Huyu mwanamke ni sahihi kuniambia maneno haya?

Huyu mwanamke ni sahihi kuniambia maneno haya?

Aisee aisee nimeandika nikafuta, nikaandika nikafuta tena...

Ni kawaida yao wanawake kuwa na Shit Tests

Kuwa makini na huyo mwanamke
 
Haya tuwe serious Kwa siku wakibhana .
Viungo meaning nyanya , hoho na hayo mazaga ni elfu Tano Kwa siku Moja .
Nyama kg 1 nanusu 15,000tsh
Nauli 3,000tsh
MATUNDA
Elfu Tano
Jumla sh. 30,000tsh Kwa siku
Nyama kilo moja na nusu kwa watu wawili wamalize siku moja jamani?? Hoho, karoti na nyanya vya 1000 vinatosha kabisa kwa siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za harakati za maisha wananzengo,

Niiende kwa hoja moja kwa moja. Nina mke wangu ambae leo tunamiaka mitatu kasoro. Tumekuwa tukiishi vzr tu bila ugomvi na kama upo ile kupishana tu kauli.

Sasa kabla ya chirismas nilipanga safari ya kwenda mkoani Kagera, nikanunua mahitaji yote mf mchele, unga, mafuta, sabuni, ngano, maharage na vitu vingne ambavyo ni mahitaji.

Safari yangu ilikuwa ni ya week moja ambapo niliondoka j'2 na kurudi J'3 ya week iliyofuata. Sasa pesa za matumizi ya mboga ,labda mshumaa In case umeme umekata nilimpa shilingi 30,000.

Ndani wapo watu watatu mke wangu, mjomba wangu yaani mtoto wa dadaangu yupo form one na mwanangu mdogo ana mwaka mmoja na nusu.

Kabla ya siku mbili kuanza safari ya kurudi alinipigia simu anasema pesa imeisha ya matumizi, mwanamme mzima naiachia familia nzima elf 30000 kwa muda wa wiki nzima ,kwakweli nikaumia sana kwa maneno yale. Lakini kubwa zaidi nilivyomuambia kuwa anivumilie kwesho kutwa nakuja akasema bora hata upate ajali ufie huko usirudi kabisaa make mme gani huwezi kulea familia.

Mm kipato changu ni shiling laki tano kwa mwezi ila ninavyoona mke wangu anahitaji maisha ya kupato cha milioni. Maneno anayoniambia kama huwezi kulea familia subiri uje usaidiwe yamenikasirisha sana wakati mm ninatoa kile nilicho nacho.

Sasa ndugu zangu mwanamke kama huyo utamfanyaje?
Katika hiyo 30,000/- ulipigaje hesabu? Kwamba kila siku, watu watatu watumie 4,285/- kila siku? Kwamba mboga itoke hapo, unga au mchele utoke hapo, mkaa utoke hapo, viungo vitoke hapo etc..!?? Wa kupimwa wewe
 
Tatizo lako/lenu mnaochangia kwenye huu Uzi, mnapanga bajet kwa kuangalia matumizi yenu, na sio ya mleta mada. Sasa umeme 50k kwa mwezi, kwani amepanga nyumba nzima? Na hata kama amepanga nyumba nzima, unajua ni vifaa gani alivyo navyo hapo kwake vyenye kutumia huo umeme per month?

Maji 25k per month, unajuaje labda maji wanalipia kwa ndoo na sio kwa bill?

Me nadhani mngesoma tena original post,ili mpate basics ya topic yetu. Msitolee mifano ya mahitaji yenu

Nimeshangaa sana, achana na huo umeme wa 50,000 , angalia maji ya 25,000 kwa familia ya watu wanne, hii familia sio ya hali ya kawaida kama maelezo ya mleta mada….
Umeme 10% maji 5% ya kipato
 
Pole sana mkuu,,huyo mkeo inaonekana amechoka maisha na wewe kwa maana mwanamke Huwa anamheshimu sana mume wake ila tu endapo kama anampenda.

Hakuna mwanamke anamheshimu mwanaume asompenda na hasa asipokua na Hela. Hata kama hiyo budget ni ndogo mkeo alitakiwa akubaliane na maisha kwamba ndio kipato cha mumewe na hata kama ilipaswa kukwambia bas angetumia lugha nzuri sio huo ushubwada alooongea.

Ndo umeshamuoa mkuu so hapa pambana na huba lako
 
Nadhani kama vitu basic vipo ndani namaanisha kwa mlo wa asubuhi mpaka jioni
1.Majani ya chai
2.Sukari
3.Ngano na other ingredients
4.Spaghetti
5. Other stuffs kama viazi au ndizi

6.Maharage
7.Dagaa
8.Kunde
9.Unga
10.Mchele
11.Mafuta
12.Gas/Mkaa
13.Chumvi

Hiyo hela kwa wiki angeishi kwa mpito kwa kuwa haupo, ila hizo kauli alizozitoa si za kiungwana maana hata kwenye ku manage matumiz angeweza for a week tuu.
 
[emoji23] nashangaa kama kweli ana familia huyu mchangiaji!!
Yaani nashangaa mpaka basi maelezo yake. Mimi tunaishi wawili uongo mbaya nyama nusu inatutosha kabisa mchana na jioni. Hoho na karoti za 500, nyanya 500 unaunga mboga mchana hadi jioni inatosha.

Kiukweli mimi 5000 kwa siku inatosha kama nina gesi, mafuta mchele, sukari na unga ndani.
Siku nikiamua kujilipua kweli naweza kutumia hata 50000 au 60000 lakini sio kwa chakula cha kupika nyumbani ni kula nje tena hotelini.
Sababu hata useme utapika pilau la kuku wa kienyeji bado haifiki 50000. Kuku ni 20000 viungo vyooote vinagota 10000 hapo mpaka nyanya za kachumbari. Watu wanaishi maisha ya kuwaza tuu sio halisia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nimetoka familia ya kawaida ,siyo ya kula maharage kila siku ila sometimes tunaweza kukosa tukapiga chai na mkate au asubuhi uji.

Nimesoma boarding ya kula marage kila siku na makande daily(No option ila kuna wanafunzi wengine walikuwa wanakula canteen kwa fedha za baba zao) ,tambua hapo ni shule kwahiyo inabidi twende hivyo hivyo ila sio kwa nyumbani.
Kipato hakitoshi, vya ziada vitatotoka wapi?
 
Nimeshangaa sana, achana na huo umeme wa 50,000 , angalia maji ya 25,000 kwa familia ya watu wanne, hii familia sio ya hali ya kawaida kama maelezo ya mleta mada….
Umeme 10% maji 5% ya kipato
Watu wanaandika tu kile wanachoona kinafaa, ila hawapo realistic
 
Nyama kilo moja na nusu kwa watu wawili wamalize siku moja jamani?? Hoho, karoti na nyanya vya 1000 vinatosha kabisa kwa siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ongea wewe mwanamke mwenzake, anaweza akaelewa. Maana uhalisia wa kula kilo moja na nusu kwa siku, tena watu wawili (maana mtoto wa mwaka mmoja na nusu, hata vipande vinne hamalizi.)
 
Katika hiyo 30,000/- ulipigaje hesabu? Kwamba kila siku, watu watatu watumie 4,285/- kila siku? Kwamba mboga itoke hapo, unga au mchele utoke hapo, mkaa utoke hapo, viungo vitoke hapo etc..!?? Wa kupimwa wewe
Nadhani wewe ndio wa kupimwa. Umesoma post nzima na kuielewa?
Kuna watu mna vichwa vibovu.
 
Umaskini nauchukia sana,
Vitu vinavuohusu pesa kwa nini ugombane na mwenzio?
Mpe hela hutosikia anaongea,
Unamwachaje mkeo 30,000 kwa siku 7 kweli😢 TOA SUALA LA KULA KUNA EMERGENCY
Ametumia lugha Kali ila ana hoja
 
Kwani so kila kitu kipo ndani
Kuna unga, mchele, maharage, ngano na mafuta wanavipikaje hivyo vitu ili wale? Je, kila siku mboga itakuwa ni maharage? Vipi kuhusu chakula cha asubuhi? Matunda na mboga za majani hawali? Viungo vya upishi?
 
Habari za harakati za maisha wananzengo,

Niiende kwa hoja moja kwa moja. Nina mke wangu ambae leo tunamiaka mitatu kasoro. Tumekuwa tukiishi vzr tu bila ugomvi na kama upo ile kupishana tu kauli.

Sasa kabla ya chirismas nilipanga safari ya kwenda mkoani Kagera, nikanunua mahitaji yote mf mchele, unga, mafuta, sabuni, ngano, maharage na vitu vingne ambavyo ni mahitaji.

Safari yangu ilikuwa ni ya week moja ambapo niliondoka j'2 na kurudi J'3 ya week iliyofuata. Sasa pesa za matumizi ya mboga ,labda mshumaa In case umeme umekata nilimpa shilingi 30,000.

Ndani wapo watu watatu mke wangu, mjomba wangu yaani mtoto wa dadaangu yupo form one na mwanangu mdogo ana mwaka mmoja na nusu.

Kabla ya siku mbili kuanza safari ya kurudi alinipigia simu anasema pesa imeisha ya matumizi, mwanamme mzima naiachia familia nzima elf 30000 kwa muda wa wiki nzima ,kwakweli nikaumia sana kwa maneno yale. Lakini kubwa zaidi nilivyomuambia kuwa anivumilie kwesho kutwa nakuja akasema bora hata upate ajali ufie huko usirudi kabisaa make mme gani huwezi kulea familia.

Mm kipato changu ni shiling laki tano kwa mwezi ila ninavyoona mke wangu anahitaji maisha ya kupato cha milioni. Maneno anayoniambia kama huwezi kulea familia subiri uje usaidiwe yamenikasirisha sana wakati mm ninatoa kile nilicho nacho.

Sasa ndugu zangu mwanamke kama huyo utamfanyaje?
Na kwa akili zako ukajua anaongea kuhusu hela na kulea familia?Utasaidiwa kweli!
 
JF kila mtu humu ni tajiri. Yaani mahitaji yote ya msingi yamo ndani mfano unga, mafuta, sabuni, mchele, maharage, mkaa,luku, nk. Halafu elfu 30 kwa wiki haitoshi???

Operation kataa ndoa acha iendelee tu hakuna namna. Kwa coments hizi nakushauri achana tu na huyo mke wakokumbe hakuna la maana unalolifanya kwake.
Inaudhi unapogundua unaishi na mwanamke anayeangalia matunzo na sio upendo! Yaani ndoa imegeuka kuwa ni kitengo cha matunzo kwa wanawake na sio upendo na kufurahia maisha! Utadhani huko walikokuwa kabla ya kuolewa walikuwa hawali kilichopo mezani wala hawavumilii yali yopo!
Baraka hufuata nyumba zenye furaha na upendo wa dhati! Wanawake badilikeni aisee kama mnajua kutunzwa anzeni kujitunza wenyewe msibebeshe mizigo watoto wa watu hii ni unyonyaji na sio fair!
 
Mkeo ni mpumbavu sana,hiyo pesa inatosha sema ana mambo yake mengine huyo
 
Back
Top Bottom