Huyu ndiye Mwigulu Nchemba

Mkapa na Mwinyi walikuwa Namibia last week. Sasa kusema jana wameenda huko ni jinsi gani inaonyesha kuwa data za kuungaunga na kuhisi. Zinatia shaka.
 
hivi mtu na akili zake anaweza vipi kwenda kujisimamaisha sehemu ili apigwe picha na mtu fulani na kuitumia picha hiyo kutangaza uchu wake?

Halafu eti ndio anautaka urais kwa mbinu za kizee hivyo. Kisha ni nani aliyemwambia hao marais wa hizo nchi alizokutana nazo ndio wapiga kura wake? Hivi hawa wataka urais wa ccm wanadhani bado watu ni mafala kwa kiwango kile ama wanadhani kwakuwa watalitumia jeshi na tume ya uchaguzi isiyojitambua ndio watapata nchi watakavyo?
 
Kama ni hivi sasa kuna hatari ya siku moja kuamka na kukuta tuna raisi aliyetoka Mirembe
 
Hili li nchi hili kila mtu akiamka anajitangazia urais enzi za mwalimu hata wajumbe wa nyumba kumi walikuwa wanatazamwa kwa jicho la tatu... rudi tanganyika..
 
Mwaka huu hata fisi watapiga kura
 

Attachments

  • 1427532300818.jpg
    40.6 KB · Views: 159
" Haiwezekani katika taifa hilohilo shirika la umma likavuna raailimali ya umma na kuwa na fedha za ziada hata kukosa wazitumie wapi na kutumia kwa anasa wakati huohuo katika Taifa hilohilo akina mama wajawazito wakawa wana lala wawili kwenye kitanda na wengine kulala chini, hakuna dawa au watoto kukaa chini. Tutazichukua fedha hizo tuwapatie huduma masikini. Mwigulu Nchemba
 
NUKUU NZITO YA LEO KUTOKA DODOMA BUNGENI " Haiwezekani katika taifa hilohilo shirika la umma likavuna rasilimali ya umma na kuwa na fedha za ziada hata kukosa wazitumie wapi na kutumia kwa anasa wakati huohuo katika Taifa hilohilo akina mama wajawazito wakawa wana lala wawili kwenye kitanda na wengine kulala chini, hakuna dawa au watoto kukaa chini mashuleni.Tutazichukua fedha hizo zisaidie Masikini. Mwigulu Nchemba
 

Ukweli unanykia kwa mbaaaaali
 
Wakikabwa majimboni... Wanakimbilia Urais.

Mwigulu hali mbaya Iramba.
 
Binafsi nianze kumpongeza DKT Mwigulu Nchemba kwa kazi yake kama mwanasiasa na gwiji wa mbinu za ushindi ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) Kwanini mwigulu Nchemba na VIjana wengine ndani ya CCM ni mmoja wa mtu wa mbinu hatari za ushindi tangu akiwa shule .kwa mwenye kumbukumbu nzuri huyu ndiye aliye kuwa master mind uchaguzi mdogo jimbo la Igunga hilo halina ubishi ,kwani ushindi wa DKT.DALALI ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na mbinu za mtalaam huyu wa uchumi. kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015 kijana huyu alikuwa mwiba mkali saana kwa upinzani hili halina ubishi.

Hata hivyo jimboni kwake huwezi kutaja Iramba magharibi bila kumtaja mwigulu .anayedhani mimi mwongo asubiri huyu prof.uchwara Mkumbo kwani kama atajitokeza kumpinga mwigulu kuna uwezekano mkubwa kupoteza nafasi ya ukatibu mkuu wizara ya maji na kurudi kufundisha kama fani yake ilivyo.

MWIGULU NI NANI SUBIRI MAKALA ZIJAZO CCM OYEEEE MAGUFULI OYEEEEE
By mnkondya
0628227033
 
Sisi wanaccm tulishamkataa mwigulu Kwenye Jimbo letu la IRAMBA mwaka huu tunahitaji mabadiliko na Kura zetu zote zitaenda Kwa kitila mkumbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…