Nakushauri usifanye matangazo ya mume mitandaoni, kama Kweli ni mcha Mungu, mwombe Mungu kwa imani atakupa anayefanana na wewe, kuna Siri kubwa kwa Mungu Kuhusu mume/mke, Kwani Mwenza mwema ana zaidi ya sifa ulizozitaja, unaweza pata mwenye sifa hizo ukashangaa msimalize hata mwaka, sifa za macho hazitakupa furaha kwenye ndoa, NARUDIA mume ni zaidi ya sifa uzitakazo. Mungu peke ake atakupa akufaaye, ila uwe mcha Mungu kwelikweli na kumbuka ucha Mungu sio kuacha uzinzi tu, ni pamoja na ulevi, umbea, uchoyo, dharau, kiburi, fitina na mengine yanayofanana na hayo bila kusahau kusamehe, kuwaombea na kuwajali wengine na kuwa mtoaji kwa wahitaji na kanisani (kama bibilia inavyoelekeza)