Huyu ndio mwanaume ninayemtaka, sitaki kuumiza moyo wangu una thamani

Huyu ndio mwanaume ninayemtaka, sitaki kuumiza moyo wangu una thamani

Wakuu salaam.

Kwa malezi niliyolelewa mimi sistahili kufanya ili jambo, pia kwa mira na desturi za kiafrika sistahili kufanya hiki kitu, lakini huu moyo ni wangu, na mmiriki wa moyo wangu ni mungu. Sasa nikajiuliza kwa nini niendelee kuumia? Hakuna sababu ya kuendelea kuumia? ingawa najua mwanamke kumtafuta mwanaume ni aibu kubwa, ila nikawaza kwakuwa kuna sababu ambayo najua ni muhimu sana akipatikana na nikampenda nitamuweka wazi na atanielewa. Mamayangu amenilea vizuri kwa maadili na heshima, nina Imani ninachokiandika hapa mungu yupo anashuhudia,

Wale mtakaokuja kuniponda eti kwa nini nitafute mtandaoni huku niishiko hawapo? Jibu ni kwamba wapo kibao na wengine nikiri wananililia kunioa but, for the sake of my heart wacha niweke wazi mwanamme ninae mtaka staki wahuni mm sio mhuni mung undo shihidi.

SIFA ZA MWANAUME NINAE MTAKA.

1. Awe na mama yake mzazi/mlezi lakini akiwa na wazazi wot itapendeza sana.kama hana wazazi basi sawa ni mpango wa mungu ingawa itaniuma sana,

Why awe na mama yake? wakuu nataka kumuona huyu mwanamke duniani kote yeye ndo atokee anizalie mme? Nataka kumuona nimwambie ‘mama asante kwa kubeba mimba miezi 9 ukanizalia mwanaume wa ndoa nitakupenda kama mama yangu mzazi.’

2. Awe msafiiiiii. Narudia tena awe msafi kupitiliza spendi mwanaume mchafu sipend aina yeyote ya uchafu, No no nataka siku nikikutana nae macho yangu yadhibitishe kuwa ni msafi,yaan kuanzia kwake ndani mavazi awe smart.

3 Awe mrefu.

4. Rangi Yeyote hainipi shida ila akiwa na ka uweusi Fulani atanoga

5. Awe anajua kuvaa. kama hajui kuvaa smart nitamfundisha hii sector niko vizuri sana

6. Asiwe mwembamba. nataka zawadi za nguo nitakazokuwa nampa zimkae vizuri yaan awe na body size ya kati.(gentleman

7.Awe ana upendo. jamani kama mimi.nasisitiza kama una roho ya paka usijidanganye nataka nionje taste of love

8 Awe ana care, jamani awe na mkono mwepesi hata akinipa pipi ina thamani kwamgu, namiss hii kitu mm natoa sana nikimpenda mwanaume siwezi kutoka mjini bila kumnunulia chochote nguo ndo usiseme.

9.Awe kristo rc na mcha Mungu

10. Awe na miaka 34+ ni lazima.

11. Awe ameshafika stage Fulani ya maisha. Staki mwanaume tegemezi, atleast awe na mradi mmoja wa kumuingizia pesa tofauti na ajira.staki mwanaume mzembe ambae hajui kutafuta pesa. Inshort awe na mipango ya kuwa somebody na future nzuri .staki mwanaume anaemiliki p.u.m.b.u na smartphone.mm ni mtafutaji staki mwanaume wa ovyo.

12,Awe na kucha zote miguuni, napenda weekend nikimkata vizuri kucha zikae fresh avae sandles sometimes pensi fulan amaizing atoke bomba.

13 Asiwe alishawahi kuoa wala kuwa na mtoto nje ya ndoa, Mtoto ni Baraka ila watoto wa nje ya ndoa wanaleta migogoro .staki mme wa mtu mm.

14. elimu degree, masters phd vyote sawa.
15 asiwe mhaya .plz naomba msinielewe vibaya samahani sana mnisamehe


SIFA ZANGU

1. Namshukuru mungu kunipa upendo nina upendo kwa kila mtu

2. Mimi ni msafiiiiiiiiii yaaani ni msafiiiii kupitiliza

3. Nimeajiriwa ila nimejiajiri kimradi changu kidogo pemben tho sipendi kuajiriwa ndo mana nataka mwanaume ambae atanipa sapport tupanga miradi tuwe na maisha bora.

4. Elimu –degree

5. Rangi –mweusi kiasi

6. Urefu size ya kati umbo mm sio bonge.

7. nacare sana nikimpenda mtu nampenda kwa vitendo

8. Sijawahi kumsaliti mtu

9. Dini mkristo –rc

10, najitegemea sitegemei mwanaume vitu vidogovidogo nina uwezo navyo in short mm ni mtafutaji.

11mimi ni mcha mungu.

12 napenda sana competition sipend mme wangu azidiwe na wanaume wengine hasa kimaendeleo

13 sina mtoto na sijawahi kuolewa.

14 nina akili ya maisha yaani IQ yangu ipo juu saa upstairs niko vizuri.

15 Mm ni mchangamfu sana mcheshi namshukuru mungu kuniumba hivi.

16. mm ni mvumilivu ila ikiwa too much, siwezi kuvumilia tena.

N.B. Mimi ni binadamu sijakamilika nina mapungufu yangu lakini hivyo kidogo mungu alichonijalia kinaendana na ukweli niliouandika hapa. hasa sifa zangu.


NOTE. Ningependa nikutane na mwanaume ambae alishawahi kuishi nje nchi yaani ana exposure ya mambo mengi nina sababu ya msingi hasa kimaendeleo / biashara LAKINI AKIDHI VIGEZO VYOTE NO 1-15 . lakini kama hajawahi kuishi nje na ana vigezo hakuna mbaya najua nikiwa nae tutafika mbali.


NINAVYO MISS.

1. Mme wamgu uko wapi? Nimekusubiri nimejitunza nimechoka kukusubiri

2. Nimemiss kukumbatiwa miaka sasa

3. Nimemiss kukiss staki kukiss na jitu la ajabu lichafu

4. Nimemiss kubebwa

5. nina upweke staki kukaribisha vijianaume vya ajabu kwangu

6. Uko wapi baba nikupikie uone ninavyojua kupika.

7. Njoo uone nilivyo msafiii sijawahi kuingiza mwanaume kwangu njoo uone kwangu nilivyo msafi

8. Njoo uone ninavyojipenda

9. Njoo nikuoneshe upendo
10 Njo baba mama yangu anataka kukuona.
11. Namiss neno baba njoo nikuite baba.

Kiukweli nimeniss vingi sana sio kwamba nilipo hakuna wanaume wapo wengi kazini ila nataka wangu wa moyo nimuoneshe upendo nae anioneshe maana hiki ndicho ninachokimiss kutoka kwa mtu nimpendae.

Mwisho mm ni mwanamke ninaejitambua wale ambao mtakuja hapa kunitusi eti nichonge au nizae mme wangu nawaomba tafadhari mkae kimya najua ninachokita. na nina imani huyu mtu mwenye sifa hizi yupo.

Angalizo.

kama unajua huna vigezo hivyo hapo juu plz usijisumbue kuja pm maana niko makini, najua kuna vitoto vinavyomiliki laptop baada ya kupaya mkopo wa board vitakuja plz tuheshimiane ninaomba.



Karibuni.
Umekosea mara 2 hapa:
Kigezo no. 1 umetutenga na kututonesha donda sie tuliokwishapoteza mama zetu tuliowapenda sana. Mungu anakuona!

Kigezo no. 13 unamtaka mwanaume mwenye miaka 34+ (na umesema umri huo ni lazima) ila asiwe aliwahi kuoa wala kuzaa mtoto. Kwa umri huo kama utampata ujue basi huyo sio rizki...
 
Dah! Pole sana bi dada, mwanaume wa vigezo vyote 15 hutampata popote pale duniani trust me. Labda YESU ndo atakuwa na vigezo vyote hvyo na nyongeza juu!


Ushauri: omba MUNGU upate mwanaume mwenye kujielewa, mwajibikaji, mchapa kazi na mwenye hofu ya MUNGU, pia mwenye UPENDO wa dhati. Vingine hvyo unatengeneza mwenyewe ukishampata.

Kila la kheri katika utafutaji wako mwaya
 
Pamoja na vigezo viiingi ambavyo vingi more idealistic than realistic, mwanaume hawi msafi kupitiliza, usafi utaenda kumfanyia wewe, ukipata huyo msafi kupitiliza halafu baadae ukagundua kitu cha ajabu sana usirudi kutulilia hapa.
Hahaha kitu cha ajabu sana!

Happy birtbday hommie Asprin

Cc Sky Eclat Miss Natafuta na baby espy

Bcc Daby
 
Dah kwa Hiyo sisi akina che nkapa tuwaoe kina nani na ufupi wetu kama nyundo ? na vidole kama Tangawizi ?

Masharti haya ni rahisi sana kufundisha Harvard's na cheti changu cha veta kuliko kuwa mme wako

Kila la kheri lakini
 
Mi nimemeet kigezo kimoja tu cha Dini...eeh na cha umri...sijui mwenzangu Asprin
 
Utasubiri sana mwisho wa siku utakuwa single mother hakuna mwanaume kafika 34 hajaoa na kama yupo hawezi kuwa husband material very sory ushaur wa bure tafuta vbenten under 25 umlee na umpakate utakavyo
 
Back
Top Bottom