MNAPANIKI BURE!
Mi sioni sababu inayowafanya mpaniki.... maigizo yapo hakuna anaeibisha.
HOJA HAPA , JE ALICHOIGIZA AMEPOTOSHA AU HAJAPOTOSHA KULINGANA NA KITABU CHA LUKA??
Sasa kama hakupotosha ,,povu la nini?..
Hata Mimi sikatai wakati mdogo katika maisha yangu niliamini kabisa huyo ndo YESU mwenyewe nikijumlisha na maandiko matakatifu toka katika kitabu cha luka,,, Binafsi ilinisaidia kuwa karibu na Mungu.............ile hofu ya Mungu niliyokuwa nayo mapema ilinisaidia kutoshiriki matendo maovu au dhambi hata kama nikifanya ilikuwepo hali kujutia...na unyenyekevu huo Leo naona matunda yake hata baada ya kugundua sio YESU.
Wengi mtakuwa mnamjua ndege tai anapomfundisha kinda wake kuruka. Ni kama anamtesa lakini anakuwa nia njema huo ni mfano mzuri wa maisha ya Mungu na Mwanadamu.
WAKATI mwingine ni njia anazotumia MUNGU katika harakati za kumrudisha mwanadam kwake.....MUNGU anakuanzia mbali anapotaka kukusaidia.......imani yako inapokomaa hapo anakuacha ujitegemee na hapo ndo unagundua Huyo kwenye filamu sio YESU lakini pia unagundua MAKUSUDI ya Mungu kwako.
Sasa hatua ya mwanzo kabisa tunapaswa kuamini kwa sababu kila neno lenye pumzi ya MUNGU lafaa kwa mafundisho ....Hivyo kadri tunavyokua ndivyo MUNGU anavyotuimarisha katika imani zetu.
Sasa kwenye hiyo filamu yamehubiriwa mambo mengi yanayotuasa,,
Umetajwa UPENDO, UCHOYO, UZINZI, ULAFI , CHUKI , TAMAA n.k
lakini bado miujiza mingi imefanyika kuthibitisha nguvu za Mungu.......yote hayo hatujifunzi sisi tunakomaa kwamba aliyeigiza sio Yesu sidhani kama inasaidia.
Wale wahenga zamani mtakumbuka tulikuwa tunaonyeshwa sinema za maigizo kuhusu ugonjwa wa ukimwi...unashuhudia mwanzo mwisho mpaka Mtu anavyokonda na kufa.
Yote yalikuwa ni maigizo lakini yanaleta hisia mpaka unabadili mwenendo ,, ..kama una ile hofu inakusaidia kukuokoa hata kama ni igizo.
Kwaio mi nafikiri tunapaswa kuamini kwanza yaliyomo kwenye hiyo filamu.
Hoja ya aliyeigiza sio Yesu ni nyepesi mno na haisaidii.