The _Analyst
JF-Expert Member
- May 26, 2017
- 466
- 564
Hakumaanisha kuwa ataropoka hovyo, try to know the context behindKumbuka wakenya wamemchagua tena baada ya kuwaambia raundi hii ATAKUWA kama Magufuli.
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakumaanisha kuwa ataropoka hovyo, try to know the context behindKumbuka wakenya wamemchagua tena baada ya kuwaambia raundi hii ATAKUWA kama Magufuli.
Ok, what is the context behind Mr. Brains? Is it a no nonsense type of leadership or what??Hakumaanisha kuwa ataropoka hovyo, try to know the context behind
Sent using Jamii Forums mobile app
Unahitaji kutahiriwa kwa kucha kama kule kwetu ifanyikavyo. Uhuru kazoea maisha ya ikulu kuku weye. Halipuki. He has got his ancestors archives to learn from. And, he is doing all fine you moron!Siyo kama mjomba wako. Ukoo hauna history ya uongozi zaidi ya kuwa "mzelambeba"! Kuwa makini you hopeless fella! Siyo unaandika tu kama unatafuta siku zako.
Umenena jambo kubwa sana sababu wengi hawaoni ama kukumbuka vile Odinga amenena.Aliulizwa aende kutoa ushahidi juu ya "kashfa" ya Eurobond akasema "siendi na siendi ,wale jamaa ni watu wadogo sana kwangu" Pia akaulizwa na waziri wa uchumi aende kuona vile pesa zimetumika akasema "who does he think he is to ask me to his office"Hawa wakenya wangefanya makosa makubwa sana kama wangemchagua RAILA...
Sent using Jamii Forums mobile app
Watu ni wavivu sana kukumbuka, Uhuru na kundi lake wameanza kucopy ya Magufuli.
Mbona na wewe umeweka full chuki, au mnatoka zizi moja?Hebu acha uongo wewe! Uhuru huwezi kumfananisha na huyo nduli dikteta uchwara. Hana cha kucopy kwenye kudhara katiba, sheria za nchi, Bunge na kuleta hofu kwamba nchi nzima kwa kauli na matendo yake yaliyojaa chuki za kutisha.
Mbona na wewe umeweka full chuki, au mnatoka zizi moja?
Sina chuki naye kama binadamu bali nachukia kauli na matendo yake dhidi ya Watanzania na Tanzania. Alilijua neno la unyenyekevu alipokuwa anaomba kura mara tu baada ya kuingia akaamua kuwa nduli na dikteta uchwara na kufanya Watanzania wengi waishi kwa hofu kubwa kitu ambacho hakikuwapo kabla hajaingia Ikulu.
Udikteta uchwara na unduli kama huu wa kuwadhalilisha Watanzania walioishi kwenye nyumba zao wengine kwa karibu miaka 50 kuwavunjia nyumba zao bila kuwalipa fidia na huku akidharau mahakama ambayo imesimamisha bomoa bomoa hiyo.
Naona unahadaika na mbwembwe za kisiasa za Uhuru huku ukifumbia macho maamuzi yake ambayo mengine ni kandamizi kwa upinzani. Nani alituma watu wake bungeni wabadili sheria ya uteuzi wa jaji mkuu na naibu wake? Umesahau wabunge wake walivyopitisha sheria ya uchaguzi ya kuhesabu kura kwa mkono kama mitambo ikizima, kitu ambacho ndio chanzo cha wizi wa kura, tena wamefanya hivyo bila wapinzani kuwepo bungeni. Na yeye bwana mkubwa akaitia saini haraka haraka na kuifanya kuwa sheria. Wakati Tanzania tunwapa wakimbizi uraia, mwenzake ana wabeba Wasomali juu juu na kuwarudisha makwao. Hapo hujaenda kwenye issue ya ICC na sarakasi zake, hujawauliza waislamu wa Mombasa, wala hujauliza raia waliopoteza maisha pasipo na hatia. Huyo bwana ana mazuri yake lakini sio malaika, in fact yuko mbali sana na kuwa malaika kama utafatilia mwenendo mzima wa rushwa na upotevu wa mali ya uma kwa kipindi cha urais wake.
Sina chuki naye kama binadamu bali nachukia kauli na matendo yake dhidi ya Watanzania na Tanzania. Alilijua neno la unyenyekevu alipokuwa anaomba kura mara tu baada ya kuingia akaamua kuwa nduli na dikteta uchwara na kufanya Watanzania wengi waishi kwa hofu kubwa kitu ambacho hakikuwapo kabla hajaingia Ikulu.
Udikteta uchwara na unduli kama huu wa kuwadhalilisha Watanzania walioishi kwenye nyumba zao wengine kwa karibu miaka 50 kuwavunjia nyumba zao bila kuwalipa fidia na huku akidharau mahakama ambayo imesimamisha bomoa bomoa hiyo.
Mkuu ubinadamu kazi...wananchi kama hao kunyanyasika kiasi hicho sio dalili nzuri katika utawalaUmeona eh! Mkuu. Jamaa alilijua neno unyenyekevu wakati wa kuomba kura, sasa kaingia Ikulu huo unyenyekevu haujui tena ni unyama unyama tu na chuki za kutisha.
Mkuu ubinadamu kazi...wananchi kama hao kunyanyasika kiasi hicho sio dalili nzuri katika utawala
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimehuzunika sana kuwaona katika hali hiyo..Mungu hamtupi mja wake..na waogope mtu anayenyanyua mikono kumshitakia Mungu kwa kudhulumiwaMkuu inashangaza sana kuona hii Serikali imekaa kimya kabisa kuhusu hawa Wazee na Watoto kuvunjiwa nyumba zao na kuwalazimu kulala nje. Watu wameishi pale kwa miaka 45 sasa. Hakuna mtu ambaye asingependa kuona maendeleo lakini maendeleo yaje na haki watu walipwe fidia zao wanazostahili na siyo kudhulumiwa. Walitumia nguvu ya kubwa pesa ya kununua viwanja kujenga mpaka nyumba zikastahili kuitwa nyumba na wao kuishi humu. Sasa wanaachwa wakiwa hawana mbele wala nyuma! Fikiria mvua, fikiria mbu baridi n.k. yaani ni udhalimu wa hali ya juu.
Nimehuzunika sana kuwaona katika hali hiyo..Mungu hamtupi mja wake..na waogope mtu anayenyanyua mikono kumshitakia Mungu kwa kudhulumiwa
Sent using Jamii Forums mobile app
Amen
Uelewa wako ni mdogo. Uhuru anaheshimu katiba yao tofauti na huyu nduli dikteta uchwara. Uhuru kakubali sheria iachwe ifuate mkondo wake wakati Tanzania hata kupinga matokeo mahakamani hairuhusiwi. Uhuru hakamati kamati wapinzani kwa sababu za kipumbavu ambazo hazina kichwa wala miguu huyu kahudhuria mkutano wa jimbo la mbunge mwengine wa chama chake, huyu kazidisha mkutano kwa dakika 7, na yule kasema ukweli kuhusu kukamatwa kwa ndege ughaibuni na pia kutoa hongo kwa Wabunge wake ili wapitishe miswaada uchwara kwa mfano wa kuminya uhuru wa habari nchini.
Husikii Kenya magazeti kufungiwa fungiwa kila kukicha kwa kumkosoa Uhuru au chama chake ukilinganisha na magazeti huru ya Tanzania ambayo sasa hivi hayana uhuru wa kumkosoa mungu mtu kwa madudu yake kwa kuhofia kufungiwa.
Unaona ya wakimbizi lakini huoni ya Watanzania wanaopotea katika mazingira ya kutatanisha yuko wapi Ben Saanane mwezi wa 10 huu sasa hajulikani alipo. Ponda kazungumza juzi tu kuhusu Watanzania waliotekwa na Serikali imeamua kukaa kimya! Tia akili kichwani badala ya kumsifia huyo uchwara anayeiangamiza nchi.