Huyu ndiye Mwigulu Nchemba

Huyu ndiye Mwigulu Nchemba

Katika hali ya kuonesha kuwa Mwigulu anazidi kupenya kwenye Vichwa vya watanzania wengi,Wanasiasa,Wanafunzi,Wakulima na Wafugaji.
Zitto Kabwe ambaye anatajwa kuwa Mwanasiasa bora Nchini Tanzania katika Uga wa Kusimamia anachokisema na kukijengea hoja,Zitto Kabwe wakati huu taifa likielekea Uchaguzi Mkuu 2015 ameamua kuweka bayana kuwa Mwigulu ni Mgombea Urais 2015 anayemkubali zaidi.
Kupitia Ukurasa wake wa Facebook mbali na maongezi marefu zaidi waliyoyafanya jana kwenye kikao kisichorasimi yeye na wanasiasa wengine akaamua kuutangazia Umma kuwa mwigulu ndiye Mgombea Urais.

Zito analipa fadhila kwa nchemba kwa kumsaidia kwenye mkakati wake wa usaliti ndani ya chama hatimae kupewa bilioni 3.6. Tunakumbuka email ya nchemba na nchimbi wakijadili jinsi ya kumrubuni zito na kupongezana jinsi walivyomuua mvungi na kusema sasa tutapata katiba tunayoitaka. Watz hatudanganyiki tena.
 
Huyu jamaa kingine kinachommaliza ni kulishwa maneno.
 
jamiiforums inageuzwa jukwaa la kijadir upuuzi na wapuuzi

Ilishakua hivyo zamani sana kiongozi. Humu ni udaku tu, mapenzi na kutafuta wachumba. Lakini serious matters hamna!!

Naona Zitto ndio kapewa jukumu la kututangazia mpigania urahisi 2015.
 
Kazi mnayo...Urais siyo mchezaji wa akiba..Rais anatakiwa kuwa among the first eleven...kafanya nini Mwigulu so far? Maneno yake hayatoshi na kumpa sifa ya kuwa Rais.

nilijisikia vyema sana katika moja ya midahalo wakati wa BMK pale Nkrumah Hall, huyu Bwana Mwigulu alipokiri kuwa, bila maridhiano katiba mpya haiwezi kupatikana..na nikadhani angeendelea hivyo na msimamo wake hadi bungeni. Kufika kule...akendelea kubaki Bungeni na kura ya ndio aliipigia ile katiba ya CCM. Uzalendo wake kwa nchi hiii upo wapi? Mnaompigia chapuo mjipime kama anatosha kwa hii nafasi.

Ili kuleta maendeleo endelevu Tanzania inahitaji Rais mzalendo...
Raisi atakayesema
kuanzia sasa atakayeua Tembo anafikishwa kwenye sheria na kufungwa...Tena mnawajua, aanze na waliopo
Kuanzia sasa mwizi wa mali ya umma hafai kufanya kazi ya Umma..akalime shamba lake kule Kibaigwa
kuanzia sasa, wananchi wahoji viongozi wao
Kuanzia sasa nyumba zote za Serikali zilizochukuliwa kiwizi wizi Oysterbay na maeneo mengine nchini zirejeshwe Serikalini
Kuanzia sasa, walimu wapewe stahiki zao zote
kuanzia sasa mikataba yote ya rasilimali ya nchi hii iwe wazi
Kuanzia sasa huduma zote za msingi katika zahanati zetu zipatikane bure na zitosheleze
kuanzia sasa kiongozi wa nchi hakuna kusafiri kama Vasco da Gama na msusuru wa wapiga debe huku wakifuja pesa za walipakodi
Kuanzia sasa matibabu yote ya vongozi yapatikane Tanzania...

Kuanzia sasa hakuna kufanya biashara Ikulu...no NGO no nothing...

Nani katika hao mlionao huko Chama chenu tawala ana sifa hizo?
 
hiyo statement ni tata sana

zitto anautaka urais na mwigilu anautaka urais
 
PAC nayo imejiingiza kwenye makundi ya wasaka urais?!
 
Jamaa kashapoteza uelekeo kabisa!! Siasa za kibongo si za kuingia kichwakichwa.
 
hiyo statement ni tata sana

zitto anautaka urais na mwigilu anautaka urais
Hapana, anatumikia mmoja wa wasaka urais. Ujinga uliopitiliza kuihusisha kamati ya bunge na vita za njaa zao.
 
"TUNAHITAJI RECORD YAKE YA MIAKA 15 ILIYOPITA YA UTENDAJI WAKE" / "15~20"years on duty ktk senia position/unless otherwise asije akaingia madarakani mtu ambaye akawa ni BALAA KUBWA NA MAANGAMIZI KWA TAIFA LETU
 
Katika hali ya kuonesha kuwa Mwigulu anazidi kupenya kwenye Vichwa vya watanzania wengi,Wanasiasa,Wanafunzi,Wakulima na Wafugaji.
Zitto Kabwe ambaye anatajwa kuwa Mwanasiasa bora Nchini Tanzania katika Uga wa Kusimamia anachokisema na kukijengea hoja,Zitto Kabwe wakati huu taifa likielekea Uchaguzi Mkuu 2015 ameamua kuweka bayana kuwa Mwigulu ni Mgombea Urais 2015 anayemkubali zaidi.
Kupitia Ukurasa wake wa Facebook mbali na maongezi marefu zaidi waliyoyafanya jana kwenye kikao kisichorasimi yeye na wanasiasa wengine akaamua kuutangazia Umma kuwa mwigulu ndiye Mgombea Urais.

Combination ya mwigulu (rais) na zito (pm) kama kenyata na ruto vile mchakamchak wake usipime
 
Hata bila ZZK kusema hivyo, hilo linajulikana kuwa Mwigulu ni mgombea urais, kwani alishatangaza nia yeye mwenyewe. Kuwa mgombea urais ni tofauti na kuwa rais, kama mnavyojua hata Dovutwa alikuwa mgombea urais!
 
Tunaukumbuka vizuri uhusiano wa mwigulu na Zitto katika kucheza lile movie la UGAIDI wa Lwakatare,naona haya ndio makubaliano yao! Pia tunakumbuka ile email ya Mwigulu kwenda kwa Lukuvi ikimjulisha namna watakavyoshirikiana na Zitto kuhujumu katiba ya wananchi na kumuua Dr Mvungi
 
Back
Top Bottom