Ila ndugu zangu hebu tuwe wakweli kutoka moyoni. Ni wazi kwamba bado kuna watu wengi ambao wamebandika picha hizi majumbani mwao na katika kundi hilo kuna wale ambao bado wanaamini kuwa huyo aliye kwenye picha ndiye yesu halisi japo kuna kundi jingine tunaoelewa kuwa yule ni muigizaji tu na si yesu.
Lakini pia tujiulize ni kwa kiasi gani sura ile ya yesu (katika igizo) ilivyotuathiri akili zetu wengi wetu kiasi kwamba unapokuwa katika maombi binafsi au na wengine nyumbani kwako, kanisani kwako au sehemu yoyote ile, picha ya Yesu inayokuwa inakuijia akilini wakati wa maombi hayo huwa ni ya huyo huyo muigizaji mzungu mwenye nywele ndefu na siyo mtu mweusi mwenye nywele fupi au mtu mwingine tofauti na huyo mzungu.
Kuna wakati unaweza kuwa kanisani na katika hubiri lake mhubiri pale mbele akasema "wapendwa ndugu zangu hebu fikiria jinsi yetu alivyoteswa msalabani kwa ajili yetu binadamu....hebu PIGA PICHA AKILINI MWAKO yesu anavyocharazwa viboko, kudhihakiwa na kusurubiwa pale msalabani......". Sasa hapo mtu unajikuta unajenga akilini mwako taswira ya yule yule muigizaji Brian Deacon akicharazwa viboko, kudhihakiwa na kutundikwa msalabani!
Labda wenzangu mnisaidie kwa kunielewesha mnapokuwa katika maombi binafsi au na watu wengine unapojenga picha ya yesu kichwani mwako, akikunyooshea mkono wake au akisurubiwa kwa ajili yako picha inayokuja akilini mwako siyo hii ya huyu mzungu mwenye nywele ndefu aliye katika movie au kwenye vitabu vingi vya neno la Mungu kwa wakristo?