Huyu ndiyo Bruce Lee

Alifundishwa wing chun na Yip man baada anasema traditional martial arts huwa ziko rigid zina kufunga kufanya baadhi ya mambo kwenye fight.

Mfano: wing chun ilikuwa haina high kicks pia haikuwa na wrestling techniques mwamba akaona avumbe new style ambayo ni jeet kune do(the way of intercepting fist or a kick kwa mujibu wake)


Jeek kune do(JKD) alibidi aiongeze vitu kutoka western boxing,grappling techniques,stance kutoka art moja inaitwa Fencing na mambo kibao ili tu kuweza kupambana mazingira yoyote Yale ambayo baadhi ya Chinese traditional arts zilikuwa hazina.

Bruce alisema "absorb what is useful and reject what is useless" akaenda mbali zaidi akasema "Use the way as no way"

Kwa mtu ambae ni martial artist mzuri anaelewa mchango wa Bruce Lee kwenye hii mambo.

Ahsanteni.
 
Kwahiyo usipopenda muvi za Bruce Lee ni mshamba sana? Dah! Nilikuwa sijijui aisee, hahahahaha
Kuna siku nikawa na jamaa nikasema,muziki anaoimba Buna boy cjui mimi haunivutii na wala haukuwahi kunishawishi hata siku moja,basi nilipokea kila aina ya kejeri kwamba sijui lugha ndio maana siuelewi.

Nilistajabu sna,watu watambue binadamu kila mtu anapenda chakwakwe na wala tusibadiri maana kuwaona washamba .

Mimi ninavyovipenda wewe huwezi kuvipenda.Sisi waislam tuna msemo yule mwanamke au mwanaume unaemuona wewe mzuri mwenzako anamuona mbaya na yule unaemuona wewe mbaya mwenzako anamuona mzuri.Ili mradi kila mtu apate wake.

NB;KILA MTU APENDE VYAKE
 
Tatizo la humu WAKUJA ni wengi sana. Sasa ili waonekane wanajua wanajifanya kushobokea kila kitu na kushabikia hata wasichokijua, na ukionekana kupinga wanajionesha wajuaji na kujifanya wao ndio 'watoto wa mjini'. Hawajui nani ni nani humu, basi muda mwingine ni kuwadharau tu na kuachana nao. Wengine ukiwauliza hata sehemu maarufu za sinema hapa Bongo zilikuwa wapi hawajui? Ila anzisha mada zungumzia Avalon Cinema wataibuka kibao kujifanya walikuwepo na wanajua sana. Naishia kucheka tu...
 
[emoji16][emoji16][emoji16] mkuu hatimaye umetema nyongo
 
Sijawahi kuzipenda wala kuzielewa muvi za huyu jamaa
Uwongo dhambi.
Mimi mwenyewe huyu jamaa hajawahi kunivutia wala movie zake sijawahi kuzipenda!
Mara mia niangalie movie za Donnie Yen nazikubali sanaa....! Haijalishi anajua kiukweli au vipi kama mawe acha wanipopoe tu kwakweli
 
Be like my friend. Hizo mbinu pia kwa normal unaweza zitumia
 
Ila kusema ukweli jamaa alikuwa Yuko mbali mno kwa fani iyo ama Ni uwongo. Hakuna aliyeivunja iyo rekodi mpaka kesho
Ofcoz.. ni kama kanumba hapa bongo au Mr. Nice kwenye mziki wa bongo..
 
Sekunde moja unaijua au unaisikia
 
Alikuwa na uwezo wa kupiga mateke tisa kwa sekunde moja, alipiga teke kiroba cha mchanga chenye kilo 135 na kuruka urefu wa futi tano kwenda juu. Alikuwa na uwezo wa kufungua kizibo cha soda kwa kutumia vidole viwili.
Kila nikirudi kusoma hapa, nacheka sana...........🤣🤣🤣
 
Hapana, movie zake ni local sana, ni mara mia niwaangalie Jet Lee, Do Yen na Jack Chan
Hapo mtu ambaye analeta ukweli kwa kiasi fulani wa mapigano ni Don Yen.
 
Bruce lee alikua mwenye kiburi, jeuri na kujisikia saana.. alijiona ndo mover wa chinese movie industry.. na hii ndo ilipelekea mwisho wake
Na kweli jamaa alikuwa na kiburi cha namna yake!
 
Kwa china ule upiganaji ulikuwa ni asili yao , ni utamaduni sasa yeye kaupeleka ugenini hili jambo halikukubalika.
Kung fu ni mchezo ambao umechelewa kusambaa ukilinganisha na michezo mingine ya mapigano. Sababu kubwa ndiyo hiyo uliyoitaja wachina waliofanya ni tamaduni yao ni siri yao hivyo haifai kurithishwa kwa mtu yeyote isipokuwa ni China pekee.

Unachosema ni kweli Bruce Lee alikataa hii kitu yeye aliona kung fu ni kama zawadi ya dunia hivyo si vyema kuifungia ibaki kwa wachina pekee yake bali kila mtu ana haki.

Matokeo yake aliingia mgogoro na ma-masta wengi wa kichina. Wengine walikuwa wanasafiri kabisa kutoka China mpaka Marekani kumpa onyo!

Ila Bruce alikuwa kiburi wa namna yake! Aliwaambia ma-masta yeyote atakayenipiga nitaacha kuufundisha huu mchezo!

Kwa bahati mbaya ma-masta walishindwa kumpiga walikuwa wanachezeshewa kichapo wao.

Ila mwamba Bruce Lee kiuhalisia anapiga! Yupo vizuri! Kuna mambo anafanya ya ajabu sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…