Huyu ndiye binti wa Mwl Mwakasege ambaye ni mmoja wa marubani aliyerusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli

Huyu ndiye binti wa Mwl Mwakasege ambaye ni mmoja wa marubani aliyerusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli

Wakuu Habarini

Kuna post zimekuwa zikisambaa mitandaoni zikimuonyesha mmoja wa marubani ambaye ni mtoto wa Mwl Mwakasege, na kila mtu akizumzungumzia lake + kumpongeza kwa ndoto zake.

Huyu ni mmoja wa marubani wawili waliorusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli. Anaitwa Anna Tusajigwe Mwakasege. Ni binti wa pili wa Mwalimu Christopher na mama Diana Mwakasege.

Anna alipata maono ya kuwa rubani akiwa darasa la 3 tu. Baba yake akampeleka uwanja wa ndege angalau kuona ndege "live" badala tu ya kuziona angani tu. Alipofika darasa la 5 baba yake alitembeza uwanja mdogo wa ndege Arusha ambapo alipata nafasi ya kuongea na marubani kuhusu ndoto yake, nao wakampa ushauri masomo ya kusoma ili aweze kuifikia ndoto hiyo.

Alijifunza urubani Afrika kusini, na siku anarusha ndege kwa mara ya kwanza baba yake hakulala usiku huo (hii ni story ya wakati mwingine).

Lakini kwa sasa Anna ni miongoni mwa marubani wa shirika la ndege ATCL. Kabla ya kujiunga na ATCL alifanya kazi mashirika mengine makubwa ya ndwge kama SAA na kupata uzoefu wa kuendesha ndege kubwa kama Boeing 747, Boeing 777 na Airbus A340.

Hongera Anna kwa kuaminiwa kuendesha ndege iliyobeba mwili wa Rais. Umeweka alama kubwa kwa taifa hili, ambayo haitafutika kirahisi. Mara zote tutakapokumbuka kifo cha JPM tutakumbuka kuwa wewe kama Senior First officer na rubani mwenzio (kiongozi) ndio mlipata neema ya kubeba mwili wake.

Najua si kazi rahisi kuendesha ndege ukiwa na majonzi ya kumpoteza Rais wako lakini umeaminiwa na umeweza. Tunawaombea kwa safari ya Zanzibar, Mwanza na Chato. Wewe pamoja na cabin crew yote. Hakika wanawake mnaweza. View attachment 1732239
Kwa kweli anaishi katika ndoto zake, kutimiza ndoto malengo ni jambo la kumsifu Mungu sio kazi rahisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wangapi wamezaliwa kwenye pesa wakaishia kuwa mashoga wanahonga wanaume wawabandue?
Wangapi wamezaliwa kwenye pesa wakaishia kuwa mateja?
NB:-
Sio kila Mchungaji ni mwombaji, ndio maana wachungaji wengine shetani anawapiga kikamilifu
Haswa Chief
 
umezungumzia tishio la kupanda juu

na mwenzako kauliza eti ameolewa? kwa Mnyakyusa naona tabia na mila hataziacha bado mwanamume atakuwa juu kwake
Kuna jamaa yangu kaoa mwaka jana, lakini miezi hiyo alikuwa akimfuatilia (Kumchumbia si kirasmi) kwa hiyo naona hajaolewa
Sijawahi Kukutana na Mwanaume aliyeoa Mwanamke wa Mkoani Mbeya akawa na Sauti kwa Mkewe. Hivi ninavyoandika huu Uzi kuna Baba Mmoja Kaoa Mnyakyusa ni Daktari Kaaga mara moja Wagonjwa na amekuja Kukuna Nazi huku Mkewe huyo Mnyakyusa akiwa anafuatilia Matangazo Mubashara kutoka Zanzibar ya Maombolezo ya Mpendwa wetu Hayati Rais Dkt. Magufuli Sebuleni na amejiachia kabisa.
 
Wakuu Habarini

Kuna post zimekuwa zikisambaa mitandaoni zikimuonyesha mmoja wa marubani ambaye ni mtoto wa Mwl Mwakasege, na kila mtu akizumzungumzia lake + kumpongeza kwa ndoto zake.

Huyu ni mmoja wa marubani wawili waliorusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli. Anaitwa Anna Tusajigwe Mwakasege. Ni binti wa pili wa Mwalimu Christopher na mama Diana Mwakasege.

Anna alipata maono ya kuwa rubani akiwa darasa la 3 tu. Baba yake akampeleka uwanja wa ndege angalau kuona ndege "live" badala tu ya kuziona angani tu. Alipofika darasa la 5 baba yake alitembeza uwanja mdogo wa ndege Arusha ambapo alipata nafasi ya kuongea na marubani kuhusu ndoto yake, nao wakampa ushauri masomo ya kusoma ili aweze kuifikia ndoto hiyo.

Alijifunza urubani Afrika kusini, na siku anarusha ndege kwa mara ya kwanza baba yake hakulala usiku huo (hii ni story ya wakati mwingine).

Lakini kwa sasa Anna ni miongoni mwa marubani wa shirika la ndege ATCL. Kabla ya kujiunga na ATCL alifanya kazi mashirika mengine makubwa ya ndwge kama SAA na kupata uzoefu wa kuendesha ndege kubwa kama Boeing 747, Boeing 777 na Airbus A340.

Hongera Anna kwa kuaminiwa kuendesha ndege iliyobeba mwili wa Rais. Umeweka alama kubwa kwa taifa hili, ambayo haitafutika kirahisi. Mara zote tutakapokumbuka kifo cha JPM tutakumbuka kuwa wewe kama Senior First officer na rubani mwenzio (kiongozi) ndio mlipata neema ya kubeba mwili wake.

Najua si kazi rahisi kuendesha ndege ukiwa na majonzi ya kumpoteza Rais wako lakini umeaminiwa na umeweza. Tunawaombea kwa safari ya Zanzibar, Mwanza na Chato. Wewe pamoja na cabin crew yote. Hakika wanawake mnaweza. View attachment 1732239
Wanawake wanakuja kwa kasi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Malezi makini ya wazazi kwa watoto na miongozo sahihi ni nini tosha. Mambo ya familia kuwa na pesa ni secondary. Kuna mabillionnaire ila watoto wao hawana tofauti na chokoraaa na mifano ipo. Hongereni sana mwalimu Christopher Mwajasege na Diana Mwajasege.

Pia majina ya kuwapa watoto muwe nayo makini. Nimegundua majina ya Anna ni miongoni mwa yenye bahati na wapambanaji sana.
Hakika..umakini wa malezi ni muhimu sana
 
Siyo kweli kwamba Anna ameajiriwa na ATCL, isipokuwa ameajiriwa na Wakala wa Ndege za serikali TGFA yenye dhamana ya kusafirisha viongozi kwa anga lkn pia yenye dhamana ya kusimamia mikataba ya ukodishaji ndege kwa ATCL kwa niaba ya Serikali.

ATCL na TGFA nadhani waliingia mikataba kadhaa ikiwa ni pamoja na ushirikiano kwenye suala la manpower hasa aviation engeering na Operations kwa maana ya Pilots na Cabin crew.

Ukiacha kusukuma hiyo Dash8-Q400 (De haviland) ambayo ni kama zile Bombardier, ni senior officer anayesukuma Fokker 50 na Gulf stream yaani Ndege ya Mh. Rais.

Kwa pilots wa kike pia yupo Joanitha Boman ambaye nae anasukuma ngoma kama hizo.

"Wanawake tunaweza"
Hilda Ringo tangu aachane na Fast Jet hajarudi tena kwenye kazi yake?
 
Wanawake huu ni mwaka wenu wa kujimwambafai. Siku za nyuma mlikuwa mnatusumbua na nyimbo zenu eti wanawake tunaweza huku hakuna mifano ya kutuonyesha.

Mbali na huyo Rubani pia Rais wetu wa nchi nae ni Mwanamke, pia wapo Mawaziri na wakuu wa Mikoa na wilaya. Hata kwenye michezo yupo CEO wa timu ya Simba wote hao wanasafisha njia kwa wengine kuwa wakipewa nafasi - wanaweza.
Hakika Chief..nahisi awamu inayokuja watapata Spika Mwanamke pia...mambo yamechachamaa
 
Urubani hauhitaji akili nyingi.
Ukiwa na mambo 3 tu inatosha.
1. Pesa
2. Utimamu wa akili na mwili
3. Lengo.
Hata ukipata form form D tatu ikiwemo angalau moja ya mathematics au physics inatosha. Ukiwa maskini sahau urubani maishani mwako hata upate A masomo yote, labda utapaisha ndege za jeshi tu
Sawa sawa chief..kwa maoni.
 
Naunga mkono hoja.
Napingana na hoja za wanaojivunia sehemu zao za siri kuliko akili za kichwani mwao.
Ndugu kuna Mwanamke nimemtongoza Jana na alichonijibu najua Mwenyewe ila mwishoni akaonyesha Jeuri na Kiburi fulani hivi kwa Kutumia Urais wa sasa wa Mwanamke mwenzao Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan. Alinikera mno tu yaani Kumtongoza Kwangu kumehusiana nini na Urais wa Mama Samia? Wanaume tuwe Makini sana tu.
 
Sijawahi Kukutana na Mwanaume aliyeoa Mwanamke wa Mkoani Mbeya akawa na Sauti kwa Mkewe. Hivi ninavyoandika huu Uzi kuna Baba Mmoja Kaoa Mnyakyusa ni Daktari Kaaga mara moja Wagonjwa na amekuja Kukuna Nazi huku Mkewe huyo Mnyakyusa akiwa anafuatilia Matangazo Mubashara kutoka Zanzibar ya Maombolezo ya Mpendwa wetu Hayati Rais Dkt. Magufuli Sebuleni na amejiachia kabisa.
Hamtaelewana na Bujibuji hawa Dada zake na Mashangazi wakatiwa Msiba ni wanagalagala kweli, km sio Sugu kuwagawa wakapungua, nao wangepewa wakaage.

Lakini kwenye kazi na mapenzi wapo First class nimewaona katika masoko yote ni vinara.
 
Back
Top Bottom