu, basi kama wanaume tukaongea pale yakaisha ikaonekana demu anatuchanganya wote, basi mie nikaona hapa hamna mwanamke

Baada ya tukio hilo baada ya mwezi mmoja akaanza kunitafuta na kuniomba msamaha Sana na alinifata hadi ninakoishi mkoa mwingine lakini nilimfukuza alilia Sana ila nilikaza na baadaye akasema Akili mbili Nina Mimba na hii Mimba ni yako.

Ishu kubwa inayonitesa je hii Mimba inaweza kuwa yangu kweli au nimpotezee tu nisubiri akija jifunguwa ndiyo nione mtoto Kama anafanana na Mimi au laa?

Maana Toka tukio Lile sinaga hisia naye kabisa na namchukia sana.
Nilimpata mtu humu tukaanza mahusiano fresh tu lakini ni ya kwa simu basi yalikuwa mazuri tu tena sana .
Kidogo akasema nakuja huko Arusha mie kuja kukuona weweee siukimpigia anakuwa anafoka sasa hakujua anaongea na mtu gani basi nikawapa machalii kazi wakaenda kumsaka aliposema yupo na sehemubza starehe za watu waserikali akadakwa yupo najimama ndio amekuja kumsabahi huku Arusha , weeee nikamvumilia nikaona isiwe ishu nikamuacha .
Basi nikaja jua kuwa huku jf wengi hamjielewi wanaume mpo tu .
Unalala na limama lenye watoto watatu kila mtoto ana baba ake.
Mnawaacha wasichana tifu tifu huko mlipo au huku mnapokwenda aisee mnamoyo .

Mwingine naye unaanza mahusiano naye halafu hata wiki haiishi demu anapokea simu .
Hello hii simu ni ya bwana angu dah bwana yupi huyoo.
Akamtaja siunachoka sasa ...
Dawa ya wanaume weusi ni moja tu.
Wanawake wote wakaolewe na wazungu period....
Mie natafuta mzungu ndio wanaoendaga wanawake wazuri, wabaya wao wanataka tu mapenzii.
Basii.
 
Fimbo ya mbali haiui nyoka...mimi kuna long distance dem tulikuwa tunadate alipotea wikiend nzima...cm hapokei...mesej hajibu...nikajua tyar mwenzangu anajipakulia...na kwakuwa nlshajiandaa hilo nkapotezea...sijibu meseji na sim zake mpk leo
Long distance relationships iwe ni kwa muda mfupi usiozidi mwezi. Zaidi ya hapo utachapiwa tu hata ufanyeje...
 
Kilichonipata Mimi kitakupata naww, Cha msingi subir mtoto umuone Kwanza utauziwa mbuzi kwenye gunia..oohhhoooo
Mkuu kilikupata nini???..nipe experience maana nami kuna janga lmetokea...na ametoka copy ya mama yake...hakuna ht kucha
 
Back
Top Bottom