King Kong III
Platinum Member
- Oct 15, 2010
- 64,227
- 98,761
Mkuu, Mimi na wewe tunashindwa kuelewana, sababu hiyo 500k tunaiangalia kwa angle tofauti.
Wewe unachukulia as if kapokea 500k, then katoa 30k ndio kawaachia.
Mwanzo uliniuliza kama ninafamilia, na assume, unayo familia. Tuchukulie ni wewe ndio unapokea 500k per month, hivi mpaka ile siku unakuja kuipokea, ni kweli itakuwa Bado ni 500k?
Umekuja pazuri sana mkuu , kitu cha kwanza ni familia ,kama una kipato cha aina yeyote unaweza kuanzisha familia na kuhudumia kwa hicho kidogo au kikubwa unachopata.
Kama akipokea laki 5 kisha unasema sio chote atakuwa nacho means ameenda kulipa madeni? Mimi nachoelewa wanawake ni waelewa ukiwaambia ukweli kuhusu pesa atavumilia kwa muda! Kitendo cha kumuachia elfu 30 na ndiyo maana mkewe kampa sh!t kwasababu anajua anafanya mchezo mchezo!
Maisha ni haya haya ,wenye maDUNGU Jeshi ,wenye vibakuli na wenye "TZ Eleven aka Hamza Kanuni Mwendo wa Ngiri" wote tunanunua kwenye maduka na magenge hayo hayo! Ndiyo maana siku za minada unaona wenye mavogue na sie wauza mkaa tunaenda kushop na bei ni hiyo hiyo! Hapa nataka kusema hata kama umechoka kwa kipato haindoi uhalisia kwamba kipimo cha mkaa kopo moja ni buku jero(1,500/=) ,Nyanya nne Buku(1,000/=) ,Limao 500/= ,Mchele 3,300 , Mharage 4,000/=(Tena hapa wenye vipato vikubwa ndiyo wanatumia hela ndogo kwasababu wananunua vitu kwa ujumla na si reja reja,ananunua vitu vya week so inakuwa cheap).
Hauwezi kusema kwamba kipato chake ni kidogo hivyo ni sahihi kumuachia elfu 30 as if akienda gengeni/dukani atauziwa kwa bei ya wenye vipato vya chini wakati bei ni hizo hizo hata akija bakhresa au dangote atauziwa mchele kilo 3,300/=
Kiukweli 4,500/= kwa siku kuanzia asubuhi ,mchana na usiku haitoshi, utaigawa vipi itoshe? Kama issue ni kubana matumizi ni bora anunue unga kilo moja na chumvi ya mia 5 wawe wanapika uji tu mpaka siku kipato kikiongezeka.