Huyu ni mmoja tu; hebu fikiria Watanzania 10 wangefanya hivi ni wawekezaji au wafanyabishara wangapi tungewavuta kuja hapa nchini?

Watu wamekimbia huu uzi. Ila una ujumbe safi kabisa. Shida sasa unaweza pambana hivo, kurise awareness kuhusu nchi yako, alafu system ikagoma speed🤣🤣🤣. Inataka kula tu
Ni kawaida yetu ,, sisi tunapenda kuchangia mada nyepesi,, tutajaa sana kama inzi kwenye kinyesi na kuchangia pindi utakapo tuuliza kati ya ambaruti na gigy money nani anat*ko kubwa ,, hapa mwenyewe utakubali uchangiaji wetu
 
kwahiyo unaona hii ni habari mpya. amka
unajua kenya wananunua asali front kabisa ,yaani wanaenda wenyewe katavi na sikonge wanaenda ku process na kuuza kwenye soko la nje
parachichi zinauzwa china kupitia kenya na wanasema ni vya kwao
Wananunua machungwa mengi Sana hapo Tanga, muheza, korogwe etc na kupeleka kwao kutengeneza juice na kutuuzia
 
watu tumeandika sana. kuna lingine kwamba mlima kilimanjaro upo kenya. hilo nalo hulijui?
tatizo la nchi hii ukifanya kitu unaonekana unamsema rais na unaweza kutekwa
 
watu tumeandika sana. kuna lingine kwamba mlima kilimanjaro upo kenya. hilo nalo hulijui?
tatizo la nchi hii ukifanya kitu unaonekana unamsema rais na unaweza kutekwa
Nalijua ,, kenyans are the go getter ,,, yani watu wa fursa kweli kweli ,, lakini hii hutokana na sisi watanzania kuzubaa,, Kenya hupenda kuita Tanzania " The sleeping giant "

Kwa case ya mt kilimanjaro ipo hivi
Asilimia 90 ya picha za mlima kilimanjaro unazoziona zinasambaa mitandao ni picha zilizopigwa Kenya katika mbuga ya amboseli ,, hii hupelekea wengi waone huu mlima ni kama wao tu ,,, ikiachilia hivyo wakenya waliowengi waliweka picha za mlima huu kwenye profile zao na hata majumbani mwao ,,, hii ilipelekea wageni wengi waamini huu mlima pia ni wa Kenya ..

swali langu kwako ,,wewe unapicha yeyeto ya mlima huu hapo kwako au hata kwenye profile yako ???

Najua tu : haunaaa

Okay ipo hivi

Wakenya wengi wanataarifa za kutosha juu ya Tz ,, wakati watz hatuna taarifa yeyeto juu ya kenya ..
 
kwahiyo unaona hii ni habari mpya. amka
unajua kenya wananunua asali front kabisa ,yaani wanaenda wenyewe katavi na sikonge wanaenda ku process na kuuza kwenye soko la nje
parachichi zinauzwa china kupitia kenya na wanasema ni vya kwao
Hivi sisi kama nakumbuka kulikua kuna vikwazo vya kuuza parachichi China sijui walisha reach agreement?
Kenya wanafanya sana biashara ya mazao nje ya nchi mpaka raha.
Lakini Tanzania vikwazo vingi sana vibali kama vyote..
Ndo maana wafanyabiashara wengi wenye mitaji mikubwa wanafungua makampuni kenya.Kenya ipo friendly kwa wawekezaji wa nje na ndani.
 
Ninashamba dogo tu. Nimewahi lipist humu.
Kuna ule uzi wa "kilimo cha parachicho hakina faida."
Mimi nina mashamba mengi sijayapanda kama unaweza kujitoa mhanga njoo tupande, zopi heka 25 hazijapabdwa bado ila mi hamu sina nimeishia kupanda heka 3tu. Kilimo cha parachichi kinachangamoyo nyingi. Karibu kwa mazungumdo zaidi.
 
Ungesema na nguvu unazo ingekuwa poa sana. Mashamba yapo Kifanya na hapo katikati kabla hujafika kifanya. Kama una nguvu njoo uweke nguvu.
Shamba moja ouna udongo mzuri unastaei tikiti, karanga, maharage, mahindi, avocado, papai, viazi mviringo, maboga nk.
Yaani kika kitu kinastawi.
Kama una nguvu na upo serious njoo tufanye kazi.
Mifumo ya maji ipo.pampu ya dizel nchi 3, pipe 2 roller 3. Kama unajitaguta njoo tuanze na bustani ya nyanya mwezi sept na kama ushajipata haina shida. Ni kazi ya kujitoa kufa na kupona. Kama upo serious njoo pm.
 
Kiuhalisia mlima upo Kenya, kisiasa upo Tanzania.
 
Ahaa ok mkuu nimekupata nitakucheki asante sana kwa introduction naona kitu kikubwa hapo......
Blessed!
 
Serikali imewekeza kwenye kununua chawa wa kusifia viongozi badala ya kutangaza nchi kupitia ushawishi walionao mitandaoni, mimi nijitutumue kuelezea mazuri ya nchi ambayo muwekezaji akipatikana kodi zinarudishwa kufadhili chawa. Haya ni maajabu, kila mtu ashinde mechi zake, tule kulingana na urefu wa kamba zetu
 
Utasikia wapuuzi wa humu wanakuambia tumewazidi wakenya kila kitu mara kati ya Nairobi na dar wapi kuzuri
 
Una uzoefu na kilimo cha nyanya?
 
Ajichanganye tu, atapigwa mpaka achakachae. Wanavyosikia kuwa Kenya wana import yeye anadhani wana import kwa Whatsapp?
Kama ana huo muda wa kuja kushinda huku na watanzania tangu maandalizi hadi mavuno basi ni vyema
 
H
Huyu Sio Mteja wa parachichi atakuja kuya binya binya ayaache
 
Huwa sielewi shida yetu ni nini, Nchi yetu idadi ya wasomi inaongezeka kila Leo lakini ujinga hauiishi. Sisi tuna mazao ya biashara mengi sana lakini hatujui wapi tumekwama na serikali haijali.
Tuko na wasomi wengi wa kukariri makaratasi ila zero competence,hii inatufanya tuwe nyuma sana kwenye jambo lolote linalohusu ushindani wa kimataifa
 
Hao ndiyo kikwazo.....

Kiko kwa ajili ya kuwa kombatia
Watu wachache tu

Ova
Mfumo wetu ni wa kibepari japo tunajifanya wajamaa. Serikali iko radhi watu hao hao wachache wafaidike kuliko mfaidike wengi. Nilitaka kutuma kahawa nusu kilo kama sample iende marekani nilishindwa sababu itanicost 300k kibali cha ku export. Imagine
 
Mfumo wetu ni wa kibepari japo tunajifanya wajamaa. Serikali iko radhi watu hao hao wachache wafaidike kuliko mfaidike wengi. Nilitaka kutuma kahawa nusu kilo kama sample iende marekani nilishindwa sababu itanicost 300k kibali cha ku export. Imagine
Kweli kabisa,mfumo unabana

Ova
 
nashukuru siko tz.
mambo ya nchi yangu yalinichosha. kabla ya serikali watz wenyewe ni wana utapeli wa kishamba na uchawiuchawi
 
Tuzidi kuelimishana kuhusu jambo hili na mengine yanayofanana na haya pasipo kulaumiana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…