Huyu ndiye Mwigulu Nchemba

Huyu ndiye Mwigulu Nchemba

Amefanya nini cha maana? Hali ya watanzania imeimarika baada ya yeye kuwa naibu waziri? Hospitali dawa na vifaa tiba vimeanza kupatikana baada ya yeye kuwa naibu waziri? Ufisadi na wizi wa fedha na ukwepaji kodi umepungua baada ya yeye kuwa naibu waziri. kifupi, nini kimeboreka katika maisha ya watanzania kutokana na nafasi yake hadi aonekane yeye ni wa tofauti?

I hate politicians. Nahisi nchi ingekuwa na neema kama kungekuwa na uwezekano wa kutokuwa na wanasiasa.

View attachment 201216
 
Njaa imefanya watu wakamwasi Mungu wao, wengine wakabadili dini, wengine wakaolewa na wengine hata wakazikana asili zao. Ila hii njaa ya mleta uzi ni ya pekee. Kama unampenda saana hamia kwake. Wengi tutafanya maamuzi baada ya kuapima kikamilifu. Hizi hasara zimetosha.
 
==> I am calling ZZT to confirm this...!!!! really..!? I don't mean i don't appreciate Mwigulu, i do...i knew him long ago...since back A - Level at Mazengo High School, Dodoma, now is ST. JOHN'S UNIVERSITY...of which he was a better performer...open minded and successful candidate to UDSM...

..But, kikubwa Mwigulu has to keep in his mind..yuko ktk SYSTEM ambayo rushwa imeota mzizi...so will he go against his own system..!? Can he..!?

I hv dought kama ataweza kukishikisha adabu CCM ambayo RUSHWA NDIO NJIAA PEKEE YA MAISHA NA KUPATA UONGOZI...
 
Kama amependekezwa na Mafisadi wala sishangai lakini kwa watanzania wenye akili zetu hata kuchunga panya hafai. Muuaji mkubwa huyu hata shetani amemkataa..Nani anataka Rais muongo, mnafiki, muuaji, mla rushwa, mpenda visasi na mkabila
 
==> I am calling ZZT to confirm this...!!!! really..!? I don't mean i don't appreciate Mwigulu, i do...i knew him long ago...since back A - Level at Mazengo High School, Dodoma, now is ST. JOHN'S UNIVERSITY...of which he was a better performer...open minded and successful candidate to UDSM...

..But, kikubwa Mwigulu has to keep in his mind..yuko ktk SYSTEM ambayo rushwa imeota mzizi...so will he go against his own system..!? Can he..!?

I hv dought kama ataweza kukishikisha adabu CCM ambayo RUSHWA NDIO NJIAA PEKEE YA MAISHA NA KUPATA UONGOZI...

View attachment 201229
What's more you want than this?
 
Kama amependekezwa na Mafisadi wala sishangai lakini kwa watanzania wenye akili zetu hata kuchunga panya hafai. Muuaji mkubwa huyu hata shetani amemkataa..Nani anataka Rais muongo, mnafiki, muuaji, mla rushwa, mpenda visasi na mkabila

View attachment 201230
Tafuta muda wako ujifunze kutoka kwa Mwigulu
 
Njaa imefanya watu wakamwasi Mungu wao, wengine wakabadili dini, wengine wakaolewa na wengine hata wakazikana asili zao. Ila hii njaa ya mleta uzi ni ya pekee. Kama unampenda saana hamia kwake. Wengi tutafanya maamuzi baada ya kuapima kikamilifu. Hizi hasara zimetosha.

View attachment 201233
Sasa kwa mtazamo kama huu unadhani nchi yetu itashindwa kuwa ya kipato cha kati ?
 
Usukani ashikilie Magufuli, Pm Mwakyembe au Muhongo, Fedha Mwigulu......ni kama naiona Tanzania mpya.

Mwigulu ni taswira mpya yenye matumaini mapya kwa taifa letu
 
Njaa imefanya watu wakamwasi Mungu wao, wengine wakabadili dini, wengine wakaolewa na wengine hata wakazikana asili zao. Ila hii njaa ya mleta uzi ni ya pekee. Kama unampenda saana hamia kwake. Wengi tutafanya maamuzi baada ya kuapima kikamilifu. Hizi hasara zimetosha.

Katika hali ya kuonesha kuwa Mwigulu anazidi kupenya kwenye Vichwa vya watanzania wengi,Wanasiasa,Wanafunzi,Wakulima na Wafugaji.

Zitto Kabwe ambaye anatajwa kuwa Mwanasiasa bora Nchini Tanzania katika Uga wa Kusimamia anachokisema na kukijengea hoja,Zitto Kabwe wakati huu taifa likielekea Uchaguzi Mkuu 2015 ameamua kuweka bayana kuwa Mwigulu ni Mgombea Urais 2015 anayemkubali zaidi.

Kupitia Ukurasa wake wa Facebook mbali na maongezi marefu zaidi waliyoyafanya jana kwenye kikao kisichorasimi yeye na wanasiasa wengine akaamua kuutangazia Umma kuwa mwigulu ndiye Mgombea Urais 2015
 
Huyu jamaa anakuja vizuri ila wanao mzungu na chama chake ndio shida!

Tanganyika yetu
 
Labda raisi wa mkalama huko singida kwake c kutuongoza watanzania zaid ya million 50
 
Naona jamaa kakomaa kweli. Makuadi wa kutengeneza mafisadi. Humjui kabisaaa. Ukijamjua utajilaumu kusema haya unayosema.
 
Huwezi kumuwekea dhamana kichaa utafungwa shirikisha ubongo kabla hujapost hizo pumba uyo chiz nan ampe dhamana ya urais labda mirembe wenzake
 
View attachment 201230
Tafuta muda wako ujifunze kutoka kwa Mwigulu

Siwezi kujifunza chochote toka kwa MUUAJI wa jamaa zangu,mlarushwa mkubwa,mtu mwenye visasi.Nimekwambia atoke hadharani atuambie yote ili tuweze kumtathmin kama bado anafaa kuanza kuchunga hata panya.

Kwa sasa hata PANYA hawezi kuchunga.Kama amekupa pesa umsafishe mwambie kama ameshindwa kujisafisha kwenye MTO hawezi kujisafisha kwenye DIMBWI!
 
MWIGULU NCHEMBA RAFIKI WA WALALA HOI, KIPENZI CHA VIJANA , ALAMA YA UZALENDO, UJASIRI NA UTHUBUTU

HISTORIA YAKE

Kwa Mtanzania yoyote anaefuatilia siasa hili jina sio geni sana masikioni mwao, wapo waliolisikia jina hili kwa namna yoyote ile mbaya au nzuri leo nataka nimzungumzie Mwigulu Lameck Nchemba Mbunge wa Iramba Magharibi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM na Naibu Waziri wa fedha kwa namna ninavyomjua na harakati zake za kisiasa ninavyozitazama.
Alizaliwa tarehe 7 January 1975 katika kijiji cha Makunda Wilaya ya Iramba katika familia ya kimaskini kabisa ambayo baba alijishughulisha na ufugaji, huku mama akijushughulisha na kilimo. Maisha ya utotoni ya Mwigulu Nchemba yamegubikwa na tabu nyingi na mara nyingi amekuwa akikiri aliishi kwa uji kutwa nzima na kukutana na mlo mmoja tu jioni hasa kutokana na muda mwingi kutumia kuchunga ng’ombe.

Maisha haya ya kushinda na wanyama porini mda mwingi na kukabiliana na wanyama wa hatari, hali ya hewa mbovu kama mvua kali au jua kali yalimjenga katika ujasiri ambao hadi leo hii anao nitauelezea badae Katika makala hii. Kama ilivyo ada familia za kifugaji kulea watoto katika misingi ya heshima, Upendo adabu na utu, Mwigulu Nchemba alikuzwa hivyo kuheshimu watu, na kuthamini utu wa Mtu na kuwa na upendo kwa binadamu wenzake.

Kutokana na familia nyingi za kifugaji kukosa mwamko wa elimu alichelewa kuanza masomo na kujikuta akianza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka 12 mnamo mwaka 1987, na kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 1993 katika shule ya msingi Makunda.
Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi alijiunga na elimu ya sekondali Mazengo 1994 - 1997 kisha kujiunga na elimu ya A-level kidato cha tano na cha sita shule ya vipaji maalumu Ilboru sekondari.
Katika maisha yake ya sekondari ndio nyota yake ya uongozi ilipoanza kujionyesha wazi wazi hasa baada ya kuchaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa wanafunzi Mizengo Secondary na kiongozi wa wanafunzi Ilboru sekondari.

Alipata ufaulu mzuri na kujiunga Chuo Kikuu cha Dar es salamu UDSM mwaka 2001 - 2014. Katika maisha ya chuo hakujishughulisha na siasa za chuo kabisa waliosoma nae wanasema alikuwa mpole kupindukia, ambaye alikuwa na marafiki wachache sana wala hakufahamika. Jambo lililokuja kumfanya kuwa maarufu ni pale alipofaulu kwa kiwango cha juu na kuwaongozea wanafunzi wenzake wa kitivo cha uchumi. Hapa ndipo alipoanza kufahamika. Nilipopata bahati ya kumuuliza kwa nini hakupenda kufanya siasa chuo kikuu alinijibu kwa kifupi “ Kila jambo na wakati wake, niliona ninasoma kozi ngumu ya uchumi, mbele yangu niliona nina wajibu mkubwa wa kutumia elimu hii kulikomboa taifa langu kiuchumi hivyo sikuona haja ya kujihusisha na siasa za kitoto nikiwa chuo wakati wangu ulikuwa bado.”
Baada ya kumaliza masomo Chuo Kikuu Dar es salamu na kupata ufaulu mzuri alichukuliwa moja kwa moja na Bank kuu ya Tanzania inayotuhumiwa kulundika watoto wa wakubwa lakini yeye alikwenda kwa sifa tu. Hakumjua mtu yoyote na hapa ndipo Bahati yake na muujiza wake wa kwanza ulipoanza kujionyesha. Na kudhibitisha nyota yake ni mshale akilenga hakosi.


SAFARI YA SIASA

Akiwa huko bank kuu ndoto yake ya siasa haikufa aliona namna pekee ya kulikomboa Taifa hili ni kuingia katika vyombo vya maamuzi ndipo alipoamua rasmi kutangaza nia yake ya kugombea jimbo la Iramba mwaka 2010. Haikuwa kazi rahisi kuifikia safari hiyo ilimlazimu kugombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Vijana Mkoa wa Singida akashinda, hivyo kuanza kushiriki rasmi siasa za UVCCM mwaka 2008. Kisha mwaka 2010 kuingia rasmi kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge. Ambapo alimshinda Mhesimiwa Juma kilimbah kwenye kinyang’anyiro cha kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi na kutangazwa rasmi kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi jimbo la Iramba magharibi.
Tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi wanachi wa Iramba wanajivunia kupiga ndege wawili kwa jiwe moja, kwa mana walichagua mbunge ambaye badae akawa na nafasi zaidi ya moja Maana kasi Mbunge huyo kuaminiwa ndani ya Chama na Serikali imekuwa ikikuwa kwa kasi ya ajabu. Mara tu baada ya kuchaguliwa 2010 kuwa Mbunge wa Iramba mwaka unaofuata 2011 aliteuliwa kuwa Katibu Uchumi na fedha Taifa wa Chama cha Mapinduzi, mwaka 2012 akiwa mwanasiasa mchanga alishinda kwa kishindo kura za NEC katika Mkutano Mkuu wa Taifa. Chombo kikubwa kabisa cha maamuzi cha CCM kwa kushika nafasi ya pili na kuwashinda wanasiasa wakongwe kama Wiliamu Lukuvi, Martini Shigera, Deo Matayo, Fenela Mkangala na wengine wengi ambao wapo kwenye siasa kwa mda mrefu.

Lakini nini siri ya ushindi wa Mwigulu Nchemba kwa wana CCM kumwamini na kumlundikia kura nyingi katika muda mfupi wa utumishi wake, ni ukweli usiofichika Mwigulu Nchemba amekuwa akiyatekeleza Matakwa ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Chama na ndani ya Uma kwa ufasaha, huku akidhibiti nguvu za vyama vya wapinzani hadharani kwa hoja na kwa mikakati yakinifu. Ikumbukwe wakati akiteuliwa kuwa Katibu wa uchumi na fedha ni mwaka 2011 ni wakati ambao Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kilikuwa kimepata umaarufu mkubwa huku kikiimarika siku hadi siku hali ambayo ilikuwa ikiwatia hofu wanachama wengi wa CCM.

Ni katika wakati huo alipoamua kulitekeleza jukumu lake la nafasi ya kushughulika na kubuni miradi ya Chama kama nafasi yake ya uchumi na fedha ilivyomtaka na kuingilia kazi ya uenezi iliyokuwa inashikiliwa na Nnape Nnaye na nafasi ya Naibu Katibu Mkuu kwa kufanya harakati nyingi za siasa, ikiwa ni kutumia uwanja wa bunge kujibu mara zote hoja mbalimbali zilizoibuliwa na upinzani. Kwenda hadharani kufanya mikutano ya hadhara kujibu mapigo dhidi ya upinzani na kufanya propaganda kali dhidi ya upinzani. Hali hii ya kuingilia shughuli za Uenezi na Katibu Mkuu alimfanya aingie katika mkwaruzano na Nnape Nnauye ambaye aliona kama “anaingiliwa katika majuku yake ambayo alikuwa hayatimizi” ni katika wakati huu ambapo alikaliliwa na baadhi ya watu wake wa karibu akisema hawezi kubuni miradi ya uchumi katika Chama ambacho kipo hatihati kutolewa madarakani miradi hiyo haikuwa na maana hivyo lazima ashughulike na kudhoofisha upinzani.
Ni katika wakati huo tuliposhuhudia wanachama wengi kutoka upinzani wakirudi CCM ikiwa ni pamoja na kuvurugika kwa Umoja wa Vijana Chadema BAVICHA Kwa Makamu Mwenyekiti wake Juliana shonza, Pomoja na Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Mtela Mwampamba kunyakuliwa na Mwigulu Nchemba na kurudi CCM. NI katika wakati huo ambapo madiwani mbalimbali kutoka Chadema walijiuzulu na kurudi CCM.

Ni katika wakati huo alipobuni kuvaa skafu ya bendera ya Taifa shingoni ambapo hakuna sehemu yoyote alipoicha kuutambulisha uzalendo wake hali hiyo ya kujibu mapigo ya wapinzani mara kwa mara huku akiwachukulia wanachama wake ilimwingiza katika chuki kubwa na wapinzani huku wakipitisha azimio la kutomsalimia popote bungeni, kumzushia yeye ni gaidi hasa alipofuga ndefu na kuwa na mwonekano wa mwanaharakati che Guevara kwa lengo lake, wao wakageuza anamwonekano wa savimbi. Hali iliyosababisha akate ndevu hizo.
Kutokana na uchapa kazi mkubwa na uliotukuka wa Mwigulu Nchemba wa kuamsha ari mpya na kufufua uhai wa Chama uliokuwa unaenda kufa chini ya Katibu Mkuu mzigo William Mkama mwaka 2012 mwishoni katika kikao cha nec kilichofanyika DODOMA . Katibu Mkuu Mzigo Mkama aliondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Abdulrahmani Kinana na Mwigulu Nchemba akakabidhiwa Jukumu kubwa zaidi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara.
Ambapo aliendelea na wembe ule ule na kasi ile ile ya kuyasimamia matakwa ya Chama cha Mapinduzi na watumishi wake huku akiwa kipenzi bora cha wafanyakazi wa Chama cha Mapinduzi kuwahi kutokea amekuwa kiongozi wao msikivu asiye na majivuno mwenye kufikika kirahisi kuliko kawaida na kudhibitisha malezi ya kifugaji alikokulia.
Mwaka 2014 nyota yake ya mshale iliendelea kulenga bila kukosa baada ya Raisi kumpa jukumu lingine zito kuwa Naibu Waziri wa fedha waswahili wanasema kipele kimepata mkunaji kwa maana wizara ya fedha imepata mtu sahihi. Mwigulu Nchemba ni mtu sahihi kwa wizara ya fedha kwa maana mbili.
Kwanza tayari amekwisha fanya kazi Ofisi ile ile kwa miaka zaidi ya sita, amesomea uchumi na fedha ndio kitu anachokisimamia ukichukua sifa hizi mbili za kosomea na kufanya kazi katika Wizara hiyo unampata Waziri aliyebora kabisa kuwahi kutokea hapa Mh. Raisi aliona kitu.


UZALENDO NA UJASIRI WA KUTHUBUTU..

Katika Wizara hii ndipo nilipoubaini uzalendo wa Mheshimiwa Mwigulu Nchemba pamoja na uthubutu wake akiwa katika Wizara hii ndipo alipobuni kauli mbiu ‘’mabadiliko ni vitendo’’ jambo lilimsikitisha ni kuona Vijana wengi waliopo kwenye nafasi za utumishi wa uma wamekuwa wanafiki na wasiopenda kuwakomboa wenzao, hasa kutokana na ukweli kwamba Vijana wengi wenye dhamana ya kubuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuikomboa jamii wamekuwa wabunifu wakubwa wa matukio yasio na tija ni rahisi sana kusikia Family Day ya Tasisi fulani walibuni kujifanyia event imetumia million 160 Lakini hao hao ukiwaambia tafuteni hela ya madawati haipatikani.

Pia amekuwa mpingaji mkubwa wa sikukuu zisizo na maana aliwahi kuzitaja sikuku 60 zinazotumia gharama kubwa pasipo na tija mfano sikukuu ya kunywa maziwa, siku ya kansa, sikuku ya motto wa afrika wiki ya kuhamasisha akina mama kunyonyesha. Sikuku zote hizi na nyingine zaidi ya 60, amekwisha tangaza Wizara ya fedha haitatoa fedha katika sikukuu zisizo na tija.
Ni katika wakati huu amejipambanua na amethubutu kukamata walipa kodi kwa kuwafuata pamoja na polisi amejivika vita ya sokoine hali iliyosababishwa kubatizwa jina la utani sokoine amekuwa akikerwa na vitendo vya wakwepa kodi huku akikaliliwa akisema kama kodi katika Taifa hili ingekusanywa vema hakika Taifa lingejitegemea Kiuchumi na sio kuomba omba.

Amepingana wazi wazi na suala la mishahara hewa na kuokoa kiasi cha shilingi Bilioni 40 ambazo zilikuwa zinapotea kila mwezi kwa mda mfupi amekuwa mwiba kwa wara rushwa huku fedha hizo zikielekezwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu waliokosa mikopo. Huku ni kuthubutu kwa kiwango cha juu.
Hakuishia hapo anakelwa na kuongozeka kwa pengo kubwa baina ya walio nacho na wasio nacho amekuwa wazi na kuonekana kukerwa na hali hii huku akitoa suluhisho sahihi ya kupunguza pengo hilo ni kutoza kodi kwa (matajiri) walionacho na kupeleka huduma kwa wasionacho (maskini) na sio kuwatoza kodi wasionacho (maskini) kuwapelekea huduma walionacho’’ (matajiri) hii haikubaliki chini ya kijana huyu shupavu Mwigulu Lameck Nchemba akiwa ametokea familia ya kimaskini hakubaliani na utaratibu wa kuwakamata na kuwatoza kodi wafanyabiashara wadogowadogo kama vile mama lishe wamachinga, n, k katika Taifa lenye rasilimali nyingi kama Tanzania.

Kwa kifupi ni mtu anaeguswa na maisha ya watanzania anajua watanzania wanataka nini kwa sasa hajawa na nafasi kubwa ya kufanya maamuzi yatakayogusa watanzania moja kwa moja ila ameshauri na tumeona busara zake, hekima zake, na uzalendo wake, amethubutu kukamata wakwepa kodi, amethubutu kudhibiti mishahara hewa na billion 40 zimepatikana chini ya mkakati huo na fedha hizo wanafunzi kupewa mikopo, amethubutu kutofautiana na msimamo hata wa Chama chake alipotaka bunge la katiba liairishwe lisije huko mbeleni likashindwa kupata theruthi mbili. Na watanzania wameona hali ilivyokuwa ngumu kupatikana kwa theluthi mbili na kizungumkuti chake. Ndio maana kuna wakati anatamani kugombea nafasi ya Uraisi kudhibiti mambo mengi yanayokwenda bila mpangalio, katika tasisi nyingi na kudhibiti Rushwa iliyokithiri katika Taifa letu.
Huyu ndio Mwigulu Nchemba kipenzi cha wana Iramba wanasingida kipenzi cha Vijana na kipenzi cha wanaCCM Mungu amjalie maisha marefu naliona Taifa limepata kijana jasiri asiye na nyongo ya uoga …

JAMBO LA KUSHANGAZA

Ni pamoja na wadhifa wake kua mkubwa ndani ya serikali na chama Mwigulu Nchemba ameendelea kuishi maisha ya kawaida hajabadlika chochote tangu akiwa bank kuu mpaka sasa Naibu Waziri wa fedha, tofauti na wenzake ambao wakipata uongozi hubadilika. Maisha yake akiwa Dodoma na popote ni ya kawaida humkuti Mwigulu Nchemba akila Dodoma hoteli au hoteli za nyota, ameendelea kula ugali dagaa na maziwa ya mgando kwa mama lishe pale area C Dodoma utamkuta kapaki gari yenye namba za usajiri F maana yake waziri wa fedha usidhani dereva wake kapaki anakula bosi hayupo ingia ndani utamkuta mtoto wa mfugaji Mwigulu Nchemba anakula huku akitaniana na walala hoi kuhusu mambo mbalimbali ya michezo siasa na maisha kwa ujumla, Mara ya mwisho nilipomkuta nilimuuliza Mheshimiwa kwa nini unakula huku uswahilini alicheka na kunijibu “napenda kula chakula kilichonikuza” lakini hapa ndipo nakutana na watanzania sahihi wanaoweza kukueleza ukweli na nini wanatamani serikali yao ifanye. Nilipomuuliza mbona upo peke yako dereva wako yupo wapi alitabasamu kisha akasema ahaa kapata posho labda kaenda kula Dodoma hoteli.

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba, 0757023523
 
Back
Top Bottom