Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi ukiniambia anasimamia anachokiamini sikuelewi maana tumeshuhudia hapa majuzi katoka nje ya kikao cha kamati kuu akisema CCM hawajatenda haki, halafu baada ya mwezi mmoja anapanda jukwaani kumnadi huyo mtu aliyesema hakupitishwa kwa haki, huu msimamo wa kinafiki umenifanya nimshushe vyeo
Jamani Sita hafai kabisa.Tungekuwa na katiba mpya sasa hivi na hii matatizo ingekuwa hakuna.afadhali ya polepole kuliko sita.huku Jusa haingii...Polex2 ajaribu.
Nchimbi hawezi shika cheo chochote na kudumu, laana za wazee bado zinamtafuna, hawezi fika kokote, ndio mwisho wake pale alipo, huyu alimfanyia mabaya sana mzee Gama,
* AKICHAGULIWA, NCHI KUPATA SPIKA BORA KAMA "JOHN BERCOW" WA UINGEREZA
Uongozi ni mchakato wa ushawishi ndani ya jamii, kwamba mtu moja anapopata madaraka uwasaidia wengine kukamilisha malengo ya pamoja.
Uongozi ni kuvuka mipaka ya mazoea na kuanzisha mchakato wa mabadiliko inayowasaidia watu kufikiri, kushiriki na kufikia malengo kwa tija na ufanisi mkubwa. Katika mbio hizi za kumtafuta Spika wa bunge la JMT lazima tukiri wengi waliojitokeza wana sifa ila ni vyema pia tukakiri ya kwamba Dr. E. Nchimbi ana sifa za ziada dhidi ya wengine...
1. Anawaza Mafanikio Makubwa
Kiongozi bora lazima awe na maono juu ya kuhakikisha kuwa nchi yake, kampuni yake au eneo lolote alilofanyia/analofanyia kazi inapata mafanikio makubwa. Tumeshuhudia hilo kwa Dr. Nchimbi alipokuwa UVCCM, serikalini katika wizara mbalimbali na idara mbalimbali..
2. Ana Nia
Haitoshi tu kwa kiongozi kuwa na mawazo bali kiongozi mzuri lazima awe na nia ya kutimiza. Kiongozi mzuri na bora atafaa kuchaguliwa kuwa kiongozi endapo atakuwa na uwezo wa kuratibu na kutekeleza alichowaza, ajue njia anayopita na kuwatangulia anaowaongoza kwa vitendo. Dr. Nchimbi ana sifa hii
3. Kujitambua
Lazima kiongozi ajitambue mwenyewe ni mtu wa namna gani, ajue uwezo wake na mapungufu yake na awe tayari kujiongeza maarifa kila siku, ili aweze kupokea changamoto na mabadiliko. Dr. Emmanuel Nchimbi ana sifa hii
4. Msimamizi wa Maamuzi
Katika maisha ya siasa, mara nyingi malengo hukumbana na vikwazo. Hivyo ni wajibu kwa kiongozi kusimamia maamuzi sahihi na kwa wakati. Dr. Emmanuel Nchimbi ana sifa hii
5. Kukubali Kukosolewa
Viongozi wengi wasiokuwa na sifa za uongozi huwa hawakubali kukosolewa, wakidhani kuwa hivyo ndio njia ya kuthibitisha usahihi wao. Kiongozi makini ni yule ambaye atakuwa tayari kukosolewa na kuwapongeza wanaomkosoa. Dr. Nchimbi ni kiongozi anayekubali kukosolewa...
6. Kuwa Msikilizaji
Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kuwasikiliza walio chini yake, wakubwa, apokee maoni yao na ikiwezekana ayafanyie kazi. Dr. Nchimbi kalionyesha hili alipokuwa UVCCM, wizara mbalimbali alizopita, ndani ya NEC na CC. Huyu ndio tunamhitaji katika nafasi ya spika wa bunge la JMT
7. Kufata Haki
Kiongozi imara anatakiwa kufata haki. Asijione au kuona kundi fulani ina haki zaidi ya wengine katika sheria. Ni muhimu kwake kuonyesha jamii wako huru katika mawazo na matendo. Dr. Nchimbi marazote amekuwa mfano wa kuubiri HAKI na Amekuwa muumini wa haki.
8. Kuwa Egemeo la Watu
Kiongozi lazima awe egemeo la watu katika shida na raha. Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kusikitika, kuomboleza au kufurahi pamoja na watu anaowaongoza bila kujitenga nao. Na kubwa zaidi ajitolee kuwatumikia watu kwa hali na mali. Dr. Nchimbi katika hili ni mfano wa kuigwa. Amefanya hayo UVCCM, serikalini na wizara mbalimbali..
9. Kukubali Lawama
Kiongozi mzuri ni yule anayediriki kukubali lawama, awe amefanya au la. Anachotakiwa kufanya ni kukubali kulaumiwa. Dr. Nchimbi ni mfano wa kuigwa katika hili, amewahi kubeba lawaza zisizo zake kwa sababu anaelewa dhana ya dhamana na ni kiongozi aliyeiva.
10. Utatuzi wa Matatizo
Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa kuzuia migogoro na kuitatua kwa haraka. Muongozo bora katika hili ni kusimama katika mawasiliano bora na watu unaofanya nao kazi. Hakuna shaka kwamba Dr. Nchimbi ni wa kuigwa katika hili. Amefanya hili akiwa ndani ya UVCCM, wizara mbalimbali na katika vikao vikubwa vya kimaamuzi..
11. Uaminifu/Ukweli
Kiongozi mzuri na bora ni yule aliyemwaminifu na mkweli. Ni yule atakayekuwa tayari kuonyesha ubora wa matendo na kauli zake. Dr. Nchimbi amekuwa mfano katika hili..
12. Mbunifu
Kiongozi mzuri ni yule anayejua au kubashiri nini kitatokea kesho kulingana na mienendo ya jamii. Baada ya kugundua hilo ni wajibu wake kuwa mbunifu na kuzuia madhara kutokea. Dr. Nchimbi ni kiongozi aliyembunifu, ndio maana katika kipindi chake UVCCM tulishuhudia jumuiya iliyoimara na kulinganishwa na jumuiya zenye nguvu kama ANC Youth League au iliyokuwa KANU Youth 1992...
13. Mfuatiliaji wa Katiba, Taratibu, Sheria na Kanuni za kiutendaji na kiuongozi...
Lazima tukubaliane kuwa uongozi ni utaratibu na sio maamuzi ya watu fulani. Ni taratibu, sheria na kanuni zinazowekwa kufikia malengo. Dr. Nchimbi marazote amekuwa muumini wa kufanya kazi zake kwa kufata utaratibu, sheria, na kanuni husika..
NB: Ni jambo la wazi kwamba kumchagua Dr. Nchimbi kuwa spika wa bunge la 11 la JMT nchi itakuwa imepata spika bora, mahiri na shupavu kama "John Bercow" wa House of Commons. Dr. Nchimbi ana uwezo, ana sifa, na kubwa zaidi anatosha..
Note: Haya ni mawazo huru, hayana muingiliano na kundi lolote!.....
Hafai kuwa spika. Bado ana u-uvccm sana. Bado ni kada sana wa ccm kiasi kwamba hawezi kuwa fair kwenye uspika. Hiyo nafasi inamfaa aidha Ndugai au ZunguTwende na Nchimbi
Ni msomi
Ni kijana
Ana uwezo
Ana uzoefu mkubwa
Anaweza kuunganisha watu wa mitizamo tofauti
Ni mwanadiplomasia
Ana kipaji cha uongozi
Ni rika la wabunge waliowengi ktk kipindi hiki
Anaijua ccm ndani nje
Anaijua nchi yetu
Anaweza tumsaidie atalisaidia bunge.