Kwa hivyo tukitazama kwa umakini video hii imepigiwa maeneo ya pwani kwani unaweza kusikia upepo ukivuma ktk microphone na pia miwani aliyovaa jamaa inaakisi bahari ya buluu na mchanga wa ufukweni pwani.
Hivyo vyombo vya usalama vinaweza ku-''zero'' ni maeneo gani video hii imechukuliwa na ni jengo/nyumba gani iliyo mkabala kabisa na ufukwe wa pwani yenye madirisha yasiyopungua mawili huku ikiwa na chumba kikubwa kisicho samani (fenicha) nyingi kama inavyokuwa reflected na miwani ya huyu jamaa.
Pia uso wa huyu jamaa haujazibwa vya kutosha pia ana kijikovu usoni hivyo jamii inayomzunguka inaweza kumtambua hasa hasa majirani, waliosoma nae shule, wasomajiwa GlobalPulishers na watumiaji wa mitandao.