Wewe umelewa Kenya na huyo Uhuru, hivi nini kilimpata Gado alipowachora hao kima Kenyatta, au juzi tuu yaliomkuta Robert Alai. Magazeti ya Tanzania yana tabia ya kuelemea upande mmoja wa kisiasa bila kufuata utaratibu au kanuni za kiundishi. Magazeti ya Kenya yanashindwa kufanya hivyo kwasababu yakiandika vibaya kundi fulani kabila lote la huko watakushambulia.
Sasa kushindwa kuhoji uchaguzi mahakamani na hayo yameletwa na Magufuli? Maana watu wengine mtamlaumu Magufuli hata mkikosa usingizi. Wewe umejaa mapemzi kwa Kenyatta, na unaimani kwamba anaheshimu katiba, nimekuuliza hapo nyuma mbona anapindua pindua sheria kwa mgongo wa bunge la upande mmoja huku wapinzani wakikosa nguvu ya kupinga?
Unauliza kwanini wapinzani wananyimwa haki yao, katika vyama 18, ni vingapi vina nyimwa hiyo haki? Jee huyo aliye hoji ndege, ameshindwa kutumia nafasi yake kama mbunge na kuhoji serikali bungeni kuliko kuhoji barabarani? Halafu unashangaa kwanini katika vyama 18 ni hicho tuu ndio kina andamwa. Si ndio huyo bwana aliyesimama bungeni ni kuvujisha siri zote za hii nchi huku akijuwa yuko bungeni na hakuna watakacho nifanya. Saa nyingine watu wamesoma lakini akili za kiungwana ni bure kabisa. Mnakibilia kusema watu wamehongwa, hiyo ni njia nyepesi mnatumia kujibu hoja za watu waliochoshwa na harakati zisizo zaa matumda.