Huyu ndiye Muigizaji Brian Deacon, aliyeigiza kama Yesu na anachokifanya kwa sasa katika Maisha

Huyu ndiye Muigizaji Brian Deacon, aliyeigiza kama Yesu na anachokifanya kwa sasa katika Maisha

Sura ya Yesu Ili kuwepo toka karne za mwanzo kabisa za Ukristo.....

Infact huyo muigizaji ametafutwa ili ku-fit kwa sura ambayo ilikuwako karne na karne
Thibitisha ilo kama picha ya YESU ilikuwepo iliifadhiwa wapi ili nikienda Israel nikaifuatilie.
 
Hazisujudiwi ila uwepo wake unakumbusha tu uwepo tu wa kitu cha namna hiyo. Ni kama unavyoweza kuchora picha yako its not real ila ukiiona unajikumbuka. Lakini cha zaidi ni kuna hata wapagani ambao wanaabudu miti na mawe na hawana shida na mtu yoyote. Pa kuanzia kuna dini ambazo ni kitovu cha fujo na ughaidi hizi ndizo zinahitaji kufanyiwa overhaul.
Kabisa...
 
Thibitisha ilo kama picha ya YESU ilikuwepo iliifadhiwa wapi ili nikienda Israel nikaifuatilie.
Wewe! Hiyo movie ya juzi tuu....Makanisa yana picha toka karne na karne...

Picha ya Yesu ya the last supper ya Dan vinci ipo tola mwaka 1515 ...jiulize...

Wewe acha utani bana
 
Na yule aliyetasfsiri kwa kiswahili aliweza sana jamani. Sijui ni nani na yuko wapi
 
MNAPANIKI BURE!

Mi sioni sababu inayowafanya mpaniki.... maigizo yapo hakuna anaeibisha.

HOJA HAPA , JE ALICHOIGIZA AMEPOTOSHA AU HAJAPOTOSHA KULINGANA NA KITABU CHA LUKA??

Sasa kama hakupotosha ,,povu la nini?..

Hata Mimi sikatai wakati mdogo katika maisha yangu niliamini kabisa huyo ndo YESU mwenyewe nikijumlisha na maandiko matakatifu toka katika kitabu cha luka,,, Binafsi ilinisaidia kuwa karibu na Mungu.............ile hofu ya Mungu niliyokuwa nayo mapema ilinisaidia kutoshiriki matendo maovu au dhambi hata kama nikifanya ilikuwepo hali kujutia...na unyenyekevu huo Leo naona matunda yake hata baada ya kugundua sio YESU.

Wengi mtakuwa mnamjua ndege tai anapomfundisha kinda wake kuruka. Ni kama anamtesa lakini anakuwa nia njema huo ni mfano mzuri wa maisha ya Mungu na Mwanadamu.

WAKATI mwingine ni njia anazotumia MUNGU katika harakati za kumrudisha mwanadam kwake.....MUNGU anakuanzia mbali anapotaka kukusaidia.......imani yako inapokomaa hapo anakuacha ujitegemee na hapo ndo unagundua Huyo kwenye filamu sio YESU lakini pia unagundua MAKUSUDI ya Mungu kwako.


Sasa hatua ya mwanzo kabisa tunapaswa kuamini kwa sababu kila neno lenye pumzi ya MUNGU lafaa kwa mafundisho ....Hivyo kadri tunavyokua ndivyo MUNGU anavyotuimarisha katika imani zetu.

Sasa kwenye hiyo filamu yamehubiriwa mambo mengi yanayotuasa,,

Umetajwa UPENDO, UCHOYO, UZINZI, ULAFI , CHUKI , TAMAA n.k

lakini bado miujiza mingi imefanyika kuthibitisha nguvu za Mungu.......yote hayo hatujifunzi sisi tunakomaa kwamba aliyeigiza sio Yesu sidhani kama inasaidia.

Wale wahenga zamani mtakumbuka tulikuwa tunaonyeshwa sinema za maigizo kuhusu ugonjwa wa ukimwi...unashuhudia mwanzo mwisho mpaka Mtu anavyokonda na kufa.
Yote yalikuwa ni maigizo lakini yanaleta hisia mpaka unabadili mwenendo ,, ..kama una ile hofu inakusaidia kukuokoa hata kama ni igizo.

Kwaio mi nafikiri tunapaswa kuamini kwanza yaliyomo kwenye hiyo filamu.

Hoja ya aliyeigiza sio Yesu ni nyepesi mno na haisaidii.
Inasikitisha wasomi kutoa povu kwenye swala lililowazi kabisa. Hiyo ni movie iliyoigizwa kama KItabu cha Luka. Sasa siwaelewi kabisa yaani walitaka Yesu arudi kuja kuigiza?
 
Umetoa Maelezo marefu lakini yenye kufikirisha lakini hoja apa niupotoshwaji mkubwa wa wahubiri asa Wakristo kumtumaini nawakati mwingine kuchukulia picha zake kuziabudu nk. Kwanini hatukuambiwa kuwa yule ni muigizaji aliyesoma kitabu cha Luka? Kwanini tulifichwa ukweli huu asa Mapadri/Wachungaji!
Naumia sana kwakudanganywa.Wakatoriki ni mabingwa wa kukwepa kuhubiri ndo maana waliamua kutimkia kwenye sinema.
Wale wote waliobariki filamu hii nakushindwa kuitolea Maelezo wote niwanafiki na dawa ya wanafiki mnaijua.
Nataka Mapadri/Wachungaji nje mtuombe radhi kwakutulisha matango pori.
Uyu muhuni aliyecheza hii filamu alikaa kimia uku akijua fika kuwa yeye sio YESU.
Namwamini sana Mungu ataendelea kujitukuza na kujifunua ili watu wote wamjue yeye.

Ndugu hoja zako niza kidini sio za Kiroho lazima tuseme ukweli kwamba hakuna mwanadamu anayetambua sura ya YESU zaidi wale waiokuwepo maana ata wachoraji wawakati ule naona hawakufunuliwa ikizingatiwa camera hazikuwepo.
Uyu nimsanii kama kina Wema, Kanumba nk. Kwani uyu kahaba (Wema sepetu) akiigizaa kama mlokole nikweli atakua kaokoka?

Acheni kutetea ujinga nakusudia kufungua Shauri Mahakamani kupinga mikanda hii kuoneshwa mpaka watakapoamua kuwaeleza watazamaji kuwa yule sio YESU bali ni comedian.
Hii inajulikana hata mwanzo wa movie wamesema imeigizwa kama kitabu cha injili ya luka. Sasa wewe ndiyo haueleweki uliyeamini huyo ni Yesu
 
Hiyo ni depiction tu na wala watu hawawezi kuiabudu picha hata siku moja.., anayeabudiwa ni Mungu pekee.., by the way hivi marehemu muddy alikuwa anafananaje kwanza kwa sababu nasikia tu watu wakimswalia sasa utamswalia vipi mtu ambaye hata hufahamu alikuwa akifanana vipi?
Wewe unafahamu yesu alikuwa akifanana vipi?
 
Yesu alizaliwa middle east na middle east hakuna asili ya wazungu, wazungu kwao ni europe...yesu yupo group moja na wayahudi wa asili(sio fake jews km netanyahu) pamoja na waarabu wa palestina, jordan, na lebanon
 
Inasikitisha wasomi kutoa povu kwenye swala lililowazi kabisa. Hiyo ni movie iliyoigizwa kama KItabu cha Luka. Sasa siwaelewi kabisa yaani walitaka Yesu arudi kuja kuigiza?
Ishu siyo movie ishu ni hyo picha ya hyo jamaa mnaitundika majumbani kwenu na kumuita yesu
 
Mkuu ivi unajua maana ya sanamu?
Soma kitabu cha kumbukumbu la Torati kitakusaidia inawezekana unaabudu bila kujua ukibisha nakuwekea ushahidi. Wakatoriki wanaabudu sanamu.
Soma Leviticus 26:1. Msifanye sanamu yoyote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, Jiwe lolote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi bwana Mungu wenu.
 
Ishu siyo movie ishu ni hyo picha ya hyo jamaa mnaitundika majumbani kwenu na kumuita yesu
Mkuu tunapingwa na watu wanaoabudu picha za yule muigizaji wakimuita YESU, pole yao.
 
Kwan keshaacha ushoga au bado
Una uhakika kama shoga?
IMG_20190223_151916.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom