Japo siamini kama ni kweli,lakini acha nikupe mbinu. Kama umefikia hatua ya kuwa na akiba ndani,unajiweza. Kitu kama hiki kiliwahi tokea. Ikawa hivi: siku moja,mwambie hapo hapawafai,unatafuta nyumba nyingine mhamie. Kama siku 2 badae, mwambie apangikie kila kitu,usiku mtahama. Chukua gari,pakia vyako. Vikiisha,begi lake shusha,panda gari. Mwambie mhusika,umekodi wewe,haingii mtu kasoro wewe na vitu vyako. Tembea.
Hili ukiona ni gumu,vitu vyote weka,mwambie kwenye gari hamtoshi,mtaenda na pikipiki. Utajua mwenyewe mazingira umeyaandaaje. Fika sehemu,agizeni hata soda. Toka kama unaenda uani,panda pikipiki. Begi la chupi utajua kama utalitunza,utamrudishia au utalitupa.
Ila sasa,somo umepata, uhuni na uzinzi acha. Shobo zako ndo chanzo cha hayo.