Huyu ndio mwanaume ninayemtaka, sitaki kuumiza moyo wangu una thamani

Huyu ndio mwanaume ninayemtaka, sitaki kuumiza moyo wangu una thamani

Mbona Miaka yako hujataja?? Ila unataka 34+...Taja na ya kwako kwanza
 
Kumpenda mtu ni kuzipotezea kasoro zake na kuangalia mazuri yake sasa bi dada umesahau kwamba maisha ni mtihani sasa ikiwa ni mtihani kwanini achague maswali ya kuulizwa , we subiri watu waje ukija kumkuta ana madhaifu kama ka uchafu au hana baadhi ya vitu ni kupambana na hali lakini hayo mengine yote unayoyataka ni ya kwenye tamthilia sio uhalisia , ukimpata wa hivyo njoo nikupe zawadi
 
Sasa huu ni upunguani, usikute Malaya, kila mtu kachovya, au sura mbayaaa, kuna mmoja alishawahi kutoa tangazo lake hapa, sifa kibao, nikamfata pm. Tukajadiliana, nikamtumia picha za uongo, basi akaingia mwenyewe. Akanipa namba, tukuanza kuchati, siku nakutana nae Mungu wangu, asee hapana nilimuuliza Mara mbili mbili ni wewe mwenye I'd hii, ooh ni Mimi. Nakapiga stori pale, tulipoacha tu, nikablock kabisa namba zake. Sasa usikute anatajia sifa nyingi kumbe mtu mwenye wa hovyo hovyo
We kaka mi naomba kukutana na wewe
 
Wanaume mtandaoni siku hz hakuna ...ww tembelea daladalani huko na vibanda vya mpira utampata mwenye sifa hzo [HASHTAG]#amini[/HASHTAG]
 
Wanaume hawavuwi na maneno mengi, kwa vigezo hivyo utasubiri Sana. Zaidi sana utamegwa na kukimbiwa kama ilivyokua ada. Maana wanaume hakuna mbinu wasiyoijua.
Kua na maneno machache yenye mvuto. Utapata haraka
 
Ukimbaumbau na umri umenikosesha mke...Nina 28 Dada...kama unaweza nifikiria
 
Chura ya kupiga makofi wakati wa mambo yetu yale ipo au umekuja tu kutusumbua hapa?![emoji32][emoji32][emoji32]
 
Wakuu salaam.

Kwa malezi niliyolelewa mimi sistahili kufanya ili jambo, pia kwa mira na desturi za kiafrika sistahili kufanya hiki kitu, lakini huu moyo ni wangu, na mmiriki wa moyo wangu ni mungu. Sasa nikajiuliza kwa nini niendelee kuumia? Hakuna sababu ya kuendelea kuumia? ingawa najua mwanamke kumtafuta mwanaume ni aibu kubwa, ila nikawaza kwakuwa kuna sababu ambayo najua ni muhimu sana akipatikana na nikampenda nitamuweka wazi na atanielewa. Mamayangu amenilea vizuri kwa maadili na heshima, nina Imani ninachokiandika hapa mungu yupo anashuhudia,

Wale mtakaokuja kuniponda eti kwa nini nitafute mtandaoni huku niishiko hawapo? Jibu ni kwamba wapo kibao na wengine nikiri wananililia kunioa but, for the sake of my heart wacha niweke wazi mwanamme ninae mtaka staki wahuni mm sio mhuni mung undo shihidi.

SIFA ZA MWANAUME NINAE MTAKA.

1. Awe na mama yake mzazi/mlezi lakini akiwa na wazazi wot itapendeza sana.kama hana wazazi basi sawa ni mpango wa mungu ingawa itaniuma sana,

Why awe na mama yake? wakuu nataka kumuona huyu mwanamke duniani kote yeye ndo atokee anizalie mme? Nataka kumuona nimwambie ‘mama asante kwa kubeba mimba miezi 9 ukanizalia mwanaume wa ndoa nitakupenda kama mama yangu mzazi.’

2. Awe msafiiiiii. Narudia tena awe msafi kupitiliza spendi mwanaume mchafu sipend aina yeyote ya uchafu, No no nataka siku nikikutana nae macho yangu yadhibitishe kuwa ni msafi,yaan kuanzia kwake ndani mavazi awe smart.

3 Awe mrefu.

4. Rangi Yeyote hainipi shida ila akiwa na ka uweusi Fulani atanoga

5. Awe anajua kuvaa. kama hajui kuvaa smart nitamfundisha hii sector niko vizuri sana

6. Asiwe mwembamba. nataka zawadi za nguo nitakazokuwa nampa zimkae vizuri yaan awe na body size ya kati.(gentleman

7.Awe ana upendo. jamani kama mimi.nasisitiza kama una roho ya paka usijidanganye nataka nionje taste of love

8 Awe ana care, jamani awe na mkono mwepesi hata akinipa pipi ina thamani kwamgu, namiss hii kitu mm natoa sana nikimpenda mwanaume siwezi kutoka mjini bila kumnunulia chochote nguo ndo usiseme.

9.Awe kristo rc na mcha Mungu

10. Awe na miaka 34+ ni lazima.

11. Awe ameshafika stage Fulani ya maisha. Staki mwanaume tegemezi, atleast awe na mradi mmoja wa kumuingizia pesa tofauti na ajira.staki mwanaume mzembe ambae hajui kutafuta pesa. Inshort awe na mipango ya kuwa somebody na future nzuri .staki mwanaume anaemiliki p.u.m.b.u na smartphone.mm ni mtafutaji staki mwanaume wa ovyo.

12,Awe na kucha zote miguuni, napenda weekend nikimkata vizuri kucha zikae fresh avae sandles sometimes pensi fulan amaizing atoke bomba.

13 Asiwe alishawahi kuoa wala kuwa na mtoto nje ya ndoa, Mtoto ni Baraka ila watoto wa nje ya ndoa wanaleta migogoro .staki mme wa mtu mm.

14. elimu degree, masters phd vyote sawa.
15 asiwe mhaya .plz naomba msinielewe vibaya samahani sana mnisamehe


SIFA ZANGU

1. Namshukuru mungu kunipa upendo nina upendo kwa kila mtu

2. Mimi ni msafiiiiiiiiii yaaani ni msafiiiii kupitiliza

3. Nimeajiriwa ila nimejiajiri kimradi changu kidogo pemben tho sipendi kuajiriwa ndo mana nataka mwanaume ambae atanipa sapport tupanga miradi tuwe na maisha bora.

4. Elimu –degree

5. Rangi –mweusi kiasi

6. Urefu size ya kati umbo mm sio bonge.

7. nacare sana nikimpenda mtu nampenda kwa vitendo

8. Sijawahi kumsaliti mtu

9. Dini mkristo –rc

10, najitegemea sitegemei mwanaume vitu vidogovidogo nina uwezo navyo in short mm ni mtafutaji.

11mimi ni mcha mungu.

12 napenda sana competition sipend mme wangu azidiwe na wanaume wengine hasa kimaendeleo

13 sina mtoto na sijawahi kuolewa.

14 nina akili ya maisha yaani IQ yangu ipo juu saa upstairs niko vizuri.

15 Mm ni mchangamfu sana mcheshi namshukuru mungu kuniumba hivi.

16. mm ni mvumilivu ila ikiwa too much, siwezi kuvumilia tena.

N.B. Mimi ni binadamu sijakamilika nina mapungufu yangu lakini hivyo kidogo mungu alichonijalia kinaendana na ukweli niliouandika hapa. hasa sifa zangu.


NOTE. Ningependa nikutane na mwanaume ambae alishawahi kuishi nje nchi yaani ana exposure ya mambo mengi nina sababu ya msingi hasa kimaendeleo / biashara LAKINI AKIDHI VIGEZO VYOTE NO 1-15 . lakini kama hajawahi kuishi nje na ana vigezo hakuna mbaya najua nikiwa nae tutafika mbali.


NINAVYO MISS.

1. Mme wamgu uko wapi? Nimekusubiri nimejitunza nimechoka kukusubiri

2. Nimemiss kukumbatiwa miaka sasa

3. Nimemiss kukiss staki kukiss na jitu la ajabu lichafu

4. Nimemiss kubebwa

5. nina upweke staki kukaribisha vijianaume vya ajabu kwangu

6. Uko wapi baba nikupikie uone ninavyojua kupika.

7. Njoo uone nilivyo msafiii sijawahi kuingiza mwanaume kwangu njoo uone kwangu nilivyo msafi

8. Njoo uone ninavyojipenda

9. Njoo nikuoneshe upendo
10 Njo baba mama yangu anataka kukuona.
11. Namiss neno baba njoo nikuite baba.

Kiukweli nimeniss vingi sana sio kwamba nilipo hakuna wanaume wapo wengi kazini ila nataka wangu wa moyo nimuoneshe upendo nae anioneshe maana hiki ndicho ninachokimiss kutoka kwa mtu nimpendae.

Mwisho mm ni mwanamke ninaejitambua wale ambao mtakuja hapa kunitusi eti nichonge au nizae mme wangu nawaomba tafadhari mkae kimya najua ninachokita. na nina imani huyu mtu mwenye sifa hizi yupo.

Angalizo.

kama unajua huna vigezo hivyo hapo juu plz usijisumbue kuja pm maana niko makini, najua kuna vitoto vinavyomiliki laptop baada ya kupaya mkopo wa board vitakuja plz tuheshimiane ninaomba.



Karibuni.
Naomba kujua Umri wako kwanza.
 
nisamehe tuuu nakuomba
Sina cha kukusamehe maana hujanikosea kitu, ukweli upo hivi binafsi God blessed me with karibu na kila kitu ulichoandika, ingawa mchumba wangu ni mdada wa kawaida mno, ila ana IQ kubwa mno, me the same ila sikuwahi kufikiria kuwachagua wanawake kwa sura, maumbo yao, akili zao, zaidi nilimwomba Mungu akanipa moyo wa kutowapenda wanawake wahuni, malaya, wenye majivuno na wenye dharau hakika Mungu siyo John wala Abdarallah nashukru ameniepusha na wadada kama wewe.

Nasikitika kuwa unadai kuwa na IQ kubwa but sina uhakika, mwisho mke/mume bora utoka kwa Mungu. katubu...!
 
wewe ni kenge... alafu unaonekana umri umeshaenda ndio maana unataka kuolewa, nkwambie kitu ? finyanga mwanaume wako umpe sifa zote unazozihitaji, .... i bet wewe ni 30plus, utazeekea kwenu ukichagua
 
Eti P.U.M.B.U na Smartphone. Halafu unasema wewe ni una mcha Mungu.
 
Back
Top Bottom