Huyu ndiye Mwigulu Nchemba

Huyu ndiye Mwigulu Nchemba

Siasa za ccm ni rahisi sana ! Ukitaka ukumbukwe kwenye uwaziri we TISHIA kugombea urais tu !
 
mmepewa pesa ili mumpigie debe huyo mpuuzi mwenzenu nn? eti nchema nchemba haaaaa! hafai kabisa na kama amewahonga ili mumsaidie mwambieni ukweli kwamba hakubaliki hata kidogo

Kama humkubali ni wewe ila sisi Watanzania tuliowengi masikini na wanyonge wa nchi hii mtetezi wetu sisi ni Mwigulu na ndiye tunayemtaka awe Rais wetu 2015
 

Baada ya kumalizika kwa Kamati kuu ya chama iliyoketi kwa siku mbili hapa Dodoma,Kamati kuu ilimpongeza mh Mwigulu Nchemba kwa jitihada zake za dhati katika kupambana na kuisaidia serikali hasa katika Kukusanya kodi toka bilion300 hadi bilion 800 kwa mwezi pia kwa kutatua kero nyingi za walimu Nchini.

Nikimnukuu kuhusu yeye kuwa rais anayependekezwa mh Mwigulu anasema
“CHAMA chetu ni chama cha utaratibu na mimi ndiye msimamizi mkuu ndani ya chama, kundi langu ni CCM, wana CCM wana matumaini makubwa na mimi ya kuwavusha katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu”.

Mwigulu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba.

Katika kipindi kifupi tangu kuteuliwa kwake katika nafasi ya Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu ameonesha ni kwa kiasi gani alivyo na uwezo mkubwa katika uongozi na kusimamia ustawi wa nchi na watu wake.

Tumeweza kushuhudia hofu ya Mwigulu pale aliposimama bungeni katika Bunge Maalumu la Katiba kutoa tahadhari kuhusiana na fedha za walipa kodi.
Akiwa miongoni mwa viongozi tulionao nchini, aliweza kupatwa hofu ya fedha za walipa kodi kutumika ndivyo sivyo.

Hili si jambo la kupuuzia hata kidogo, bali ni jambo la kujivunia kuwa na kiongozi mwenye uthubutu katika kipindi hiki ambacho Watanzania wanasumbuliwa na misigino ya kisiasa.

Katika mchango wake alionesha hofu yake ya kuendelea na majadiliano kwa siku 84 na hatimaye kushindwa kupata theluthi mbili za Tanzania Bara na theluthi mbili za Tanzania Visiwani ili kupitisha Rasimu tayari kwa kupigiwa kura ya maoni na Watanzania.
Mwigulu alifikia hatua ya kumtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba afanye hesabu na kujiridhisha juu ya kupatikana kwa takwa hilo la Kikatiba.

Hii ilikuwa ni hofu kuu. Ni hofu iliyotoka rohoni, isiyokuwa na chembe ya shaka. Aliweza kuona dalili za kulazimisha visivyolazimishwa.

Hofu inayolenga kuponya fedha za walipakodi wa nchi hii zinazoweza kutafunwa kwa siku 84 bila ya kupelekewa Rasimu ya Katiba kuipigia kura.

Ni hofu ya wengi, wachambuzi na wachokonozi wa kisiasa waliiona kauli ya Mwigulu kama kuanza kushtuka kwa CCM na viongozi wake.

Mwenyekiti wa Bunge hilo hakuweza kuiona hofu ya Mwigulu, hakuufanyia kazi ushauri wa mjumbe wake, lakini naamini ya kuwa nafsi ya Mwigulu ilikuwa huru baada ya kutoa dukuduku lake.

Kutokana na wadhifa wake ndani ya chama na Serikali Mwigulu amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anasimamia fedha za walipa kodi wa nchi hii zisitumike vibaya bali kwa maslahi ya wote.

Tumeshuhudia ni kwa kiasi gani amesimamia fedha zilizokuwa zikiibwa kupitia mishahara hewa na kutoa angalizo kuhusiana na fedha hizo.

Nchi inao viongozi wengi, lakini viongozi aina ya Mwigulu ni wa kuhesabu kama si kutafuta. Tunalo jukumu la pamoja kuhakikisha viongozi wetu wanatekeleza majukumu yao kama afanyavyo huyu ambaye ameonesha njia.

Tunalo jukumu kumhakikishia ya kuwa tunamuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake na katika kulitumikia taifa letu na sio kumbeza kama ambavyo wengine wanafanya.
Pamoja na Mwigulu kuwa Naibu Katibu Mkuu CCM amekuwa akitimiza majukumu yake ya Naibu Waziri wa Fedha bila ubaguzi jambo ambalo limekuwa adimu katika kipindi hili.

Tanzania yangu ya sasa inahitaji viongozi walio na utayari wa kuwatumikia wananchi wake, walio na uchungu na mali na raslimali za nchi na si vinginevyo.

“Mimi sio matokeo ya jitihada za kundi lolote kufika hapa nilipo, niligombea ubunge nikiwa sijulikani na kundi lolote na wala sikutengenezwa na kundi lolote. Hata nilipokwenda kugombea sikuwa hata na baiskeli, pikipiki wala gari. Mimi sina kundi na wala sitokani na makundi yanayokinzana, sina kundi lolote ndani ya chama wala siegemei kundi lolote.”

“Lililo jema ni kutokuwa na chuki wala ugomvi na wanaCCM wenzangu. Sina sababu na wala sioni faida ya kuingia kwenye makundi katika ngazi hii na muda huu.” anasema.

Hii ni miongoni mwa kauli zilizowahi kutolewa na Mwigulu, kauli inayopashwa kutolewa na kiongozi anayesimamia kile anachokiamini katika utekelezaji wa majukumu yake bila kuegemea upande wowote ule.

Tanzania ya kizazi hiki inahitaji viongozi wenye maono, wenye uthubutu wa kusema hapana sasa imetosha, viongozi walio na uchungu na ndugu zao kutokana na maisha wanayoyaishi.
Mwigulu Nchemba ni miongoni mwa viongozi walioonesha msimamo wao katika kutetea kile wanachoamini kuwa ni kwa ajili ya Watanzania wote na kwa faida ya wote.

Ni vyema tukasimama na kumuunga mkono yeye pamoja na viongozi watakao kuwa tayari kutimiza wajibu wao kama afanyavyo Mwigulu.

Tunalo jukumu la kusimama pamoja na Mwigulu kuhakikisha ya kuwa yale anayoyabainisha anayatetea bila hofu kwa faida yetu sote.

CHANZO: DIRA YA MTANZANIA
Kwenye hii rasimu ya mafisadi kura yake ilikuwa NDIYO au HAPANA?Wake me up when you come up with the answer of NO!
 
Siasa za ccm ni rahisi sana ! Ukitaka ukumbukwe kwenye uwaziri we TISHIA kugombea urais tu !

Sikulau kwani huo ndio mwisho wa uwezo wako wa kufikiri. Watu wanaongea mambo muhimu kwa mustakabari wa taifa wewe unaleta uzwazwa shame on you.
 
Huyu jamaa mi namkubali sana he is focused, realistic and seems to b patriotic na mengine mengi... lakini si kila anayefanya vizuri basi awe rais chamsingi next muhula apewe uwaziri kamili wa fedha ili tumuassess vizuri.
Tanzania ina tatizo kubwa la kimfumo I.e everything is centralised nothing is independent na mbaya zaidi mfumo wote upo corrupted.
 
Acha tu awe rais,
Hakuna jina lililokuwa safi zaidi ya hilo.
 
MPANGO WA MUNGUE Waambie na wakwepa kodi wenzako mtafute urais maana Mwigulu hataki mzaha na masuala nyeti ya kitaifa
 
Last edited by a moderator:
Hata kama atakuwa ni kiongozi mzuri kwenye usimamizi wa fedha bado ana tatizo moja kubwa sana tena sana ana jazba na kiburi na pia ni mzuri wa kuratibu mambo ya kiuharamia zaidi kuliko uzuri wake wa kiutendaji,Matukio mengi ya mauaji ya raia walio kinyume na ccm yaliwahi kutokea na yeye kutuhumiwa kuhusika kwa namna fulani kwa hiyo mtu kama huyu akiwa rais watakufa raia wengi sana wenda hata ww unaempigia upatu hapa mkiwa tofauti baadae atakupoteza ni vizuri watz tungekuwa tunaona mbali na kutafuta viongozi thabiti kwa faida yetu na ya kizazi kijacho
 
Acha uongo ametatuaje kero za walimu?umesahau siku ya walimu mpaka policcm wakavunja mabango yao!
 

Attachments

  • 1413637669886.jpg
    1413637669886.jpg
    98.2 KB · Views: 126
Back
Top Bottom