Huyu mwanamke ni sahihi kuniambia maneno haya?

Kipo mkuu, na kama umesoma vizuri, jamaa aliacha kanunua ngano, hiyo inafaa kuandaa vitafunwa hata vya wiki nzima
Yah...lakini kwa mtu mwenye mtoto mchanga kama shemeji yetu,kupika vitafunwa kila siku inachosha mkuu. Pia huo upishi unaambatana na matumizi ya sukari ,mafuta na nishati kwa kiasi fulani ambapo kama ukinunua utasevu hivyo vitu.

Nikiwa fair kabisa kwa shemeji yetu niseme amejitahidi sana hizo siku 5 kutumia balance ya 30k.Lakini kauli zake kwa ndugu yetu hazikuwa kauli za mke kwa mume wake.Ingawa ndugu yetu pia hajatuambia dialogue ilivyokuwa hadi wakafikia huko....
 
30k kwa wiki mzee baba?🤔
Ndiyo uwezo wake,maisha ni kama vidole kuna vifupi kuna virefu yeye kaacha 30K kuna mwengine anaacha 20K na life linasonga,ukiwa hujui maisha utaona kitu cha ajabu.

Shida mwanamke akiwa na tamaa na kupenda kuishi kuiga marafiki ndo tabu zinapoanzia,mwanamke anatakiwa kuwa faraja kwa mume maisha hayaji tu from no where mimi early 2016 niliacha kazi kwa mtu binafsi nikiwa nyumba ya kupanga nikaanza biashara home natoka naacha chini ya 5K tupo watatu mimi yeye na mtoto wife anavumilia ananitia moyo leo anaishi nyumba yake kubwa anachokitaka anakipata tena on time.

Maisha lazima yawe na kiasi mimi huyo aliyemuombea mumewe afe kwa sababu kaacha 30,000/= ingekuwa amri yangu ni aachwe mara moja hafai kufanya maisha na mtu aliye serious.na utakuta huyo anayemuombea kifo mtoto wa mtu yeye alikulia maisha mabovu kula ugali kwa limao leo anataka alishwe vizuri huku akiwa ni kisirani kwa mumewe.
 
Aisee kuwa tegemezi tabu sana. Nikajua laki 3 kumbe elfu 30 yaani elfu 10 ziwe tatu. Pole yake huyo mkeo
Nani asiyewajua nyie???

Hata kama ungekuwa na zako still ungempigia simu kumpa hizi shit huku ukimjaza pressure na bill kwamba nimenunua hiki nimenunua kile,hela ya mwanamke itumike mwanaume asiilipe wewe ulisikia wapi?
 
Nina imani hata ungempatia laki mbili kwa huo muda uliokaa safarini angetafuta janga lingine ilimradi tu mfarakane. Huyu hana sifa ya kuwa mwanamke mkuu kama yupo tayari ufariki kwa ajari kisa umemuahia 30k!! Na je ukifa atapata wapi hizo pesa anazodhani alistahili kuachiwa,? WASHA TAA YA TAHADHARI chief.
 
📌🔨
 
Kwanza mmefikaje fikaje hapo... sababu siamini kama ni ishu imeibuka siku moja tu, lazima kulikua na vimaneno maneno na mienendo flan hv mpaka mke kutoa kauli hiyo. Hebu dadavua kidogo..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…