Huyu ndo Mkuu wa Majeshi ambaye watu wanaweza kujivunia kuwa naye

Huyu ndo Mkuu wa Majeshi ambaye watu wanaweza kujivunia kuwa naye

Ni General Dan Caine, mkuu wa majeshi ya Marekani [Chairman of the Joint Chiefs of Staff].

Nimemtazama na kumsikiliza leo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika baada ya operesheni ya kumkamata Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ilipomalizika kwa mafanikio.


View: https://youtu.be/qe2RuYI8KZY?si=jW9g514EO5u_65aS

Ukiambiwa kwamba huyu jenerali ni msomi na anajua anachokifanya kwenye hiyo kazi yake, halafu umuone anavyoelezea namna walivyoifanikisha hiyo operesheni, ni lazima utakubali tu kwamba jamaa ni “kichwa”

Anaongea kwa kueleweka bila kigugumizi wala kujing’ata ng’ata.

Hata akiwa anasoma, anasoma hayo maelezo kama mtu ambaye ni msomi aliye na elimu ya juu.

Sasa hebu jaribu tu walau kidogo kumlinganisha General Caine na Jenerali Mkunda 🤣.

Nina mashaka sana na elimu ya Mkunda……seriously!

Ulishaaema, au umesahau; “Miafrika Ndivyo Tulivyo”
 
Back
Top Bottom