Huyu ndio mtoto mwenye akili nyingi kuliko wote Tanzania 2024

Huyu ndio mtoto mwenye akili nyingi kuliko wote Tanzania 2024

Huyu mtoto ukimsikiliza ana uwezo mkubwa sana wa kujieleza na kufanya hesabu.
Anajibu maswali ambayo hata wewe huwezi kuyajibu hapo ulipo saivi
View attachment 3159995
Ee Mungu tunakuomba huyu mtoto asiharibiwe na mfumo wa elimu yetu.

Mtumie huyu mtoto kuonyesha ukuu wako.

Amen na Jumapili njema

WE PROTECT THIS YOUNG ANGEL BY BLOOD OF JESUS. AMEN
Nilishawahi kukasikia tangu mwaka Juzi, sijui ni ka wapi haka katoto! Kalikuwa kanataja mpaka majina ya marais na Mawaziri!
 
Kwamba ulipita vijiji na tarafa zote nchini ukafanya tathmini kujua huyo ndiye mwenye akili kuzidi wote nchini? Acha mtindio wa akili
 
Kwamba ulipita vijiji na tarafa zote nchini ukafanya tathmini kujua huyo ndiye mwenye akili kuzidi wote nchini? Acha mtindio wa akili
Mwombe Mungu akupe uwezo wa kupima vitu kwa haraka. Huyo mtoto ni mdogo sana kuelewa vitu kama hivyo.
 
Mwombe Mungu akupe uwezo wa kupima vitu kwa haraka. Huyo mtoto ni mdogo sana kuelewa vitu kama hivyo.
Ni mtoto wa shangazi yako? Huyo atakua na akili kuliko ndugu zako tu,huwezi kuchukua takwimu za kifamilia ukazifanya za kitaifa.
 

Tazama hiyo video kisha nikupe ushauri wa kiroho.
Yapo mapepo ya ufahamu pia, hivyo usifurahie tu kuwa umepata mtoto genius, muda mwingine mwekee mkono kichwani kwa mamlaka ya kimungu unaweza kuona analipuka mapepo.
Mara nyingi mapepo haya huambatana na Imani . Kuna watoto wanaitwa Shariff kwa lugha za Kiarabu, hawa watoto mpaka makanisani wamo . Katika huduma zangu za kiroho nimewahi kukutana na vihoja vingi. Kama si mtu wa rohoni utapokea kila utakaloletewa.
But mwisho wa safari hawana impact yoyote kwa Taifa.
 
Nilishawahi kukasikia tangu mwaka Juzi, sijui ni ka wapi haka katoto! Kalikuwa kanataja mpaka majina ya marais na Mawaziri!

Mtoto mwenye mwaka na nusu had miaka mi 4 ana uwezo mkubwa sana wakushika vitu ki mtiririko utadhan ana soma mahali..
Hata mtoto wako anaweza kuwa hivyo ila uwe una jua Namna yakumuelekeza tena kwa wakati mfupi sana..

Tatizo miaka kama hii sisi tunawatamkia maneno kama wanavyotamka kimakosa mtu anamtamkia mtoto MMA badala ya Maji. Nae atachukua muda sana kubadilika kujua jina sahihi.
Pia ndo muda wakuta tunawasikilizisha manyimbo na mambo mengine ambayo wakiwa wanafanya si tunacheka badala ya kuwafundisha

Ndo maana ndo umri watoto wanakuwa katika kufanya vituko vingi ambavyo hautarajii yeye kufanya
 
Kama mtoto wa age hiyo anaweza kuhesabu hadi 50 kwa kiswahili na kingereza hawezi kushindwa hivyo endapo utamfanyia routine ya kila siku ya kukariri
 
Hata kama kamekariri siyo kosa kanauwezo mkubwa sana! Anaebisha ebu akariri na yeye kama nirahisi!

Wengi wanaobisha walipokuwa na umri kama huo walikariri harufu ya maziwa ya mama tu bhaasi!

Iwe kakaririshwa au kameza haiondoi uwezo wake ni mkubwa mno!
Kukariri takwimu siyo jambo dogo
 
Akili ni nini!?

Je kuhifadhi kwa wepesi, kuhifadhi jambo kwa muda mrefu, kuwa na kumbukumbu nzuri? Ama uwezo wa kutatua mambo katika namna tofauti tofauti.

Hapo dogo kaonesha ana uwezo wa kumeza, ila sio ana akili nyingi.
Tukifundishwa 1 jumlisha 1 ni 2, 3+2 ni 5 na tukafundishwa imepatiknaje kisha tukapewa swali maandazi ma5 ukipewa na vitumbua vitatu na chapati sifuri, utakuwa na vitafunwa vingapi.
Ule uwezo wa kuchanganua hilo swali, kujua linahitaji kujumlisha japo hakuna sehemu imesemwa jumlisha, kwangu mimi huyu ndio mwenye akili.
Na si lazima iwe kwenye hesabu tu, hata mazingira yoyote yale.
 
Ni vyema tuwe tunaleta video kama hizo hapa jukwaani ili kuutukuza ukuu wa Mungu.
Kuna vitoto vya madurasa vimekariri Qoran nzima na hadithi sijui za Ibn Omar!

Sasa, hiyo siyo akili. Kuwakaririsha watoto mavitabu ya kishamba kama bibilia na Kuruani ni kuendeleza ujinga na ujima katika jamii.

Watoto wafundishwe vitu vya maana.
 
Back
Top Bottom