Huyu mwanamke ni sahihi kuniambia maneno haya?

Huyu mwanamke ni sahihi kuniambia maneno haya?

Mkuu una familia kwanza? Mtu una kazi halafu unasafiri week nzima unaacha unga,maharage na mchele kisha unasema elfu 30 inatosha as if ni wafungwa wa kula maharagae kila siku ,mkaa ,mafuta ya kupikia ya kula etc? Mkaa kopo moja Tsh 1500 , Mafuta ya Taa lita rejareja 4000 ,nyanya nne buku.

Kama hawezi kulea familia bora amrudishe kwao..
kula maharage wiki nzima kuna shida gani?
 
Tatizo sisi wana ndoa huwa hatuelezi ukweli wote ikiwemo na picha shilingi upande wa pili, wewe hapo ulimwambia nini mpaka akaja kukujibu hivyo.
 
Aisee kuwa tegemezi tabu sana. Nikajua laki 3 kumbe elfu 30 yaani elfu 10 ziwe tatu. Pole yake huyo mkeo
Hiyo hela ni nyingi sana , iwapo vitu vingine kama gesi, umeme unga, mchele, mafuta yapo.
labda kama ni chuma ulete au ana genge.
 
Mkuu una familia kwanza? Mtu una kazi halafu unasafiri week nzima unaacha unga,maharage na mchele kisha unasema elfu 30 inatosha as if ni wafungwa wa kula maharagae kila siku ,mkaa ,mafuta ya kupikia ya kula etc? Mkaa kopo moja Tsh 1500 , Mafuta ya Taa lita rejareja 4000 ,nyanya nne buku.

Kama hawezi kulea familia bora amrudishe kwao..
Jikune pale unapoweza. Ambacho inabidi uelewe, matumizi ya mtu yanaendana na uwezo wake. Hapo wengi mnamshambulia jamaa, kwakua either mnachukulia reference familia zenu, au familia zenye kipato kizuri.

Jamaa amesema kipato chake kwa mwezi ni 500k, tuassume hiyo ni net amount. Movements zake za kila siku ili aweze kuleta kipato kingine, inabidi zianzishwe na hiyo hiyo 500k. Kuna vingi vya kufanya, sio kula peke yake, Panahitajika pia akiba ya dharura.

Matumizi mazuri ya hiyo hela, ndio yatawafanya wasilazimike kukopa au kuishi kwa madeni.

Unaposema kama hawez kulea familia, amrudishe kwao, hapo ni sawa na kusema ili uoe na kuanzisha familia, lazima uwe na hela nyingi sana, Hapana!

Tena huyo pamoja na jeuri aliyoonesha, kwao unaweza kuta wanamaisha magumu pia.

Mke akiwa na akili, familia lazima iwe stable
 
Mtu mwenye kipato cha 500k kwa mwezi hawezi kuachia familia Ths 30,000 kwa week nzima.

Kama issue ni kubana matumizi angewanunulia unga kilo moja na chumvi ya mia 500 tu wawe wanapika uji asubuhi mchana na usiku.
 
Habari za harakati za maisha wananzengo,

Niiende kwa hoja moja kwa moja. Nina mke wangu ambae leo tunamiaka mitatu kasoro. Tumekuwa tukiishi vzr tu bila ugomvi na kama upo ile kupishana tu kauli.

Sasa kabla ya chirismas nilipanga safari ya kwenda mkoani Kagera, nikanunua mahitaji yote mf mchele, unga, mafuta, sabuni, ngano, maharage na vitu vingne ambavyo ni mahitaji.

Safari yangu ilikuwa ni ya week moja ambapo niliondoka j'2 na kurudi J'3 ya week iliyofuata. Sasa pesa za matumizi ya mboga ,labda mshumaa In case umeme umekata nilimpa shilingi 30,000.

Ndani wapo watu watatu mke wangu, mjomba wangu yaani mtoto wa dadaangu yupo form one na mwanangu mdogo ana mwaka mmoja na nusu.

Kabla ya siku mbili kuanza safari ya kurudi alinipigia simu anasema pesa imeisha ya matumizi, mwanamme mzima naiachia familia nzima elf 30000 kwa muda wa wiki nzima ,kwakweli nikaumia sana kwa maneno yale. Lakini kubwa zaidi nilivyomuambia kuwa anivumilie kwesho kutwa nakuja akasema bora hata upate ajali ufie huko usirudi kabisaa make mme gani huwezi kulea familia.

Mm kipato changu ni shiling laki tano kwa mwezi ila ninavyoona mke wangu anahitaji maisha ya kupato cha milioni. Maneno anayoniambia kama huwezi kulea familia subiri uje usaidiwe yamenikasirisha sana wakati mm ninatoa kile nilicho nacho.

Sasa ndugu zangu mwanamke kama huyo utamfanyaje?
Mpwa.​
 
One day ni 50,000tsh hapo umenunua kila kitu ndani 100,000tsh per day kama hujanunua vitu ndani
 
Mtu mwenye kipato cha 500k kwa mwezi hawezi kuachia familia Ths 30,000 kwa week nzima.

Kama issue ni kubana matumizi angewanunulia unga kilo moja na chumvi ya mia 500 tu wawe wanapika uji asubuhi mchana na usiku.
Mkuu, Mimi na wewe tunashindwa kuelewana, sababu hiyo 500k tunaiangalia kwa angle tofauti.

Wewe unachukulia as if kapokea 500k, then katoa 30k ndio kawaachia.

Mwanzo uliniuliza kama ninafamilia, na assume, unayo familia. Tuchukulie ni wewe ndio unapokea 500k per month, hivi mpaka ile siku unakuja kuipokea, ni kweli itakuwa Bado ni 500k?
 
Mkeo hana busara. Hata kama 30,000 ni ndogo sana, hakupaswa kukwambia hayo maneno.

​
 
Mtu mwenye kipato cha 500k kwa mwezi hawezi kuachia familia Ths 30,000 kwa week nzima.

Kama issue ni kubana matumizi angewanunulia unga kilo moja na chumvi ya mia 500 tu wawe wanapika uji asubuhi mchana na usiku.
Mkuu mbona unakuwa mzito kuelewa, baadhi ya mahitaji ya muhimu kashanunua. Na matumizi ya pesa sio kula tu. Lazima na mambo mengine yaende. Ukiendekeza tumbo unawezajikuta unapiga mak tyme tu.
Hio 500k ni kubwa, labda kama ni kwa ajili ya kula tu.
Kuna bills zingine inabidi zilipiwe na pesa hio, kuwa open. Maskini nae ana haki.
 
inawezekana ni hasira msamehe tu rugeikamu,yaani 30 tena sikukuu kwakweli kama sio kutia hasira basi inahuzunisha
ushauri tu fanya hima umfungulie ka mradi ka kuingiza hata elfu tano ili akuboost pale unapolemewa
yaani hiyo hela ni ndogo mno,tena mna mtoto mdogo dharura ikitokea kwa mfano
nakuomba hii kwako iwe changamoto ya kuongeza bidii kwenye utafutaji,
 
Soma vizuri uzi wa jamaa mke wake alijitahidi kubana matumizi lakini kabla ya siku 2 jamaa arudi mke akampigia simu kuwa ile elfu 30 imeisha.

Kwa hiyo kwa mahesabu rahisi mke wa jamaa yetu kajibana bana katumia elfu 30 kwa siku 5

Hatujui kama wanapikia gesi mwanzo mwisho au huwa wananunua mkaa kupikia hayo maharage na mchele ambao jamaa kanunua? Hivyo vyote mume hajataja kwenye uzi wake au kama gesi ipo iliisha ikabidi akanunue, hatujui. Je, kuna siku umeme uliisha mke akanunua? Hatujui!

Ukiacha hayo pia nyumbani kunakuwa na matumizi ya dharura na ya ghafla wakati mwingine

Mke kajitahidi sana kosa lake ni kwenye kauli na hatujui ni nini kilipelekea mke aseme hivyo kwa sababu hapa tunasikiliza upande mmoja tu wa mume. Usikute mwanetu ndiye aliyeanza kumvuruga shemu

Ila kwenye matumizi elfu 30 kwa siku 5 mke kajitahidi kikweli
ni kweli kabisa,inawezekana jamaa aliongezea maneno ndo maana akajibiwe vile hapa jamaa atumie busara
 
Wanawake wengi wanacheza vikoba kwa hela za mtumiz ya familia...!! Ukilegea utakuwa unaliwa kekundu kila siku...!! Tulia akirudia mpe kichapo hakuna namna
 
One day ni 50,000tsh hapo umenunua kila kitu ndani 100,000tsh per day kama hujanunua vitu ndani
50,000 tsh kwa ajili ya kununua mboga na viungo tuu?? Unanunua nn aisee hata kama ni kuku wa kienyeji kila siku na sato kg 2 bado huwezi tumia 50k kwa siku kwa mboga na viungo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kumuachia 30k anakuombea ufe siku ukakosa hata jero si ndo anakupa sumu kabisa.
30k ni ndogo ila kama ndio iliyopo inaweza ikapangiliwa ikatosha.
 
Back
Top Bottom