Huyu ni Mungu wa aina gani anaacha niteseke kiasi hiki?

Huyu ni Mungu wa aina gani anaacha niteseke kiasi hiki?

Luteni Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2019
Posts
337
Reaction score
312
Wakuu
Najitahidi sana kufanya kazi kwa bidii kwa miaka kadhaa hapo nyuma mpaka leo mwaka wa tano huu bila kutetereka.

Kama ni kuumia nimeumia sana. Kuna muda nafikia stage najiuliza ya kwamba hivi kama yupo MUNGU wetu tunayemuabudu, kumuimba na kumsifu kila uchao, je anaweza niacha naendelea kuteseka namna hii?
 
Bado unauliza ni Mungu wa aina gani wakati unakula, na kushiba na una viungo vilivyokamilika vya kukuwezesha kujipatia riziki?

Always unapojisikia upo desperate, ama haupo unapotaka kuwepo maishani hebu waangalie wa chini yako. Angalia wanavyostruggle. Halafu mlani shetani na umshukuru Mungu kwa alipokufikisha.
 
Kuna wakati sisi binadamu tunapo fikia kikomo wetu wa kufikiri au kutatua changamoto hapo ndipo mungu huanza kufanya kazi, na uonapo giza limekuwa kingi ujue kupambazuka kumekaribia.

Pole ndugu kwa uelewa wangu mdogo jaribu kubadili badili mbinu za kupambana ila usitoke kwenye malengo. MUNGU NI MWENA SIKU ZOTE HUTENDA MAMBO AMBAYO MWANADAMU AMEYASHINDWA
 
Kula kunywa kulala sio Mambo yote Mtu anahitaji ziada ambayo itamsaidia apatapo tatizo pia anahitaji kujimwambafai kwa matokeo mazuli yajuhudi zake.

Mkuu umejituma kwa juhudi ukayaacha maalifa
 
Daah.! Wakuu najitahidi sana kufanya kazi kwa bidii kwa miaka kadhaa hapo nyuma mpaka leo mwaka wa tano huu bila kutetereka kama ni kuumia nimeumia sana kuna muda nafikia stage najiuliza ya kwamba hivi kama yupo MUNGU wetu tunaemuabudu,kumuimba na kumsifu kila uchao je anaweza niacha naendelea kuteseka namna hii.
Mbona huangalii neema ulizojaaliwa unaangalia ambavyo huna?

Hapo wewe sio mzima wa afya? Kuna watu wana pesa kibao lakn hawafaidi maisha hata kidgo kutokana na maradhi yanayowakumba, ww mpk unamiliki smart4n na kuweza kuweka bando na kuchati jf unajiona una hali ngumu?

Binadamu tumejaaliwa neema nyingi sana lakini kazi yetu ni kuangalia tumenyimwa nn, Mungu atusamehe sana.
 
Mbona huangalii neema ulizojaaliwa unaangalia ambavyo huna?
Hapo wewe sio mzima wa afya? Kuna watu wana pesa kibao lakn hawafaidi maisha hata kidgo kutokana na maradhi yanayowakumba, ww mpk unamiliki smart4n na kuweza kuweka bando na kuchati jf unajiona una hali ngumu?

Binadamu tumejaaliwa neema nyingi sana lakini kazi yetu ni kuangalia tumenyimwa nn...mungu atusamehe sana.
Hakika japo tunapitia magumu mengi but nimejifunza kujipa uvumilivu ndo silaha mkuu.
 
Kuna wakati sisi binadamu tunapo fikia kikomo wetu wa kufikiri au kutatua changamoto hapo ndipo mungu huanza kufanya kazi, na uonapo giza limekuwa kingi ujue kupambazuka kumekaribia.

Pole ndugu kwa uelewa wangu mdogo jaribu kubadili badili mbinu za kupambana ila usitoke kwenye malengo. MUNGU NI MWENA SIKU ZOTE HUTENDA MAMBO AMBAYO MWANADAMU AMEYASHINDWA
hakika mkuu shukran
 
Kula kunywa kulala sio Mambo yote Mtu anahitaji ziada ambayo itamsaidia apatapo tatizo pia anahitaji kujimwambafai kwa matokeo mazuli yajuhudi zake.

Mkuu umejituma kwa juhudi ukayaacha maalifa
hakika hio ndio maana yangu mkuu umemjibu vyema
 
Kuna muda huwa tunamlaumu Mungu bure tu.

Wengi wetu tumekosa mipango na nidhamu ya pesa.
Mtu anataka afanikiwe na wakati huohuo awe anakula bata kila akipata kichache, ni kweli inawezekana lakini si kwa wote, si kwa kipato tunachpata wengi.
 
alafu mwishoni unatuambia 'sina hela ya kul' sijui 'nimelala nyaa naomba msaada' wakati umetu 'bore' na kukufuru………….!
Ni wapi nimekufuru mkuu rudia tena kusoma thread.
 
Always nasema kuwa pamoja na mapambano makali ya kutafuta kufanikiwa maishani,but always msimamo wangu utabakia kuwa katika maisha KUFANIKIWA NI BAHATI..haijalishi nani anaisababisha hiyo bahati,but ukweli kama hauna BAHATI mafanikio sahau...kuna wengi hata hawapambani kiivyo na wanatoboa,na weeengi wapambanaji huwa wanakufa wakiwa na average life,tofauti na matarajio ambayo walikuwa wamejiwekea maishani..
 
Daah!

Wakuu, najitahidi sana kufanya kazi kwa bidii kwa miaka kadhaa hapo nyuma mpaka leo mwaka wa tano huu bila kutetereka kama ni kuumia nimeumia sana kuna muda nafikia stage najiuliza ya kwamba hivi kama yupo MUNGU wetu tunaemuabudu, kumuimba na kumsifu kila uchao, je anaweza niacha naendelea kuteseka namna hii?
Mungu hawahi wala hachelewi, endelea kuvuta subira
 
Always nasema kuwa pamoja na mapambano makali ya kutafuta kufanikiwa maishani,but always msimamo wangu utabakia kuwa katika maisha KUFANIKIWA NI BAHATI..haijalishi nani anaisababisha hiyo bahati,but ukweli kama hauna BAHATI mafanikio sahau...kuna wengi hata hawapambani kiivyo na wanatoboa,na weeengi wapambanaji huwa wanakufa wakiwa na average life,tofauti na matarajio ambayo walikuwa wamejiwekea maishani..
Hakika mkuu
 
Hivi mnamlalamikia Mungu kwa kipi..?
Mi nijuacho ye alishaliza kazi yake na ameacha system zijiendeshe!,ameshamaliza usitegemee atakuja akusaidi ondoa hichi kitu akilini mwako maana ye hayupo hivyo!.. jinsi mnavyomfikiria alivyo ni tofauti sana na hakika hatokuja kukusaidia isipokuwa wewe mwenyewe ujue utatoka vipi!.

Nothing can change na hapo usikute hana hata taarifa kuwa Kuna mtandao unaitwa jf na Kuna member anaitwa Luten Jr!,na huyo member anamlalamikia yeye Mungu!.
Ukweli ambao wengi hawataki kuusikia ni kuwa Mungu hana cha kufanya juu ya shida zako maana yeye pia ni sehemu ya shida hizo.!😅 Think and think again kilishagaumana kitambo sana lolote litakalokupata ukashindwa kulihandle na likashindikana kwa maarifa yetu trust me usitegemee muujiza.
 
Back
Top Bottom